Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) inasomeka hivi " Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa nchi ya kidemokrasia na ya mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu
Katika mazingira hayo vyama vya upinzani vinapaswa kutoa "constructive criticism" ambavyo ndivyo vifanyavyo vyama hivyo, hususani chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na kwa mujibu wa Katiba ya nchi, tulitegemea chama tawala cha CCM kijibu hoja hizo kwenye majukwaa ya kisiasa
Hali ni tofauti sana, hususani kwenye utawala huu wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli, ambapo wanachukulia wao kuwa "constructive criticism" kuwa ni makosa ya jinai, ambapo Jeshi la Polisi nchini "linaagizwa" liwakamate na kuwafungulia mashitaka ya uchochezi, kukosa uzalendo, usaliti na kutumiwa na mabeberu!
Kwa mazingira ya sasa, Jeshi la Polisi nchini linafanya kazi kwa "maagizo" ya watawala wa CCM na hivyo kufanya Jeshi hilo kuwa kama kitengo cha CCM!
Niwakumbushe wosia muhimu sana uliowahi tolewa na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye mkutano mkuu wa CCM, mwaka 2012, huko Dodoma, alipowatahadharisha wanaccm wenzake, kuwa ni makosa makubwa sana kulitegemea Jeshi la Polisi nchini, kuwalinda na kuwabakiza madarakani, kwa kuwa chama cha siasa kama CCM wajibu wake mkubwa ni kuzijibu hoja zinazotolewa na wapinzani kwenye majukwaa ya kisiasa
Niwaambie tu wanaccm, kwa kuwa mmepuuza wosia huo muhimu sana uliotolewa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, basi niwatabirie kuwa anguko lenu litakuwa kubwa na lenye kishindo kikubwa sana!