Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wale walikuwa ni wapuuzi tu! Makamanda mimi nasema hv, bila serikali 3 ni bora tusiwe na muungano wa kijinga namna hii. Patachimbika
Hao wasomi wamesahau kusema kuwa gharama za serikali moja ndio nafuu kuliko zote.
Kwa hiyo kwa akili zako zilivyo fupi Warioba anavyo tetea na kufafanua juu ya serikali 3 anasimamia upande wa CDM? Tambua 64% ya watanzania walipendekeza serikali 3 hivyo kwa kauli yako basi CDM ipo na wananchi tafauti na CCM unayoishabikia.
Hawa ni wana CCM ambao mlikwisha taarifiwa walikaa wakachakachua rasmu ya pili ya Katiba. Wanaongozwa na tumbo. Timu imeundwa na akina Mukandala,Bana na wachumia tumbo wengine kama Malyamkono yule Mganda Kyaka toka Misenyi!
ccm kwa uzoefu hawafanyi mambo kwa jazba. Mfumo bora kwa muungano wa Tanganyika na zanzibar ni serikali mbili na hawayumbi kuhusu hilo. Vyama vingine vina jazba na kuhamasisha wananchi kufuata njia isiyokua na maslahi kwa mstakabali wa taifa. Wasomi sasa wanazinduka usingizini wakati Warioba kashatoa pendekezo kutokana na maoni yaliyotolewa kwa jazba badala ya hekima. Yeye pia inaelekea ana jazba. Ni wajibu wa bunge la katiba kupiga tiktak wazo la serikali tatu na kubakiza mambo yote mema ya tume ya Warioba.
Kiuchumi, kwa nini si serikali moja? Tunataka kuona serikali ya tanganyika huru. No tanganyika, no zanzibar, muungano wa serikali mbili kwa faida ya nani? Kama sio manyang'au!