Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaugua wewe, tena kichwani. Hicho chuma kimekulia kwenye moto, sio hawa wafuga makalio wanarukaruka wakigongwa mguuni wanatingisha vidole vya mkono.Ukizungumzia lishe ni wazi kabisa picha ya marehemu Kizota zinaonyesha hakuwa na physical fitness kulinganisha na players wetu wa sasa .
Kwenye picha utaona mwili mkubwa ambao haujajengeka kabisa, no wonder inasemekana alikuwa anapiga sana pombe
Unaugua wewe, tena kichwani. Hicho chuma kimekulia kwenye moto, sio hawa wafuga makalio wanarukaruka wakigongwa mguuni wanatingisha vidole vya mkono.
Hivi unaweza kumlinganisha Kizota na Ajibu au Samata wewe? Kama ulikuwa mdogo, uliza uambiwe. Ule mfupa umejaa wewe...hatari!
Kwanza kwa taarifa yako, tangu hawa wabishi wastaafu soka, hakuna timu yeyote ya Tanzania iliyothubutu kukwea pipa na kombe. Ni huyu mume and company ndio waliandika historia ya kwenda kwenye ardhi ya watu wakakichafua na kumchukua mwali wakarudi naye katika ardhi ya Tanganyika. Na mambo haya yamefanywa na Yanga peke yake
Mchezaji aliyepunjwa sifa na HESHIMA .Yaani mpira ulikuwa zamani huyu alikuwa anauwezo wa kuwa beki na kuwa mshambuliaji hatareee ,binafsi niliacha kushadadia,kubishana,na kuhudhuria uwanja wa taifa baada ya LUNYAMILA kustaafu mpira
wewe ni jau yaani mpira wa zamani wa kumpigia mtu magoti unauita mpira?Yaani mpira ulikuwa zamani huyu alikuwa anauwezo wa kuwa beki na kuwa mshambuliaji hatareee ,binafsi niliacha kushadadia,kubishana,na kuhudhuria uwanja wa taifa baada ya LUNYAMILA kustaafu mpira
miili sio tatizo hata moringa mbona ana mwili mkubwa tu na anapigwa chenga na watoto wadogo kabisaUkitazama maumbo ya Wachezaji wa zamani na wa Sasa hivi utagundua kuna Tatizo kubwa sana siku hizi
mwili wa kizota ni wa wachezaji wa watford waliopigwa 8 juzi na citySio tatizo mkuu , acheni kukariri.
Mifumo ya mpira imebadilika sana , sahizi mpira hauchezwi na Giants, mpira unachezwa na watu wenye maumbo madogo , haya Mapinduzi yalianza kufanyika Barcelona wakiifuata falsafa ya Cruyf..
Nenda England kaangalie Man city wanavyowasha Moto, angalia maumbo ya wachezaji kama Bernard Silva, sterling, Aguero, Gundogan n.k, wachezaji wadogo wadogo kiumbo ni ngumu kuwakaba na pili wana mbio balaa , hao MaGiant wenu wa zamani kwa mpira wa sahizi wangeweza kujiharishia uwanjani maana wangekimbizwa kwa kugongewa pasi kama 800 hivi fupi fupi mpaka wauone Moto.
Umri wako hauruhusu kujua misuli iliyokuwepo nchi hii. Hawa watoto laini wasingefanania kuwapeleka kushindana na watu kama kina George Semogerere. Mtafute mzee wako muulize jinsi ndimu ilivyopigwa zamani. Siku hizi ni promosheni tu zinawabeba watu, ni kama tu kwenye muziki.Una kichaa wewe.
Yaani unamlinganisha Samatta na huyo mlevi?
Samatta in terms of professionalism hana wa kushindana nae, ameutunza sana mwili wake, huwezimlinganisha na hao wanywa Chang’aa wenu wa zamani
Umri wako hauruhusu kujua misuli iliyokuwepo nchi hii. Hawa watoto laini wasingefanania kuwapeleka kushindana na watu kama kina George Semogerere. Mtafute mzee wako muulize jinsi ndimu ilivyopigwa zamani. Siku hizi ni promosheni tu zinawabeba watu, ni kama tu kwenye muziki.
Umri wako hauruhusu kujua misuli iliyokuwepo nchi hii. Hawa watoto laini wasingefanania kuwapeleka kushindana na watu kama kina George Semogerere. Mtafute mzee wako muulize jinsi ndimu ilivyopigwa zamani. Siku hizi ni promosheni tu zinawabeba watu, ni kama tu kwenye muziki.
Hata mimi nashangaa, eti mechi moja tu ya fainali unapata kiatu cha dhahabu kwa mabao mawili!Umeweka chumvi nyingi sana mwaka 1993,Kizota hakwenda kucheza mechi ya fainali tu
Wale wana miili mikubwa siyo kama wetu.Kuna jamaa alirushiwa jezi na Joe Hart aliivaa ikampwaya.jamaa anakaa kinondoni hapo.Nitajie timu kubwa ulaya iliyojaa Giants....
Ukinitajia kina VVD, nitakutajia kina firmino, keita,Mane, Salah , Xhaqiri na wengineo ambao sio Giants...
Every General rule has exceptions.
Huyo mlevi, huyo mlevi...una ugomvi naye au ulevi ndio namna pekee unayomtambua?Mzee
Picha za huyo Mlevi si ndio hizo hapo Juu?
Tunajua Old is Gold lakini muacheni kusifia hadi mkaanza kufanya kufuru.
Kama huyo mwenzako anayemlinganisha Samatta na huyo Kizota!
Ukitazama maumbo ya Wachezaji wa zamani na wa Sasa hivi utagundua kuna Tatizo kubwa sana siku hizi
Unauliza au unatuambia?Zamani kulikua hakuna Chips
Asante kwa historia nzuriLeo nikiwa maeneo fulani nikiwa nafuatilia mchezo wa CHAN kati ya Tanzania na Sudan nikawa napata story fupi ya mpira yenye kusisimua kuhusu mchezaji wa zamani wa Yanga marehemu mzee SAID NASSOR MWAMBA KIZOTA .
View attachment 1213754
View attachment 1213733
Unaambiwa ilikuwa mwaka 1993 ndio mwaka ambao fundi huyu aliwapa burudani mashabiki wa Yanga na kumfanya kuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo.
View attachment 1213755
Basi kipindi hicho Yanga ikiwa inajiandaa kuvaana na Sport Club Villa ya Uganda katika fainali ya klabu bingwa afrika mashariki na kati mjini Kampala Uganda.
View attachment 1213764
Timu ilikuwa imeshaondoka na kutangulia nchini Uganda jamaa alikuwa anaendelea na mishe zake akiwa na tuhuma za kupiga ulabu alipokuwa kambini basi akawa amepoa kwa dada yake maeneo ya mwembe yanga aitwaje White Mama (jina maarufu)
Basi watu wa Yanga baada ya kujishauri muda mrefu wakamfuata na kumchukua mahali hapo na kumpeleka nchini Uganda kuamkia siku ya fainali.
Siku ilipofika jamaa bila kufanya mazoezi ya pamoja na timu akaingia mzigoni akaweka kamba mbili wavuni huku goli la tatu la Yanga likifungwa na Lunyamila hivyo kuifanya Yanga kutawazwa ubingwa mbele ya SC Villa nchini Uganda Kizota akarudi na ufungaji bora wa michuano hii na katika mwaka huo huo akabeba kiatu cha ufungaji bora ligi kuu ya Tanzania bara kipindi ikidhaminiwa na TBL.
Mechi kubwa iliyoacha historia kipindi hicho ni ilipowakutanisha watani wa jadi Kizota alipiga goli mbili huku moja ya goli maridhawa akimchambua na kumfanya atakavyo goli kipa mahili wa wakati huo Mohamed Mwameja .
Wakati mwengine fundi huyu alitupiwa virago na wana Jangwani kwa tuhuma za kuhujumu timu walipopokea kipigo cha 4-1 kutoka kwa Simba na Kizota akadondokea Simba
View attachment 1213765
Kizota Vs Mmachinga
Mwaka 1995 ;Wakali hawa wa kufumania nyavu na kuchezea mpira walikutana katika Mbungi ya kkoo moto ulikuwa mkali pale ambapo Mmachinga alipopachika goli la kuwapa Yanga uongozi kipindi cha kwanza,wakati Yanga wakijua turubai limehamia kwa jirani Kizota anapiga goli maridadi la kusawazisha na kuwachanganya Yanga ambao kutahamaki wanapigwa kamba ya pili na Mchunga Bakari ‘Mandela’ kukamilisha hesabu ya 2-1 na mchezo kuishia hivyo.
View attachment 1213753
YANGA WAMPIGIA MAGOTI
Yanga walitambua makosa yao na kumsotea Fundi huyu wa mpira na kwa vile alikuwa akiishi maeneo hayo ya mitaa ya Jangwani haikuwa kazi sana kumpata na kumvisha tena uzi wa watoto wa Jangwani kwa mara nyingine.
View attachment 1213751
AKUTANA TENA NA SIMBA
Kizota anakutana tena na Simba mwaka 1996 na kushiriki katika matokeo ya sare ya maajabu jijini Arusha 4-4
View attachment 1213749
Hahah kuna hili la kizota na waarabu jamaa alienda uarabuni na kupiga mpira wakina maradona jamaa wakamtaka hadi abadilishe uraia usifanye masihara moto anaouwasha mtu mpaka waarabu waelewe somo (hii ni stori nyingine)
Kizota pia amechezea timu ya taifa na kupata mafanikio ikiwemo challenge cup
Fundi huyu wa mpira alifariki dunia tar 11/02/2007 kwa ajali ya gari maeneo ya Veterinary akitokea kushuhudia mchezo wa marudiano, Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, Raundi ya Awali kati ya wenyeji Simba dhidi ya Textil de Pungue ya Msumbiji ulioisha kwa Simba kutolewa kwa njia ya matuta 3-1 baada ya sare pacha ya 1-1 .
View attachment 1213748
View attachment 1213766
View attachment 1213794
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya fundi huyu wa mpira na wengine wengi waliotangulia mbele ya haki.
Timu alizopitia Kizota ni pamoja na Shirika la posta Tabora (wakiti huo ikijulikana kama Posta na Simu) ,Yanga,Simba,Al Nasar ya Oman na Al Jazeera ya uarabuni Abu Dhabi.
Hebu tupia hapa kisa chochote unachofahamu au kusikia kuhusiana na wachezaji wa zamani wa Tanzania kama Sunday Manara ‘Computer’ ,Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’ ,Maulid Dilunga ‘Mexico’Juma Pondamali ‘Mensa’ ,Omar Hussein ‘Keegan’, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ ,Ezekiel Greyson ‘Jujuman’ ,Ally Yusufu ‘Tigana’ ,Athuman China na wengine wengi
Huyo mlevi, huyo mlevi...una ugomvi naye au ulevi ndio namna pekee unayomtambua?
Sijui macho yako yamejawa na husda au upofu, maana unamzungumzia utadhani unamwongelea mtu mwenye kimo cha Mohamed Ibrahim wa 5imba, kumbe unamzungumzia Kizota, mtu na misuli yake.
Shida yako unajua upande mmoja wa shilingi na mdomo mwingi. Mimi Kizota nimemuona na hawa wanaocheza leo nimewaona. Kuna watu wasikie tu, sijaona body stamina yao katika kizazi hiki cha chips mayai.