SoC03 Maajabu matatu (3) yenye nguvu ya kutisha yaliyoifanya familia masikini kuikopesha Marekani

SoC03 Maajabu matatu (3) yenye nguvu ya kutisha yaliyoifanya familia masikini kuikopesha Marekani

Stories of Change - 2023 Competition

Isleter BM

New Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Hapo zamani za kale pembezoni mwa upwa wa bahari ya hindi kulikua na familia ya wabantu. Familia hiyo kwa umaarufu wake wa kumiliki kila aina ya vito vya thamani hata vile visivyoweza kupatikana kwa malimwengu yote yaani tanzanite, vilipelekea familia za walowezi kutumia mabavu kujimilikisha aridhi ya familia hiyo. Baada ya kuchoshwa na hujuma za walowezi, Baba mmoja mwerevu na mwenye busara katika familia hiyo alifanikiwa kuikomboa milki yoote ya familia kwa stara kutoka kwa walowezi. Tarehe 9 Disemba 1961 Ilikua ni siku ya kihistoria ambayo haikutosha kuandikwa na kufundishwa katika mitaala ya historia ya familia ile bali walikubaliana kuienzi na kuikumbuka siku hiyo kila mwaka. Hata hivyo baba huyo alipata umaarufu kutokana na mbinu na umahili wake katika ukombozi wa familia, wanafamilia wakambatiza jina jipya “Baba wa taifa”

Kama ilivyokuwadesturi ya familia za kiafrika kabla ya ukoloni, familia moja iliungana na nyingine ili kulinda milki zao dhidi ya wanyama wakali, hata hivyo wahenga walisema “umoja ni nguvu utengano ni udhaifu”. Basi familia hiyo iliamua kuungana na familia jirani inayoishi visiwani katika bahari ya hindi kwani familia hizo zilifaana kweli kweli na kutimiza ule usemi usemao “akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli”.

Baba wa taifa kutokana na upendo aliokuanao juu ya familia yake aliweka mikakati ya kuimarisha ujenzi na kulinda milki za familia yake. Alianza na suala la maadili ya wanafamilia huku akiwaasa kuwa na umoja, uzalendo, uwajibukaji, utu na uadilifu katika ujenzi wa familia hiyo.

Kana kwamba haitoshi bila uchoyo, Baba wa taifa aliamua kutoa elimu sawa kwa wanafamilia katika sekta na nyanja zote za uwekezaji kwa maendeleo ya familia. Familia ikawa na wimbi kubwa la wataalam na wabobevu wa maswala ya utawala bora, siasa, uchumi, sheria, teknolojia, na elimu kiasi kwamba mpaka hivi leo wengine wamekaa tu mtaani na kusahaulika kuwa walisomeshwa kuitumikia familia yao kwa manufaa ya wajukuu. Kutokana na wingi wa wasomi na wataalam mbalimbali wenye ujuzi kutoka pande zote nne za dunia, nitakua sahihi nikisema kuwa hakuna andiko juu ya utawala bora na uwajibikaji ambalo halijaandikwa, hata hivyo familia hiyo imefanikiwa kuwa na waasisi na waandishi nguli wakuigwa kama vile Mwalimu J.K.Nyerere na kitabu chake cha ‘Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania”, Mkuki na Nyota Publishers, (2016), Benjamin W. Mkapa, Marehemu Jaji J.L.Mwalusanya katika jarida lake la “Matumizi ya Katiba na Sheria Zilizopo ili Kudumisha Utulivu, Amani and Mshikamano (1993)” naishia hapo kwani haitoshi kuwataja wote.

Kwa hiyo utakubaliana na mimi nikisema kuwa Andiko hili halitakua na ‘maajabu ya nabii Musa’ juu ya utawala bora na uwajibikaji katika ujenzi wa familia hii zaidi ya kuwakumbusha wazazi wangu juu ya mbinu za uhakika 3 zitakazosaidia kujenga nyumba yetu kwani nami ni mwanafamilia ili iwe nzuri zaidi ya falme za magharibi.

Ziko familia ambazo zinapitia katika kipindi kigumu cha maisha kama umasikini na migogoro mingi ya wenyewe kwa wenyewe mfano Sudani na Somalia. Hata hiyo suala hili linategemea sana aina ya familia, ziko familia ambazo wanafamilia wametengana na zingine zinaundwa na wanafamilia wasio wa asili moja hivyo kupelekea ubinafsi, ubaguzi, na unyanyasaji kwa baadhi ya ndugu kuongezeka. Lakini cha kushangaza ni hiki familia yetu ni moja, Baba wa taifa ni mmoja je tatizo likowapi? Kwanini hatutoki kwenye umasikini? Labda watoto si watiifu kwa wazazi au pengine wazazi wamewatelekeza watoto wao! Je hatuna utajiri wa kutosha kutufanya kuwa familia ya kwanza Afrika? Naamini utakua unatamani sana kupata majibu ya maswali haya haraka iwezekanavyo na majibu ni kama ifuatayo hapa chini: -
  • Familia inahitaji wazazi wazalendo na wenye upendo wa dhati. Hakuna wazo lenye manufaa mpaka lifanyiwe kazi, na maendeleo ya familia asilimia 100% hutegemea wazazi. Wazazi wanaoponda anasa huharibu matawi ya uzalishaji na hata mizizi, hali ambayo hupelekea usanii katika uwekezaji. Hatuna la kubadilisha zaidi ya utekelezaji, utawala wa sheria ndio utawala bora na uwajibikaji. Wageni wahatoijenga nyumba yetu kwa uwekezaji, zaidi wataiharibu na kujinufaisha kwa unyonyaji, Ni lazima tuwe wakali kwa kulinda zetu mali, kwani wanaubahili wa ujuzi toka enzi za sultani.

Wazazi wekeni maslahi kwa watoto, kwani sisi ndio taifa la kwesho. Msitupende kwa kupokea na kutugawia misaada ya kondom na uviko, wala kwa kukopa mikopo ya mateso, bali kwa kusikiliza maoni ya wazalendo.
  • Familia inahitaji wafanyakazi wenye maadili. Mashamba mengi ya familia yamekua na wafanyakazi wavivu, licha ya kwamba mafunzo yote wamefuzu. Hifadhi, Hospitali, Mamkala zote pamoja na bandari ya Dizim, hakuna kupalilia wala kumwagilia karibu kila msimu, hata mazao kidogo yapatikanayo wamekua wakihujumu, hebu tusihurumiane sana na tuwahukumu, waachie usukani mara moja ili nasi tulio mtaani tushike hatumu ya majukumu, ndipo nidhamu ya utawala bora na uwajibukaji itadumu.​
  • Familia inahitaji uhuru katika maamuzi. Tunahitaji umoja katika uwajibikaji, lakini uhuru wa mahakama ndio msingi wa uwajibishaji. Huu ndio mtaji pekee wa utawala bora na uwajibikaji, tukubali serikali kuu isihusike katika uteuzi wa majaji. Sina maana mihimili itengane katika kazi, bali wazo huwa na manufaa pindi linapofanyiwa kazi.​

Rushwa imekua ndio mtaji wa viongozi, mashtaka yamekufa kifo cha mende kisa kuchelewa kwa upelelezi, meno ya mahakama ni uhuru wa maamuzi, kama katiba ndio kizuizi tukubali ifanyiwe marekabisho kwa wakati.

Mwenye akili na afahamu andiko hili limetimia si kwa mahadhi ya shairi bali kwa Sanaa ya uandishi, halihitaji picha za ushahidi wala nukuu za wanafalsafa kwani yaliyosemwa yote yanatrendi. Bungeni, vyombo vya habari na wanaharakati wamekua wakiyajadili, Siogopi kuyataja yote ya SAG na Jamii forum, pengine wazazi wameziba masikio yao wasisikie ya redioni, lakini naamini macho yao yako wazi kulisoma andiko hili.

Maoni huru nimeyatoa taarifa kuwapatieni, uchambuzi yakinifu umefanyika juu ya utawala bora na uwajibikaji, uchunguzi ni wenu majaji kura namba moja kunipatieni. Tuijenge Tanzania yetu kwa kuthamini maoni ya wazalendo, hata hivyo kunausemi maarufu wa kizungu “Everything is wrong until proved”.​
 
Upvote 1
Back
Top Bottom