Maajabu ya Corona Tanzania: Badala ya Madaktari Bingwa wa tiba kuliokoa Taifa, ni Bingwa wa Kemia ndiye analiokoa Taifa kwa ushauri wa kikemia


Tatizo la huyu Mkemia Bingwa na Mkuu wa nchi huwa hachagui cha kuxungumza...!!Kuropoka na kupayuka ndo TABIA na ASILI yake na kwa kawaida TABIA haina Dawa!!!
 
Huyu nguli wa kemia fani anayoweza kuimudu sawa sawa ni kwenye mabarabara tu huku kwingine chenga tu.Naodha karudi
 
Matamko yake yamekua hatari kuliko hiyo Corona yenyewe sio nafuu yoyote kwa Watanzania akiongea bora akae kimya tuu akijenga Uchumi wa Nchi kipindi cha janga la Dunia..
 

Jibu maswali yafuatauo:
  1. Je,umeshawahi kujifukiza na maji ya Moto yanayochemka kwa joto la nyuzi 100 Celcius?
  2. Je,umeshawahi kunyonyoa kuku kwa maji ya Moto yanayochemka?
Ukinipa hayo majibu 2 njoo tuendeleze hii hoja mfu ya kujifukiza! Kwa kifupi ni hoja ya kipuuzi na ulaghai mtupu!
 
Haya Mzee mzima na Msaidizi wa Mkemia Bingwa Tanzania kama wewe umemwelewa hebu jaribu ku-share huo ufafanuzi wa utafiti huu! Karibu.
Kwenye ugonjwa Wa aina ya corona, siraha yoyote unayoshauriwa kutumia, tumia. Mtu hawezi kukushauri kitu ambacho hakijawahi kutumika huko nyuma.

Ni kwa sababu ya ubishi watu tunashindwa kutumia shauri mbalimbali ambazo waafrika wenzetu walioexperience huu ugonjwa huko ulaya wametumia na wamepona.

Ukiuliza wangapi wanajiandaa kuimarisha kinga kwa kutumia limau na maji ya moto au mchanganyiko Wa tangawizi na limau kabla ya kukumbwa na corona sijui kama utawapata.
 
Kuhusu Kujifukiza Sipingani na Mkemia Rais Dokta John Pombe Maghufuli.

Ninahisi Nilipona Korona Kwa Kujifukiza. Nilipata Homa Kali ikafuatiwa na Kikohozi Kikali Sana.

Mfukizo ulikuwa na limao na maganda take, Tangawizi na Kitunguu Saumu.

Mfukizo uliletwa ndani ya sufuria nami huku nimekaa mkao wa kibudha nikajifunika na Blanket huku Sufuria yenye mfukizo ikiwa ndani ya blanket inaleta mvuke mwingi puani. Nikawa navuta mvuke puani nautoa mdomoni Mara kadhaa.

Hakika Nilipona usiku ule.

Mungu ametubarikia Mimea tuitumie kwa Afya Zetu.

Mungu awabariki.
 
yaani hiyo ni pure stori ya vijiweni ajabu imeletwa na rais
 

Saharavoice,
I beg to differ with you.
Unaposema kuna wenzetu huko Ulaya Wana experience ya kutumia huu UFUKIZAJI, MCHANGANYIKO WA LIMAU, TANGAWIZI NA MAJI MOTO naona unapotosha.
Sina Hakika ni ULAYA ipi unayo izungumzia! Covid-19 imeanzia Wuhan-China na ikasambaa dunia nzima mpaka Ulaya, Asia na sasa Africa. Je, unataka kuniambia kuwa kote huko Ulaya, Asia na America waliko kufa kwa makumi maelfu hawana hiyo akili ya kutumia hayo majimoto yanayochemka, tangawizi, malimau, ndimu n.k.?
Karibu.
 

Mkuu you are out of your mind.
Uliza Profesa Janabi yuko wapi aliyeanza toka awali kutoa taarifa za kitibabu na akapigwa stop.
 
Umejitahidi kutumia tafsida kumponda Bingwa wa kemia. Huwa unahisi hakuelewi? Kwa taarifa yako Mzee huwa anakuelewa kwa kila neno unalotoa dhidi yake. Ile ndoto ulonayo utaisubiri sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kirchoff,
Hakika hii ni taarifa Tata na inayopotosha.
Ati UNAHISI(you're NOT SURE)...!
Kwa kifupi ni kwamba hiyo haikuwa Corona yalikuwa MAFUA YA KAWAIDA TU ambayo aghalabu huambatana na homa Kali na kukohoa.
Hoja yako Ingelikuwa na mashiko kama: BAADA YA KUPATA HIYO HALI UNGELIKWENDA HOSPITALI, UKACHUKULIWA KIPIMO CHA VIRUSI VYA CORONA NA KUTHIBITIKA KUWA UNA MAAMBUKIZI then ukaanza hiyo dose yako ya kufukiza na baadaye kurudisha kupima tena na kuonesha huna maambukizi ningelikubaliana na wewe.
NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK!
 
Mkuu you are out of your mind.
Uliza Profesa Janabi yuko wapi aliyeanza toka awali kutoa taarifa za kitibabu na akapigwa stop.
Jidu La,
Hebu tujuze ni nini kilimtokea Prof.Janabi?Au tayari wamesha mu-gwandize, Bensaananize au kolimbalize? Maana kweli sijamsikia Tena kitambo!
 
Huyu nguli wa kemia fani anayoweza kuimudu sawa sawa ni kwenye mabarabara tu huku kwingine chenga tu.Naodha karudi

Umenikumbusha maneno ya Mzee Kingunge Ngombare Mwiru(rip) wakti wa kampeni za Urahisi 2015!
Alisema, nanukuu:.,.."Huyu John Pombe Magufuli hastahili KUPEWA URAIS BAALI ANATAKIWA AENDELEE KUWA MNYAPARA WA KUSIMAMIA BARABARA NA MADARAJA TU! Ndiyo kazi anazoweza kuzimudu" Mwisho wa kunukuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…