kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,742
Shule ya Msingi SEFANONI iliyopo katika Wilaya ya Manyoni Singida imeingia katika maajabu ya shule kuendelea kuwepo huku kukiwa hakuna mambo yanayowezesha uwepo wa utoaji wa taaruma katika shule hiyo kwani Mwalimu mkuu wa shule hiyo katika kikao cha Halmashauri kilichofanyika ili kupanga mikakati ya kuinua Elimu aliweza kuelezea kuwa shule yake ya SEFANONI ina WALIMU WAWILI TU yaani yeye na mwalimu mwingine, Shule ina MADARASA MAWILI TU, Shule ina IDADI YA WANAFUNZI 500, Ebu tujifikirie kwa idadi ya wanafunzi hawa, idadi ya Madarasa na walimu je kuna elimu inayotolewa hapo? na kusikitisha Afisa Elimu ametoa taarifa kwa msisitizo kuwa Serikali kupitia hii BRN wilaya imepewa kiwango cha ufauru lazima kifikie 68% na yeye amesema wao kama Wilaya wamejiwekea 70% ya Ufauru, Je kwa hali ya Shule zinazolingana na hiyo ya SEFANONI malengo hayo yatatimia au ni kuendeleza USANII katika suala zima la elimu hapa nchini?