Maajabu ya dunia: Ndege yaondoka Hongkong 2025 yafika Marekani 2024

Maajabu ya dunia: Ndege yaondoka Hongkong 2025 yafika Marekani 2024

Geography ya form two mtu anaona ni ajabu.
..........Siku zote tunahimizwa kwenda shule.
 
Hayo siyo maajabu na isitoshe waliliset hilo tukio kwa makusudi
 
kwahiyo maajabu ya dunia yanakuwa sio maajabu kwa kuwa tunakuwa tumeyasoma form two?
Hakuna cha ajabu hapo shehe.

........Muda kutofautiana kutoka sehemu moja na nyingine Duniani sio kitu cha ajabu.
 
Unaambiwa Abiria wa Ndege ya Cathay Pacific Flight 880 walifanikiwa kusherehekea Mwaka Mpya mara mbili kwa kuruka kutoka mwaka 2025 na kurudi mwaka 2024.

Safari ya ndege hiyo iliyovuka Bahari ya Pasifiki ilianzia Hong Kong muda mfupi baada ya usiku wa manane tarehe 1 Januari 2025, dakika chache baada ya jiji hilo kuukaribisha Mwaka Mpya.

Baada ya kuvuka kanda tisa za saa na Mstari wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tarehe katika safari yake ya saa 14, ndege hiyo ilitarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Los Angeles saa 4 usiku tarehe 31 Desemba 2024 - ikiwa ni muda muafaka kwa kuhesabu masaa mawili ya kuukaribisha Mwaka Mpya tena.

Huduma ya kufuatilia safari za ndege, Flightradar, ilichapisha ujumbe kwenye X (zamani Twitter), ikisema:
"Ndege hii imeondoka Hong Kong mwaka 2025 na itatua Los Angeles mwaka 2024."

"Baada ya saa 11 na nusu angani, ni wakati wa kusherehekea Mwaka Mpya tena!"
Kipya ni kipi! Wakazi wa Kasumulu Kyela boda ya Malawi na wa Tunduma boda ya Zambia kila mwaka husherehekea mwaka mpya mara mbili.
 
Imekuwa ni uthibitisho tena Dunia si tambarale. Wale wa Dunia tambarale wanaumiaaaaa
 
Back
Top Bottom