Uchaguzi 2020 Maajabu ya kampeni CCM Arusha, Joshua Nassari aubamiza Upinzani

Uchaguzi 2020 Maajabu ya kampeni CCM Arusha, Joshua Nassari aubamiza Upinzani

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana, heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Wahenga walisema staajabu ya Mussa lakini siyo ya Firauni.

Kwa kweli binadamu tuko tofauti. Huyu bwana alikuwapo siku Mh. Lissu aliponusurika kuuwawa. Je, ni Kwamba amesahau tukio lile au aligundua kuwa hatua ile ilikuwa halali?

Je, huyu si ndiye aliyemtuhumu jiwe kununua wabunge?


Ama kweli nani alijua kuwa petro katawi alikuwa afisa kipenyo wa daraja fulani huko?

Ama kweli staajabu ya Mussa!
 
Mwanasiasa sio mtu wa kumuamini. Tafakari, ndio maana mimi hata Mbowe sina imani naye kabisa.

Ila Magufuli ndiyo wa kumwamini kwa sababu anathubutu kunena Mungu hoyeeeee?!

Akinena hayo, wakati huo huo wengine wakipotea, wengine wakiokotwa kwenye viroba na wengine wakijeruhiwa kwa risasi mchana mchana?

Ila Mbowe?

Mbowe, Lissu, Maalim, Membe, Zitto nk kazeni hapo hapo kuna mitu inazidi kuchanganyikiwa karibu itaanza kurokota makopo.
 
Ila Magufuli ndiyo wa kumwamini kwa sababu anathubutu kunena Mungu hoyeeeee! Wakati huo huo wengine wakipotea, wengine wakiokotwa kwenye viroba na wengine wakjeruhiwa kwa risasi mchana mchana?...
Sijasema namuamini Magufuli. Nimesema mimi kama mimi Mbowe sina imani nae, 2015 alifanya sarakasi, mwaka huu anafanya sarakasi. Kaa utafakari.
 
Sijasema namuamini Magufuli. Nimesema mimi kama mimi Mbowe sina imani nae, 2015 alifanya sarakasi,mwaka huu anafanya sarakasi. Kaa utafakari...

Yupo anayefanya sarakasi kuliko Magufuli?

Hajali maisha ya kina Azory, Ben, Lissu na wengi wengine achilia mbali wale wa kwenye viroba.

Anathubutu kutamka:

Mungu hoyeeeee? Na yuko vizuri tu? Ila macho yenu kwa Mbowe tu?

Ama kweli "ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni!"
 
Yupo anayetaka sarakasi kuliko Magufuli?..."
Ya akina Azory yametokea, Magufuli yupo madarakani, unadhani nini suluhu kwa mtu kama mimi na wewe?
Huyo aliyefutwa ubunge karudi CCM. Nini suluhu kwa walalahoi?
 
HUYU KIJANA AMEIFUTA CHADEMA RASMI HUKO ARUSHA.

Kwa huo utopolo? Umemsikia vizuri lakini tokea katika TV yetu ya chama pendwa?

Hizo ndiyo nondo kweli kweli yaani best of the best walizothubutu kuturushia kutoka kwake.
 
Ya akina Azory yametokea, Magufuli yupo madarakani, unadhani nini suluhu kwa mtu kama mimi na wewe?
Huyo aliyefutwa ubunge karudi Ccm. Nini suluhu kwa walalahoi?

Siyo huyo tu hata aliyekuwa mmoja wa vigogo CDM bwana petro katawi, kumbe alikuwa afisa kipenyo.

Si tu kuwa karudi CCM bali karudi kwa waliomtuma. Hawa ndiyo kama huyu dogo, labda na wewe pia ambao kazi zenu ndiyo hizo za kuleta tafrani ili mradi jiwe aendelee kufanya yake nanyi ka buku 7 kaendelee kuwapo.

Mnasema alimradi, mkono uende kinywani.

Si kila mtu ana njaa kama zenu. Mark my words!
 
Siyo huyo tu hata aliyekuwa mmoja wa vigogo CDM bwana petro katawi, kumbe alikuwa afisa kipenyo.

Si tu kuwa karudi kwa waliomtuma bali hawa ndiyo kama huyu dogo, labda na wewe pia ambao kazi zenu ndiyo hizo za kuleta tafrani ili miradi jiwe aendelee kufanya yake nanyi ka buku 7 kaendelee kuwapo. Alimradi, mkono uende kinywani.

Si kila mtu ana njaa kama zenu. Mark my words!
Kila mtu ana uhuru wa kutafsiri na kuelewa jambo kwa akili yake. Kama wewe unaon mimi kutomuamini Mbowe ni kosa hiyo juu yako. Lakini kuw mkweli na kuwa na msimamo ni jambo la msingi.
 
Kila mtu ana uhuru wa kutafsiri na kuelewa jambo kwa akili yake. Kama wewe unaon mimi kutomuamini Mbowe ni kosa hiyo juu yako. Lakini kuw mkweli na kuwa na msimamo ni jambo la msingi.

Mbowe kawashika pabaya kila bandiko huachi kumtaja.

Jiwe kakushikia akili hakuna unapothubutu kumtaja hata kwa jina lake.

Eti huko ndiyo kunywa maji ya bendera. Utopolo mtupu.

Nani kakwambia kutomwamini Mbowe ni kosa? Kutomwamini jiwe nako je?

Mbowe alikufanya nini kila wakati kumuwaza yeye? Hujui kuwa yule ni mume wa mtu?

Khaaaa!
 
Mimi namwamini JPM? Mimi ni mtu wa msimamo,sio mtu wa kukariri na kufuata mkumbo.

Endelea hivyo hivyo Ila tambua wengine wengi tu wanamwamini Mbowe kwa sababu za msingi kabisa na si kwa kukariri wala kufuata mkumbo.

Asiyeweza kujali roho za watu huku kila uchao madhabahuni mniombee, kwa hakika kwa huyu ni heri ya shetani mwenyewe.
 
Kama CDM inafutika hivi basi jiwe kaimaliza kabisa CDM na hasa kote alikozomewa hadi warushaji matangazo wa CCM wakafanya yao.
Ndo kwisha habarii yenuuu, mwambieni jamaaa yenu arudi kwao moshii, awaache wanaarusha wajiongozee
 
Kwa huo utopolo? Umemsikia vizuri lakini tokea katika TV yetu ya chama pendwa?

Hizo ndiyo nondo kweli kweli yaani best of the best walizothubutu kuturushia kutoka kwake.
TULIENI SINDANO IWAINGIEE. NASARI ANAWASIGINA VIZURIII.
 
Dogo jinga kafika bei, hana analoweza kuwashawishi wapiga kura wa Arusha mjini.

Hao wapiga kura wa mjini ndio waliomwingiza kwenye siasa, walitia nguvu kampeni zake kwenye ule uchaguzi mdogo. Leo amejiunga na CCM anauponda upinzani uliomjenga.

Huo mdio mwisho wake kisiasa. Atunze hela alizonunulika zimsaidie, vinginevyo ameanza maisha marefu ya ujana wa msoto kutokana na usaliti wake kwa wapiga kura.
 
Back
Top Bottom