Maajabu ya tairi mbovu na utajiri uliojificha ndani yake

Maajabu ya tairi mbovu na utajiri uliojificha ndani yake

Sehemu ya pili.. Maajabu ya tairi mbovu na utajiri uliojificha ndani yake
Kiwanda kitanunua tani moja ya tairi kwa shilingi laki mbili bei ya sasa.. Ataichoma mchomo mmoja unaochukua tani nane kwenye boiler kupitia mchakato uitwao pyrolisis (kama kupika gongo tu)
Tani 8 sawa na shilingi milion 1.6
Zitakuletea wastani wao
.Mafuta ya I.D.O (industrial diesel oil) lita 3000 sawa na tani 3..
. Vumbi (black carbon) wastani wa tani 4
.Waya wastani wao tani 2
Gesi wastani wa nusu tani
Lita moja ya I.D.O kwa sasa ni Tsh 2000 zidisha mara 3000 ni Tsh 6,000,000
Vumbi (carbon black) kwasasa tani moja ni kama elfu 70 zidisha mada 4 ni Tsh 280,000
Waya kwasasa tani ni kama shilingi laki 8 zidisha mara 2 ni Tsh. 1,600,000
Gesi sijapiga hesabu
Kwahiyo mzigo wao shilingi 1.6M unakuletea wastani wa shilingi 7, 880,000/=
Ukitoa gharama zote za uendeshaji bado hukosi faida ya Tsh. 5,000,000/= tasilimu
Kwa wasiojua matumizi ya hizi bidhaa
1. Mafuta ya IDO ni kama nishati mbadala viwandani badala ya diesel, kuni, gas au umeme
2. Vumbi ni malighafi kwenye viwanda vya saruji
3. Waya zipo ngumu na Iaini.. Ngumu zinatumika kama binding wire kwenye ujenzi unaohusisha nondo, laini kama carbon catalyst kwenye viwanda vya nondo.. Si mnajua nondo bila carbon ukiipinda inakatika?
4. Gesi kwa matumizi ya kupikia nk

Hayo ndio maajabu na utajiri uliojificha kwenye tairi mbovu

Good morning Tanganyika
Bongo hapa yanauzwa wapi hayo mataili baada ya kuyachuna?
 
Bro MshanaJR..... Asante kwa taarifa mfano Mimi hapa nikiingia kitaa nokapata hizo tairi tani moja kiwanda gani kinaweza kuchukua mzigo on spot pasipo kupitia huo mchakato wa kukata kutoa hiyo mipira
 
Viwanda vinavyozalisha I.D.O
Mlandizi kipo kimoja bado kinajengwa
Kibaha Madafu na Zogwale vipo viwili
Bagamoyo Kipo kimoja
Kigamboni Kibada kipo kimoja
Kisarawe kipo kimoja
Mkuranga kuna vingine viwili vinajengwa
Nafanya kazi Kisarawe... Natafuta location ya kiwanda hiki lilipo.... Ni maeneo gani?...
 
Ok nimerudia nimekuelewa.
Zaidi ni kwamba tairi hazichomwi moja kwa moja bali hufungiwa kwenye tank kubwavla
Bro MshanaJR..... Asante kwa taarifa mfano Mimi hapa nikiingia kitaa nokapata hizo tairi tani moja kiwanda gani kinaweza kuchukua mzigo on spot pasipo kupitia huo mchakato wa kukata kutoa hiyo mipira
Viwanda vinavyozalisha I.D.O (vinavyonunua tairi)
Mlandizi kipo kimoja bado kinajengwa
Kibaha Madafu na Zogwale vipo viwili
Bagamoyo Kipo kimoja
Kigamboni Kibada kipo kimoja
Kisarawe kipo kimoja
Mkuranga kuna vingine viwili vinajengwa
Quote
 
Makadirio ya gharama za ujenzi wa kiwanda ni tsh ngapi mkuu maana wengine tuko mbali sana na dar vilipo viwanda kwahiyo bei kwetu inaweza isiwe rafiki kabisa chukulia, dsm bei ni 2000 had 5000 je ukiwa kanda ya ziwa ambapo utahitaji na gharama za usafiri na ushuru bei ya kununulia itakua itakua chini zaid kitu kama 1000 hadi 2500 jambo ambalo ni gumu kupata tairi kwa bei hyo ndogo.
 
Mikoani wanaleta sana Dar, in fact sio tairi chakavu ni tairi mbovu hata zilizochanika na kusamabaratika, mabaki ya tairi kwa watengeneza ndala yale yanaitwa maini, na kuna unga wa tairi toka viwanda vinavyofanya retrading
Bei ni kuanzia milion 100
1731735105860.png
1731735178698.png
1731735127643.png
 
Model C Waste Tyre Pyrolysis Plant
Capacity model: 1Ton-15Ton
Raw materials: Waste Tyre/rubber
Average out-put oil rate: 45% fuel oil, 30% carbon black, 10% steel wire, 10%-15% syngas
Chief kama nimeelewa ni kama hii inamaanisha kwamba 1Ton kwa wastani inaweza zalisha fuel 45%, 30% carbon na 10% steel wire.

Hivi vitatu vikiunganika ndiyo inakua tani 1. Na siyo kwamba kila kimoja ni tani moja kivyakevyake.

Kama IST ina tani 1 ikitolewa injini na kuwekwa pembeni itawezekana iendelee kua na uzito huo huo wa tani 1?
 
Hapa usichanganye vitu viwili tofauti
Kwenye tairi mafuta wala gesi havionekani mpaka tairi ifungiwe kwenye boiler .. Boiler likipashwa moto likakolea lile fukuto ndani yake kulikojaa tairi ndio litatoa mvuke ambao utapitia mchakato wa kupozwa na kugeuka kimiminika ( mafuta ya I.D.O)
Wakati huo wa fukuto kuna gesi pia itatoka.. Hivyo hivi viwili haviwezi kuonekana mpaka kuwe na mchakato
LAKINI body ya IST na engine yake ni vitu vinavyoonekana.. Mfano wa boiler huu hapa
1731735105860.png
 
Angalia I.D.O bada ya kutoka mtamboni ni nyeusi tii lakini ikisafishwa kwa kutumia chemikali maalum unapata dizeli safi na kuna viwatilifu ukiviongeza inaweza kutumika kwenye magari
Kwa Tanganyika EWURA hawatoi vibali vya kusafisha I.D.O
1731735178698.png
 
Back
Top Bottom