Wanabodi,
Hii vita ya Corona Tanzania inakumbana na twists and turns za ajabu ajabu!, kwa vile huu ni mlipuko wa ugonjwa, ilitegemewa madaktari Bingwa ndio wangekuwa wakombozi wa taifa letu kwenye janga hili, lakini kwa Tanzania ni maajabu matupu, badala ya Madaktari Bingwa wa Tiba! kuwa wakombozi wa taifa letu, Mkombozi wa kweli wa taifa letu kwenye hii vita ya Corona ni Bingwa wa Kemia, ndiye ametoa ushauri bora kabisa wa Kikemia wa namna bora ya kuikabiliana na janga hili la Corona ili kushinda vita hii.
Je, bingwa huyu wa Kemia ni nani na ametoa ushauri gani?
Andamana nami.
1. Background, Professionalism
Tangu kuanza kwa janga hili la Corona, mimi kama Mtanzania Mzalendo nimeshiriki kikamilifu katika vita hii kikamilifu katika maeneo 5
- Kama Mtanzania tuu wa kawaida
- Kama Mwana jf
- Kama mwandishi wa habari mzoefu
- Kama mtangazaji wa TV Nguli
- Kama mtu mwenye exposure.
Hivyo kwenye hayo maendeleo 5 nimeshiri kwa kutoa maoni mbalimbali, miongoni mwake ni ule ushauri wangu wa mwanzo kuwa zipo wizara zinaweza kuongozwa na Waziri mwanasiasa yoyote, lakini kuna wizara zinazo deal na technical issues, zinapaswa kuongozwa na ma professionals. Moja ya wizara ya Afya, ilipaswa kuongozwa na daktari bingwa na sio a layman kwenye medical field.
Tulipoanza tuu ile siku Waziri wa Afya akiwa daktari Bingwa kwa jina la Janet akizungumzia kuvaa face mask, daktari huyo akiwa mbele ya Waziri wa Afya alisema face mask zitavaliwa na madaktari tuu wanaohudumia wagonjwa. Nikapandisha bandiko humu na kusema it's not right kwasababu kama inachukua siku 14 kuibaini Corona kwa aliyeambukizwa, how will one knows hivyo to be on a safe side ni watu wote wavae facemasks kama China. Waziri angekuwa daktari pale pale angejua.
Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
Karibu.
Paskali