Maajabu ya jiji la Kampala

Maajabu ya jiji la Kampala

Kwa kuwa ulishafanya nao kazi, siwezi kukubishia. Ila pia na Mimi nilishafanya kazi na mmoja miaka ya nyuma. Yeye peke yake ndiye aliyekuwa Mganda kwenye taasisi yetu. Alikuwa mchapa kazi sana japo sijui kama hiyo ilikuwa ni tabia yake binafsi au alinadilishwa na mazingira.

Kilichonifanya niwaone wa huku ni wachapa kazi ni baada ya kushuhudia maduka na mama lishe yamesahafunguliwa saa kumi na mbili Asubuhi, na mama lishe kuivisha chakula mapema sana Asubuhi.
Maduka kufunguliwa saa 12? Kwani dar inafanyaje? Dar panakesha
 
Sijui nauli ya kutokea Dar. Kama unataka "kuja" Kampala, panda basi hadi Mwanza ukashangae kwanza miamba ya jijini Mwanza ndipo uendelee na safari ya Kampala.

Na kama utaanzia safari Mwanza kwa magari ya kuunga unga kama nilivyofanya, utapanda gari kutoka Mwanza hadi Katoro (Geita) Tsh 8,000/=.

Katoro hadi Bukoba Tsh 20,000/=

Kutoka Bukoba Mjini utachkua daladala hadi Mutukula Tsh 4,000/=.

Mutukula ukishagongewa mihuri, unaweza ukavuka mpaka kwa miguu kuingia upande wa Uganda kwenda ziliko hiace (Waganda huziita taxi), au uchukue bodaboda Tsh 1,000/= au Tsh 2,000/=, lakini wakikuona wewe ni wa kuja, bodaboda wanaweza wakakuambia hata Tsh 5,000/=.

Kabla ya kuvuka kwenda upande wa Uganda, ni vizuri ukabadilisha hela upate za Kiganda, na pia ukasajili line ya Uganda, mfano MTN (Vodacom). Kama una passport kubwa (siyo EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT) unaweza ukasajili line yako kwa jina lako hapo hapo Mutukula upande wa Tanzania, gharama ni Tsh 3,000/=, lakini kama unatumia EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT, watakupatia line iliyokwishasajiliwa kwa jina la mtu mwingine kwa Tsh 10,000/=, ila wakikuona wewe ni mtoaji mzuri watakuambia Tsh 15,000/=.

Ukishaingia upande wa Uganda, utapanda "taxi" kwa hela ya Kiganda Ugx 40,000 Mutukula hadi Kampala. Ingawa nauli ni Ugx 40,000/= , mimi nililipa Ugx 35,000/=, na mtu mwingine alilipa Ugx 30,000/=. Wakati wa kurudi nitabargain hadi na mimi nipande kwa Ugx 30,000/=.
Border unaweza kutumia kitambulisho gani kuingia kama huna passport na inakua valid kwa muda gani ukiwa ndani ya Uganda.
 
Huenda boda boda wa huku nao wapo rafu katika uendeshaji pikipiki kama wa Bongo. Nimeshuhudia zikipuuzia kuzingatia taa za kuongozea magari. Ni tofauti na boda boda wa Kigali ambao inasemekana ni watiifu sana wa Sheria za barabarani

Kuhusu nidhamu barabarani ni serikali ndio inazembea kwa wajinga kama hao
Rwanda wameamua hawataki ujinga
Ila Kampala pazuri sana nimeenda mara mbili
 
Kitu kingine kuhusu waganda , hoja ya uchapakazi hii haipo kwa miaka miwili niliokaa kule kwani starehe kwao ni kipaumbele kikubwa ,wanaishi wakiwaza sana kutoka nchini kwao wakiamini kutoboa zaidi.Hawajitumi ila ni wajanja wajanja sana na ukikaa vibaya watakupiga ,tabia ya udokozi kwa vitu vidogo vidogo kwao ni kawaida.
Ngono ni kitu simple sana kwani wanakauzungu flani hata dem akikuelewa anakufata anakueleza uhalisia kua anakutaka .
Bidhaa zao sijui ni kwa nn ila nyingi ni org kwa asilimia 100, copy ni chache labda miaka hii ya sasa .Kama taifa kl Waganda ni kabila kubwa ila wanawabagua sana makabila mengine .
Kujiunga UPDF (jeshini ), kiswahili ilikua sifa ya ziada
Ujanjaujanja na wiziwizi kwa Waganda ndio hulka yao! Wana kamsemo kao la, "nnfella kumali"! Ahahahahaha!!!
 
Ndio saizi huwezi kupigwa, elfu 1 nadhani wanaita Lukumi. Polepole ni mpola mpola, hao boda usiku wengi wanakuwa maji unakuta anakuita sebo(mwanaume) tugende(twende). Wewe unamuita Janguu(njoo) sebo
Nimeanza kuelewa kwanini iddi amini aliitaka kagera. Yani kwa hayo maneno iko ni kihaya kabsaaaaa. Yani mhaya anaishi uganda bila shida ya lugha kabsa.
 
Mimi nafikiri suala la vimini ni utamaduni, pengine! Sijui ni Wanyankole au ni kabisa jingine la Kiganda, ambalo mavazi yao ya kimila yanaacha sehemu kubwa ya mwili wa mwanamke wazi. Mavazi kam hayo huyavaa kwenye shughuli za kiutamaduni kama ngoma n.k. Inawezekana wameathiriwa na huo utamaduni.
Nitatembea nikiwa nimedindisha mno. 🙆
 
Kaulizie chakula kinaitwa Rolex, hakipatikan mgahawani ni vijana barabarani wanakaanga chapati Inakunjwa Kwenye mayai ni very cheap. Wape hi ba sebo na wanyabo
Nimekipata. Nimekiona kinavyoandaliwa. Nimenunua kwa Ugx 2,000 maeneo ya Mulago.

Hii hapa ikiwa imeshawekwa kwenye mfuko mweupe.
 

Attachments

  • IMG_20250102_095937_983.jpg
    IMG_20250102_095937_983.jpg
    488.7 KB · Views: 4
Kampala nenda owino market,ghazaland market uone wenzetu walivyoyapangilia masoko yao.
Binafsi huwa nikienda Kampala huwa nafikia Galaxy hotel ipo city centre na ni cheap hata wahudumu wake wengine wanagonga kiswahili vizuri sana.
 
Uganda kiswahili kinatumiwa ZAIDI na wanajeshi UPDF na majambazi.
🥺😀

Mbona leo nimekuta eneo lililopo katikati ya jiji pameandikwa kwa Kiswahili USIKOJOE HAPA?

Eneo lingine kwenye magari yanayoenda nje ya Uganda nimekuta wameandika kwa English na Kiswahili. Kwa Kiswahili wameandika: CHOO 300, KUOGA 1,000
 
Kampala nenda owino market,ghazaland market uone wenzetu walivyoyapangilia masomo yao.
Binafsi huwa nikienda Kampala huwa nafikia Galaxy hotel ipo city centre na ni cheap hata wahudumu wake wengine wanagonga kiswahili vizuri sana.
Ni typing error au ndicho unachomaanisha, MASOMO yao?

Gharama za hiyo hoteli zikoje mkuu? Chumba kwa siku ni bei gani?
 
Duu kipande cha broadway Kawempe tuliinjoi sana ,kyungu=jiko,Amazi =maji,Kaunga(ugali),binjanjaro(maharage.janguu (njoo).Nimeanza sahau mengine ila kampala Naipenda kuliko dar
Ugali siyo posho? Jana niliingia mgahawa fulani, nilipouliza vyakula vilivyopo, nilitajiwa na posho. Nikaagiza posho na nyama.
 
Back
Top Bottom