norbit
JF-Expert Member
- Jul 30, 2007
- 839
- 702
Pascal please, bingwa wa kemia anakuja na strategy za facebook kupambana na gonjwa hili hatari while him self is on hide. In cell biology study conclude inhaling steam will never be a cure for novel corona virus.Wanabodi,
Hii vita ya Corona Tanzania inakumbana na twists and turns za ajabu ajabu!, kwa vile huu ni mlipuko wa ugonjwa, ilitegemewa madaktari Bingwa ndio wangekuwa wakombozi wa taifa letu kwenye janga hili, lakini kwa Tanzania ni maajabu matupu, badala ya Madaktari Bingwa wa Tiba! kuwa wakombozi wa taifa letu, Mkombozi wa kweli wa taifa letu kwenye hii vita ya Corona ni Bingwa wa Kemia, ndiye ametoa ushauri bora kabisa wa Kikemia wa namna bora ya kuikabiliana na janga hili la Corona ili kushinda vita hii.
Je, bingwa huyu wa Kemia ni nani na ametoa ushauri gani?
Andamana nami.
1. Background, Professionalism
Tangu kuanza kwa janga hili la Corona, mimi kama Mtanzania Mzalendo nimeshiriki kikamilifu katika vita hii kikamilifu katika maeneo 5
Hivyo kwenye hayo maendeleo 5 nimeshiri kwa kutoa maoni mbalimbali, miongoni mwake ni ule ushauri wangu wa mwanzo kuwa zipo wizara zinaweza kuongozwa na Waziri mwanasiasa yoyote, lakini kuna wizara zinazo deal na technical issues, zinapaswa kuongozwa na ma professionals. Moja ya wizara ya Afya, ilipaswa kuongozwa na daktari bingwa na sio a layman kwenye medical field.
- Kama Mtanzania tuu wa kawaida
- Kama Mwana jf
- Kama mwandishi wa habari mzoefu
- Kama mtangazaji wa TV Nguli
- Kama mtu mwenye exposure.
Tulipoanza tuu ile siku Waziri wa Afya akiwa daktari Bingwa kwa jina la Janet akizungumzia kuvaa face mask, daktari huyo akiwa mbele ya Waziri wa Afya alisema face mask zitavaliwa na madaktari tuu wanaohudumia wagonjwa. Nikapandisha bandiko humu na kusema it's not right kwasababu kama inachukua siku 14 kuibaini Corona kwa aliyeambukizwa, how will one knows hivyo to be on a safe side ni watu wote wavae facemasks kama China. Waziri angekuwa daktari pale pale angejua.
Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
2. Mazungumzo na Naibu Waziri wa Afya
Kuna siku nimezungumza na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile, kama ilivyo kawaida yangu, mimi huwa nina maswali magumu. Miongoni mwa maswali niliyomuuliza Dr. Ndugulile ni swali la kwa vile Corona haina dawa, jee anaweza kueleza hao wagonjwa kwenye vituo vya matibabu wanafanywa nini au wana hudumiwa huduma gani ili Watanzania wenye uwezo waweze kuwahudumia wagonjwa wao ambao hawajazidiwa ili kuzuia hospitali zisielemewe. Dr. Alinigomea!.
Kisha nikamuuliza kwa vile Corona ni mafua, kwanini Wizara ya Afya isihamasishe alternative medicine ya watu kujitibu ili wengine wamalizane nayo juu kwa juu bila kuisumbua serikali na kupelekwa vituo vya huduma?.
Pia swali hili alinigomea na kusisitiza kila mwenye dalili aripotiwe.
Kwa kutumia uzoefu wangu wa exposure, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile alikuwa ana majibu yote tena ya kidakitari, lakini kwa vile yeye sio Msemaji rasmi, Msemaji rasmi ni Waziri wake, na Waziri sio daktari, Dr. Ndugulile aliogopa kusema akapishana na Waziri wake, lakini Waziri wa Afya angekuwa ni daktari Bingwa, Dr. Ndugulile angezungumza.
Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
3. Bingwa wa Kemia Aingilia Kati
Hayo maswali mawili magumu niliyo muuliza Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Ndugulile ambayo yalitakiwa kujibiwa na madaktari Bingwa wa tiba, leo yamepatiwa majibu badala ya kupatiwa majibu na madaktari Bingwa wa tiba, kitu cha ajabu sana kuhusu mapambano dhidi ya janga la Corona nchini Tanzania, maswali hayo yamepatiwa majibu na Bingwa wa Kemia.
Tanzania tulizoea viongozi wetu wakuu wa kisiasa huwa ni wanasiasa, hivyo ulipo tokea Bingwa wa Kemia alipoutaka urais, kiukweli kuna watu humu tulimshangaa!, tangu lini Bingwa wa Kemia akawa kiongozi wa siasa kuwa mkuu wa nchi?.
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums
4.
Bingwa wa Kemia ametoa ushauri wa Kikemia kuwa vurusi vimeumbwa cells za protein in nature na kuzungukwa fatty acid hivyo vinayeyushwa au kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka au sanitizers ambazo kikemia ni alcohol ambazo zinawayeyusha kwa kuyasaga mafuta au mvuke wa nyuzi joto kubwa una destroy protein in nature inakuwa destroyed by heat.
Bingwa wa Kemia amewataka Watanzania kuendelea kufuata maelekezo ya kitaalamu ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona ila pia na kutumia tiba mbalimbali za asili na tiba mbadala kupambana na Corona kwa kunywa tangawizi, vitunguu swaumu, au hata kujifukiza, vitu ambavyo Watanzania walipaswa kufundishwa na madaktari Bingwa wa tiba, badala yake sasa ni Bingwa wa Kemia ndio amekuwa mkombozi wa taifa letu katika vita hii dhidi ya Corona.
Ushauri huu wa Bingwa wa Kemia ndio ukombozi wa Taifa letu dhidi ya janga la Corona, kwasababu naamini kuna wengi wameugua Corona na wakajitibia kwa njia za asili na tiba mbadala na wakapona, hivyo kama kila Mtanzania akiona tuu dalili kwa mbali akaanza na huduma ya kwanza ya homeopathy treatment kwa kutumia natural remedies na treatments na alternative medicine tunaweza kuliokoa taifa letu zaidi kuliko kuwategemea hawa madaktari Bingwa wetu wa tiba za kisasa mahospitalini ambao ni mabubu huku mabingwa wa Kemia ndio wakilisaidia taifa!.
Mpaka hapa nilipofikia, bado kuna haja ya mimi kumtaja huyu bingwa wa Kemia?
Asanteni
Paskali
Below is an answer of the same question yaliotolewa na wataalamu:
Dr. Jason McKnight, Assistant Clinical Professor in the Department of Primary Care and Population Health at Texas A&M University, aliulizwa juu ya utumiaji wa mvuke dhidi ya corona virus alijibu hivi:
In general, people may find that inhaling steam during any sort of respiratory illness helps with their symptoms, such as cough, nasal congestion and chest congestion. However, this is only symptomatic relief and it is not a treatment for any viral infection,
And “you have the potential to cause real harm to yourself through burns from the heated water vapor to your eyes, face and airways, which if severe enough could cause serious and long-term complications.
Vilevile Dr. Benjamin Neuman, an expert in coronaviruses who chairs the Biological Sciences department at Texas A&M University-Texarkana, amesema, The lungs are delicate, and steam is very hot -- not a good mix. Hot steam can and does damage the lungs, and the idea that it could fight a virus that also damages the lungs is just really bad advice
Professor of cell biology at the University California, Riverside Dr. Karine Le Roch amejibu, I really don’t think that inhaling steam will treat or cure the infection.”
A study published by the Spanish Pediatrics Association notes: "It is apparent that regardless of how SIT [Steam Inhalation Therapy] is applied it carries a risk of burn injury. The usual technique of covering the head with a towel over a pan filled with hot water is dangerous due to the steam, the hot liquid, or even potential contact with the container.
The American Burn Association explains, "Hot water will burn skin at temperatures much lower than boiling point (212°F/100°C). In fact, it only takes 3 seconds of exposure to 140°F/60°C
These posts claim that inhalation of steam from boiling water, sometimes with various infused ingredients, will kill the coronavirus. This is false. While it may help ease symptoms like congestion, steam inhalation also carries the risks of burns.