Maajabu ya baadhi ya makanisa: Wapo radhi kumwabudu na kumheshimu Mwamposa lakini siyo Bikira Maria kama vile alifanya kosa kubwa sana kumzaa Yesu

Maria mtakatifu mama wa Yesu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina

Lakini Yesu ni Mungu, Mungu mwana, katika lile fumbo la utatu mtakatifu ambalo ndiyo msingi wa imani yetu


Sasa ukilijua hilo, na kama wewe ni mkristu na ukiamini kwamba Yesu ni mwana wa Mungu na ni Mungu mwana katika utatu mtakatifu basi kuna ubaya gani tuki-address hivyo?

Yaani: MARIA MTAKATIFU MAMA WA MUNGU


Yeye Bikira Maria, siyo Mugu, ila Mungu mwana (YESU) alikaa ndani yake, tumboni mwakae miezi 9 na kunyonya maziwa yake miaka miwili, na kujifanya mtu ili aje kutukomboa
 
Jamaa alimkimbia mkuu😂😂😂
Ndipo akaotokea malaika akamwambia usimkimbie maria mkeo! Hiyo mimba ni kwa uwezo wa roho mtakatifu lkn kama ingekuwa kimya kimya jamaa alikuwa kashatembea MITA.

Yaani sahwwaaaaaaaaaah

Mathayo 1:19-20 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.


Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
 

Attachments

  • 20240707_155413.jpg
    57.7 KB · Views: 5
Point yangu ni kuwa maryam si mama wa Yesu.
Yesu exit kabla ya kiumbe chochote.
Muktadha huo maryam alimzaa vipi Yesu?
Maryam katumika kama njia tu fulstop.
Yesu katoka Ndani ya Mungu kama hawa alivyotolewa ndani ya Adam.

Zaburi 2:7 SRUV​

Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia, Wewe ni mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
 
Tatizo la ukatoliki hawana standard moja tu ya mafundisho ya imani kama madhehebu mengine ambayo huamini Biblia pekee ndiyo standard ya mafundisho ya Imani

Wakatoliki hawaamini kuwa Biblia pekee ndio kiongozi wa imani

Ndiyo maana wakaja na mafundisho ya ajabu kama ya kuomba marehemu wawe Maria prtro,yohana nk ambayo kwenye Biblia hakuna fundisho kama hilo

Pili haluna sehemu Biblia inasema Maria alipaa mbinguni wakatoliki wanaamini alipaa wakati kwenye Biblia hilo halimo
 
Kwa hiyo yale yalikuwa maigizo aliyoyafanya yesu kuzaliwa na bikra maria?
Yesu amekuwepo kabla ya kuzaliwa na maryam why maryam awe mama yake?. Wakati huo hajazaliwa na Maryam Mama yake alikuwa nani?.

Gal 4:4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na MWANAMKE , amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.
 
Kwanza nataka ujue kwamba Biblia ni vitabu vilivyoandikwa na watu ambao waliona au walifunuliwa mambo makuu ya ukombozi

Sasa, ni nani aliyempangia Mungu kwamba mwisho wa kuleta hayo mambo ulikua ni baada ya Biblia kuandikwa?

Mungu anafanya kazi yake kwa namna yake na hapangiwi kuleta taarifa na anaweza akaleta mtoto wake mwingine ikawa ni Yesu part two

Tuache kukariri
 
Sawli sasa. Yale yalikuwa maigizo? Yesu aliamua kutuhadaa?
 
Mtazamo wangu bikra Maria alikuwa binadamu , kupitia yeye muujiza wa kumzaa Yesu kama ilivyo tabiriwa zamani ukatokea..heshima yes, utukufu ni kwa Mungu, baada ya kumzaa Yesu, nothing special kiliendelea kwa Maria , hata kufa kwake Bible haijasema, which means kazi yake iliisha mara moja, hatakiwi kuabudiwa , hata kama iliabdikwa amebarikiwa kuliko wanawake wpte wa wakati huo Yesu kristo alipotaka kuja..kumbuka Yesu ni jina la kibinadamu ila kristo ndio nguvu iliyomo ndani ya Yesu , na ni Mungu ..na hata sisi tunapaswa kumpokea Yesu kristo mioyoni mwetu na sio Yesu tu...kwahiyo kwa wanao muabudu sijui mtazamo wao..na wasio muabudu haimanishi wanadharau au hawajui nafasi ya Mariamu.
 
Yesu alimkweza na we mkweze pia. Kumbuka kila kilichoandikwa kwenye bible ni mafundisho ili wenye macho waone unless kama huna macho
 
Anayeabudiwa ni Mungu peke yake. Ukimwabudu mwanadamu wewe utajibu siku ya Mwisho. Kristu ni Bwana kwa Utukuku wa Mungu Baba!
 
Yesu alimkweza na we mkweze pia. Kumbuka kila kilichoandikwa kwenye bible ni mafundisho ili wenye macho waone unless kama huna macho
Yesu akiwa duniani hakuagiza kuwa akifa tumuombe mama yake akifa atuombee huko kwa Mungu
 
Bikira Maria alikuwa Mwanadamu pia.
 
Anzisha dini yako sasa na wewe mana umegundua kitu kipya
Ukisema nianzishe Dini mpya maana yake unataka niachane na Kristo na nifuate kitu kingine.
Kitu ambacho sikiwezi abadani.
dhambi zote nilizonazo nimfuate nani sasa nje Yesu??
Wakati Yesu mwenyewe ashasema Yeye ndiye Dini ya kweli na Uzima!!. .
 
Sizani kama kuna dhehebu lolote la ukristo linafundisha kumpuuza na kutokumuheshimu Bikra Maria ispokuwa madhehebu yametofautiana namna yanavomchangamkia Bikra Maria tu ila heshima ya Bikra Maria iko palepale kwa kila dhehebu.
Huwajui walokole wewe. Hawataki kabisa kusikia habari ya Bikira Maria. Ukitaka kujua hilo, sikiliza mahubiri yao yote uone kama kuna siku watamtaja Bikira Maria. Wakifikia hapo huwa wanazima data
 
Jibu zuri kasoro hapo jina la Yesu ni la kibinadamu. Jina la Yesu sio la kibinadamu. Ni jina alilorithi kutoka kwa Baba yake. Hilo ndilo jina halisi la Mungu ambalo haikuruhusiwa hata kulitaja wakati wa agano la kale. Jina la Yesu sio la kibinadamu na ndo maana ukuu wa Yesu unaanzia pale alipoambiwa wewe ni mwanangu leo nimekuzaa, keti mkono wa kuume hata niwafanyapo adui zako kuwa kiti cha miguu yako na pia asema ni mkubwa kuliko malaika kadiri ya jina alilorithi lilivyo kuu kuliko lao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…