Maajabu ya Corona Tanzania: Badala ya Madaktari Bingwa wa tiba kuliokoa Taifa, ni Bingwa wa Kemia ndiye analiokoa Taifa kwa ushauri wa kikemia

Jidula,
Hebu tujuze Ni nin
Mkuu huyu Profesa alianza vizuri tu kuonya juu ya athari za kuambukizana na kusambaa COVID19.
Next, baada ya interview yake ya kuonyesha walioambukizwa na vifo Afrika Nzima(wallikuwa 200 na vifo4 wakati huo, Afrika nzima), huo ukawa mwisho wa kumsikia.

Next tukasikia kuwa pamekuwa na "reshuffle ya kawaida" ya Idara pae Muhimbili.
Hatukumsikia tena!

Tukaendelea na mama Ummy na taarifa zake za kawaida kuwa maambukizi ni machache na vifo ni vitatu vinne.
Tuliona wale wasafiri toka Tanga ambao walienda Zanzibar na kukutwa wana maambukizi-je , wameambukizwa vipi huko walikotoka?
Tunajua kuwa video zilianza kujitokeza za wananchi wnaofia nyumbani na kukutwa kuwa ni COVID19.
Ya TBC na mazishi ya Marini Hassan hatuna haja kuyaongeea.

Hapo sasa taharuki hata serikalini ikajitokeza.
Makonda anasema lake, na Ummy anasema lake!
Wanasiasa wasio na utaalam wowote wanaeleza wananchi juu ya kitu wasichokijua-COVID19.
Hapa ndipo tulipo sasa , nafikiri sasa tunajua tulipoteza muda mzuri sana wa kuwatayarisha wananchi kimkakati na kisaikolojia jinsi ya kuukabili ugonjwa huu.
 
Kwamba uchemshe pua na maji C 100

Hii hotuba Dah nimefikiria mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda sijui maana ya kujifukiza!!

kwa ufupi tu , kuna watu wanafanya sana hii kitu huko vijijini ,si jambo geni ila wewe unalazimisha iwe kuunguza pua na mdomo, kwa wale waliowahi kwenda kwa waganga wataelewa hii kitu;

kuna magonjwa yakikutokea then ukapelekwa kwa tiba mbadala wazee wetu wanajua hii kitu maji ya moto huchemshwa na dawa huchanganywa then wanachukua shuka wanakufukiza ukitoka hapo ndg mwili wote umelowa, ni balaaa hii kitu unatoka mwili mzima unatoka maji koz ya ule mvuke

pia nilimsikiliza Dokta mmoja alisema watu watumie tu tiba mbadala kwani hakuna kitakachopungua, hata kula matunda wanakula na tangawizi nikimsikia dokta akihojiwa na BBC, ambaye aliugua pia


so nadhani labda tuangalie sababu nyingine ila kwa hoja ya kujifukiza siyo ngeni, shida ni nyie mliokulia Uswazi,maeneo ya Kinondoni, Mikocheni na kukutana na makanisa kila kona ,kwa waliokulia mwendakukima ,mwakkipolya nk nk wanajua na huenda wameshangaa comment yako maana kwao ndo makanisa yao aise!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Uko sahihi kabisaaaa! Naona baada ya reshuffle Muhimbili akajitokeza MSEMAJI MPYA WA SERIKALI Bw. Paul Makonda:
Nyunyuzia(Fumigate) Dar City kuua Virusi vya Corona.....Bodaboda ziingie Katikati ya Jiji kubeba abiria....Kila mkazi wa Dar avae Barakoa...mwenye khanga,kitenge, handkerchief avae kuzuia maambukizi....n.k.
 
Kuna dokta akihojiwa bbc mkuu alisema hii kitu ,sema clip nimeshindwa kuiweka humu, yule dokta alikuwa ameumwa korona ila alikuwa anatumia vitu hvyo mkuu tusiwe wabishi ushaidi upo wa wataalaum ,jana pia Dokta mmoja kaongea bungeni plus tibaijuka nadhani kama hivi vitu havina madhara tutumie tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kasahau alituambia Tanzania ni nchi tajiri. Leo analia tufutiwe madeni. Watu wasikae karantine kisa hakuna pesa za kuwahudumia.
Na mda huo watu wanaichangia serekali hela inaenda wapi, sababu Ile michango sehemu yake ndo ingetakiwa ihudumie watu walioko quarantine
 
Wakati wanasayansi duniani wakihangaika kupata chanjo na tiba ya virusi vya corona, rais wa Madagascar Andry Rajoelina amezindua dawa ya mitishamba ''inayotibu'' Covid-19 .

Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa hakuna ushahidi wa tiba ya Covid-19 baada ya Bwana Rajoelina kutangaza dawa yake.

Taasisi ya taifa ya tiba nchini Madagascar (Anamem) pia imeonyesha wasiwasi wake juu ya ufanisi wa dawa hiyo inayoelezewa na rais Andry Rajoelina kama yenye uwezo wa kuzuwia na kupona corona.

Taasisi hiyo imesema kuwa mitishamba inaweza kudhuru afya ya mtu kwani "hakuna ushahidi wa ufanisi wake kisayansi".

Mmea huo unatarajiwa kutolewa bure kwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na na virusi vya corona.

Ikizinduliwa kwa jina Covid-Organics, dawa hiyo imetengenezwa kutoka kwa mmea artemisia (pakanga)-ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.

Dawa hiyo ambayo imepakiwa kwenye chupa na kutangazwa kama chai ya miti shamba baada ya kujaribiwa kwa watu chini ya 20 kwa kipindi cha wiki tatu, katibu wa rais Lova Hasinirina Ranoromaro ameiambia BBC.

"Vipimo vimefanyika-watu wawili wamekwishapona kutokana na tiba hii," Bwana Rajoelina alisema katika uzinduzi wa Covid-Organics uliofanyika katika taasisi ya utafiti ya Madagascar- Malagasy Institute of Applied Research (Imra), abayo ndiyo iliyotengeneza dawa hiyo ya mitishamba.

"Kinywaji cha dawa hii ya mitishamba huonesha matokeo katika kipindi siku saba," alisema rais huyo mwenye umri wa miaka 45, ambaye aliwataka watu kuitumia kama hatua ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

"Watoto wa shule wanapaswa kupewa kinywaji ... kidogo kidogo kwa siku nzima," aliwaambia mabalozi na watu wengine waliokua wamekusanyika kwa ajili ya uzinduzi wa kinywaji hicho.

Dkt Charles Andrianjara, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti ya Imra, anaafiki kuwa Covid-Organics inapaswa kutumiwa kama kinga.

Lakini alijihadhari zaidi kuzungumzia zaidi juu ya matumizi ya dawa hiyo kama tiba, lakini akasema kwamba uchunguzi wa kimatibabu umeonyesha "dalili ya ufanisi wake kama tiba", shirika la habari la AFP lilimnukuu akisema.

Kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi kimekwisharekodi hadi sasa wagonjwa 121 wa virusi vya corona, na hakuna vifo kutokana na ugonjwa huo.

Chanzo: BBC Swahili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani jana alikuwa amevuta cha Meru na kimekolea maana hiyo confusion ya speech yake si bure
 
Tunaelekea kubaya mkuu
Ila huyu ndugu yako anakotupeleka sijui ni wapi, nahisi tumeishapotea njia
 
Hii Jamii yafaa Sana kwenye kazi za nguvu nguvu tu huku kwenye reasoning huwa inachemka Sana by research by experience.Sio kila tingo ni dereva.
 
Virusi vishaingia mwilini huo mfuke hivo virusi vinayeyuka vipi Sasa hapo ni sawa na kutumia sanitizer kuuwa virusi vilivoingia mwilini
 
Mm sikatai kwamba haiui, lkn nahitaji ufafanuzi wa kisayansi.
Labda kuna madaktari wanifafanulie.
Hii ya sabuni hata mfamasia anaweza kukueleza. Lakini hata mimi ambaye si mtalaam kama kunawa kwa kutumia chlorine kunaua virus kwa nini uk fumigate na hiyo chlorine isiue. Halafu sio sisi tu tunaofanya furmigation kwenye vyombo vya usafiri au kuwanyunyisia wale watu wa
Mm sikatai kwamba haiui, lkn nahitaji ufafanuzi wa kisayansi.
Labda kuna madaktari wanifafanulie.
 

Attachments

  • 1587628943263.png
    138.5 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…