Maafisa utumishi ambao ni approvers wa HCMIS wasiendelee kusababisha hoja hii ya ukaguzi, imekuwa zaidi ya kero

Maafisa utumishi ambao ni approvers wa HCMIS wasiendelee kusababisha hoja hii ya ukaguzi, imekuwa zaidi ya kero

Twilumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
12,576
Reaction score
14,522
Wakuu,

Nimepitia kwa uchache katika Ripoti Kuu ya Ukaguzi ya Serikali Kuu (MDA) Mwaka 2021-22 2020 ukiacha zile nyingine za LGAs na ya Mashirika, Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika ripoti hiyo iliyowasilishwa April Mwaka huu pamoja na mapungufu mengine alibaini;

Matumizi Yasiyoridhisha ya Mfumo wa Taarifa Shirikishi za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) ambapo alitoa mapendekezo, Nanukuu “Napendekeza taasisi za serikali ziandae mipango ya kutosha ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa HCMIS .Pia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ishughulikie kero zinazohusiana na ugumu wa matumizi ya mfumo huo ili kufanikisha kufikia lengo lake hatimaye kuongeza thamani ya fedha”

Kuna mifumo kama HCMIS Human Capital Management information system, mfumo huu ni mbadala wa mfumo wa awali wa Lawson, ambao umebuniwa na wazawa, lkn katika baadhi ya levels hasa ya Approve level imekuwa ni changamoto kubwa kwa hawa ndugu zetu wasimamizi wa raslimali watu. Unakuta request ya kumhamisha mtumishi ipo pending 3 months, mtumishi ameshahama taasisi moja (Vote) physically lkn kwenye mfumo wa HCMIS bado anasomeka kituo chake cha kazi cha awali yaani vote nyingine kwa maana nyingine, mtumishi analipwa mshahara na Vote ambayo haitumikii!

Uchelewashaji kama huu ndio haya ambayo CAG anasema Matumizi yasiyoridhisha ya Mfumo wa HCMIS, pamoja na kwamba wapo wengine katika levels mbalimbali lkn ambao mnaonekana kero na kujigeuza Miungu watu ni Approvers,

haya yanafanywa kwa maufaa ya nani?

Kwa nini inakuwa ninyi approvers mnakuwa kama Miungu watu?

Mnajijua kwamba mnatambulika kama Miungu watu, Je Mnataka tuendelee kuamini kuwa HRs wana Roho Mbaya, wabinafsi na wababaishaji?, ugumu wa HRs kukalia desk kwa walau dakika 10 Ku-log in PC kwa kubonyeza button ya Approve inawa cost muda gani?

Kwamba mpo Busy kweli mnashindwa ku attend pending za wateja wenu hadi 6 Months is it true? Kama kuna shida kwa nini Approver usi reject with reason kwamba u didn’t approved kwa sababu 1,2,3. Uzembe huu haukubaiki, haya ni malalamiko ya muda mrefu na hakuna hatua zinazochukuliwa na hii ni kwa sababu ya kufichiana haya mauchafu… Badilikeni Appovers wa HCMIS Mnawaharibia wanaowasimamia ambao wameaminiwa na Mh. Rais!

Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom