MAAJABU mambo 6 ya kufahamu kuhusu sayari ya Venus iliyopo karibu na dunia

Sijakuelewa mzunguko mmoja wa siku za Dunia ni 243 na Jua 224.7 ina maana gani naomba unifafanulie?
 
Safi sana kwa kutufahamisha vzr.
 
Asante sana mkuu..... Na pia wanasema kua pamoja na mercury kua iko karibu sana na jua ila venus ndo hottest planet cjuh n kwanini ila
 
Inamaana Venus huzunguka kwenye mhimili wake kwa muda tofauti lakini pia huzunguka jua kwa muda tofauti? Nifafanulie tafadhali.
 
tungekuwa tunaish huko yaan kumumba wangetawala karne na karne uzao wetu ungeendekea kuwa maskini..maana tangu mkolon aondoke mpk leo cjui ingekuwa miaka mingapi
 
Sijakuelewa mzunguko mmoja wa siku za Dunia ni 243 na Jua 224.7 ina maana gani naomba unifafanulie?
Kujizungusha kwenye mhimili Dunia inatumia saa 24(siku 1) Venus inatumia siku 243(kwa hesabu za siku za dunia). Kulizunguka jua Dunia inatumia siku 365(mwaka 1) venus inatumia siku 224.7. Natumai nimefafanua mkuu...
 
Kuimaliza Siku moja ni ndefu kuliko mwaka duuh?
 
Duh inamaana siku mbili Venus ni miaka miwili huko....kwahiyo raisi magufuli angetawala siku tano tu....
Kumbe siku moja kwa bwana ni sawa na miaka elfu kwetu du naona bado hawajaipata hiyo sayari
 
Naongeza kidogo dunia inapouzunguka muhimili wake au nguzo yake mzunguko mmoja ikifika ilipoanzia itakuwa imechukua masaa 24 sawa na siku 1. Utakuwa umepata usiku na mchana
Kwa venus ikiizunguka muhimili au nguzo yake ikifika ilipoanzia itakuwa imechukua siku 243 za dunia,ikumbukwe hii ni mizunguko ya kuizunguka mihimili au nguzo zake c kulizunguka jua maana yake kuna mizunguko miwili
1. kuizunguka mihimili yake au nguzo zake
2. Kulizunguka jua usichanganye mizunguko
Kulizunguka jua dunia hutumia siku 365 sawa na mwaka 1 maana yake dunia ifike ilipoanzia

Venus ikilizunguka jua ikifika ilipoanzia itakuwa imetumia cku 224.7 za dunia
Maana yake mwaka wa venus ni mfupi kuliko wa dunia
Na kwamba venus ina speed kulizunguka jua kuliko dunia
Na kwa mahesabu ya kuizunguka mihimili dunia ina speed kuliko venus
Nafikiri mkuu umenielewa nimeeleza kwa kirefu kama kuna wanaofaham zaid waongeze elimu haina mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…