R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,178
Nakumbuka hapo miaka ya 2015 niliwahi kwenda ugenini siku 3 hivi kuufatilia mambo yangu, ilinibidi niende kwa mjomba wangu alieniasa niende kwake.
Sasa tatizo nililokuwa nalo enzo hizo kinyesi changu kilikuwa kinanuka sana, yani nikitoka huko chooni ni kunanuka si kidogo, nilikuwa nakula mtaani nahisi ndio chanzo.
Nikiwa kwenye basi kuelekea huko, katika kuperuzi peruzi huko fb nikaona kuna mtu kashauri kwamba kiberiti kinakata harufu, nilichukulia ni kama utani ila nilinunua kiberiti kimasihara.
Nilipofika huko, mda wa kwenda chooni ulipofika nikabeba na kiberiti changu, shughuli nimemaliza choo kinatoa harufu si mchezo, nikamwaga maji (kuflash), nikachukua kiberiti nikawasha njiti 2 nikatupia kwenye choo, yani harufu yote ikakata, nilishangaa sana.
Sikuwa na hofu tena ya kuaibika kwa choo kinachonuka,
Kwa siku tatu nilizokaa pale nilitumia njiti 4 tu
Mbinu hii nimewahi kuitumia pia kwenye gesti zenye vyoo vyenye harufu, natupia njiti 2 harufu inakata.
NB: naona watu wanahofia choo kuwaka moto, Hakuna kitu hiki, Njiti ikishaingia kwenye tundu la choo inazima kwenye maji ya choo, pia nacho kinyesi hakiwezi kuwaka moto kwasababu kina unyevu mwingi.