Maajabu ya baadhi ya makanisa: Wapo radhi kumwabudu na kumheshimu Mwamposa lakini siyo Bikira Maria kama vile alifanya kosa kubwa sana kumzaa Yesu

Siku ya mwisho ni lini ?
 
Kama Mungu aliamua huyo mama amzalie mwanae, wewe ni nani wa kutoa maneno ya kashfa kama hayo.

Ndugu yangu, muogope Mungu, huyo mama amebarikiwa kulika wanawake wote, thamani yake ni kubwa kuliko wanawake wote. Ni mama wa Yesu

Imagine Yesu anaposoma comment yako anakuchukuliaje?
 
Mungu ni mmoja tu kaka ni "Mungu" where does Yesu come from, Mungu ni Mungu bwana unaupeo mdogo sana wa kufikiria🤣🤣
Mungu ni Jina la office kuu yenye mamlaka ya juu na uweza kuliko mamlaka zote Mbinguni na duniani.

Mungu analo Jina tulilopewa WANADAMU lenye kuweza kuokoa ni Jina YESU.

YESU NI JINA LA MUNGU.

Muulize Roho mtakatifu akuthibitishie.

Unaabudu usichokijua.
 
Asa unawezaje kumtenganisha Bikra Maria na Roho mtakatifu ?
Bikira Maria ni binadamu tu wa kawaida....kumweka kwenye mzani na Roho mtakatifu ni kufuru.

Acha kabisa hili chief.
 
Bikra siyo ile physical hymen, which needs to be perforated, its pureness, Immaculate, with no sins

God can never dwell in a sinful person, so Virgin Mary is pure
 
Bikira Maria ni binadamu tu wa kawaida....kumweka kwenye mzani na Roho mtakatifu ni kufuru.

Acha kabisa hili chief.
Bikra Maria ana roho Mtakatifu ndani yake . Au roho Mtakatifu anaishi wapi kama sio ndani ya mwili wa mtu ?
 
Bikra Maria ana roho Mtakatifu ndani yake . Au roho Mtakatifu anaishi wapi kama sio ndani ya mwili wa mtu ?
Roho mtakatifu huishia ndani ya mtu ni kweli......na Roho mtakatifu ndiye mwenye uwezo wa kutusaidia kuomba mbele za Mungu na sio Mwanadamu Maria
 
Yesu wapi alitoa maagizo kuwa Yeye akifa na mama yake akifa watu wawe wanaenda kumuomba marehemu mama yake awaombee kwa Mungu au waende kuwaomba mitume waliokufa wawaombee kwa Mungu
Yesu baada ya kufufuka alowatokea mitume na watu mbali mbali na akawapa maagizo, ni sawa?

Maagizo hayo yakaandikwa kwenye Biblia, ni sawa?

Je baada ya Biblia kuandikwa, Yesu hajawatokea tena watu wengine na kuwapa maagizo?

Kama aliwatokea, maagizo hayo tunayaweka wapi?

Kanisa katoliki linaamini Yesu bado anafanya kazi, hajafa huko mbinguni, inapotokea mambo ambayo anashindwa kuvumilia anakuja anawapa watu miongozo kama kawaida, sasa ni juu yako wewe na mimi kuikubali au kuikataa

SIsi wakatoliki, tunao ma-padre ambao walikua na physical encounter na Yesu, mfano PADRE PIO, huyu mwamba alikua anapoke amaagizo kutoka kwa Yesu, AMEFARIKI LAKINI MWILI WAKE HAUJAOZA MPAKA LEO, hayawa mummified ni by grace of God


Yupo St. Maria Faustina, jifunze kuhusu Devine Mercy and how to recite the chaplet of Devine mercy
 
Nataka nieleweshe, Yesu ni Mungu?
Alipokuwa dunia alikua anamzungumzia Baba..je ni baba gani?

Mimi naamini Yesu kristo ni njia ya ukweli na uzima bila yeye siwezi kufika kwa Mungu(Yahwe,Yehova).

Hivi vitu usipotafakari vinachanganya..
Hoja za dini kuna hitaji kukosoa kwa hekima mana ni elimu pana.
 
Bikra siyo ile physical hymen, which needs to be perforated, its pureness, Immaculate, with no sins

God can never dwell in a sinful person, so Virgin Mary is pure
Hakuna mtu anakataa purity ya mtu kuzaa mfano kafunga ndoa hana dhambi hata moja na ni bikira

Ubikira wake utaondoka akiingiliwa na mumewe wa ndoa lakini aweza tu kuendelea kuwa pure na sio sinful sababu hajatenda dhambi bikira kuondoka lakini sifa ya kuitwa bikira haitakuwepo tena kwake

Kwa Maria ni vivyo hivyo alikuwa pure na bikira lakini baada ya kuzaa Yesu Bikira iliondoka ili Yesu atoke azaliwe

Kuondoka Bikira sio kuwa huyo mtu ni mdhambi la hasha akiwemo Maria

Kinachogomba hapa tofauti na ukatoliki na madhehebu mengine ni kukomaa tu kwa wakatoliki kuamini kuwa baada ya Maria kuzaa Yesu,huyo Maria alibaki bikira vilevile huo ni uongo tena uliokubuhu .Hakuna dhehebu nje ya ukatoliki linasema Maria alikuwa mwenye dhambi kumzaa Yesu kinachokataliwa ni jicho cha kusema Maria ni Bikira wakati kazaa

Bikira sio neno complicated la kisomi ni neno rahisi mno hata waswahili wasioenda shule wanajua na wanajua bikira huondokaje

Maria baada ya kuzaa ni Maria mama yake Yesu .Kusema Bikira Maria mama yake Yesu ni contradiction na utapeli.Mama mzazi wa mtu hawezi kuwa Bikira.Haipo hiyo.
 
Mkuu, kwa hivyo wewe ukitoa vitu tumboni unaondoa bikira ya kinyeo, maana yake wewe hauna marinda?

Ukianza kuingiliwa na blunt objects ndiyo hapo tunasema umetolewa marinda
 
Mkuu, kwa hivyo wewe ukitoa vitu tumboni unaondoa bikira ya kinyeo, maana yake wewe hauna marinda?

Ukianza kuingiliwa na blunt objects ndiyo hapo tunasema umetolewa marinda
Hueleweki uliichoandika Weka vizuri nikujibu
Au humu kama kuna aliyekuelewa afafanue vizuri unamaanisha nini
 
Siku ya mwisho ni lini ?
Hakuna ajuaye siku wala saa ila siku hiyo Mungu ndio atatangaza nani mtakatifu sio kama sasa kanisa katoliki linajipa mamlaka ya kutangaza nani mtakatifu na kuwaambia waumini dua zao wakaombe huko kwa huyo.marehemu mtakatifu wao waliyemmchonga k8wanda cha kutengeneza watakatifu Vatican

Tanzania tuko mbioni kupata mtakatifu mzanaki Marehemu Julius Nyerere watu waanze kumuomba Nyerere awaombee kwa Mungu
 
Walokole hamna uelewa wa ndani kuhusu siku za mwisho . Mungu anafanya kazi kupitia Kwa mitume wake ambao ndio hao Kanisa Katoliki . Ni jambo jema Nyerere kuwa mtakatifu.
 
NIPE andiko, ni wapi imeandikwa ndugu yangu,

Hivi nani amewaroga wakatoliki kudanganywa kuwa Mariamu hakufa?
Anayekuw ni mwenye dhambi. Kifo ni matokeo ya dhambi. Bikira alikingiwa dhambi ya asili
 
Hahaha dah mwanangu umenifurahisha sana kwa hili andiko. Vijana wa leo wangemwita Yusufu SIMP..
 
Mtakatifu Yosefu Anapewa Heshima Kubwa Na Kanisa Katoliki Kote Ulimwenguni.

Soma Litania Ya Watakatifu Wote.
 
Walokole hamna uelewa wa ndani kuhusu siku za mwisho . Mungu anafanya kazi kupitia Kwa mitume wake ambao ndio hao Kanisa Katoliki . Ni jambo jema Nyerere kuwa mtakatifu.
Mungu Wapi aliwapa mandate au nguvu ya kisheria yaani power of attorney ya wakatoliki wao kutangaza binadamu yupi mtakatifu kabla ya kiyama ambacho Mungu mwenyewe kiyama kikifika ndie atasema yupi mtakatifu na yupi sio
Na kuwa ombeni kwa marehemu the so called watakatifu waliozalishwa na kiwanda cha kufyatua watakatifu Vatican

Sasa hivi kiwanda Vatican kinajiandaa kufyatua mtakatifu mpya Julius Kambarage Nyerere aliyepora mali za watu waliozipata kihalali kwa jasho lao kipindi cha azimio la Arusha na kutaifisha shule za kanisa katoliki nk walizojenga kwa jasho la sadaka za waumini na kuzifanya za serikali wakati serikali haikuwekeza hata shilingi moja Leo kiwanda cha Vatican kinataka ku process mtakatifu mpya Julius Kambarage Nyerere mtaifishaji shule za kanisa katoliki nk

Inauma sana hata mkizomea walokole kuna maeneo wakatoliki vichwani wako sifuri hata kama wako Vatican

Nyerere naye wa kuingizwa kiwanda cha ku process watakatifu Vatican kweli

? Something is wrong in Vatican
 
Kwa mantiki hiyo ata sisi binadamu tuna uungu kwa sababu tumeumbwa na Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…