Maajabu ya undu Lissu na CHADEMA yake

Maajabu ya undu Lissu na CHADEMA yake

Kweli huko mtaani kwenu ufipa kwa baba mkwe mlikopanga ni Lissu tu. Huku lumumba walikojenga CCM ni Magufuli tu.
Naskia kuna kushikana uchawi huko Lumumba Eti Kuna watu wanakihujumu Chama na mwenyekiti!!! Hamtapigana risasi huko mwaka huu???
 
Magufuli akiitwa masiha wa bwana mnatokwa na povu, ila ninyi mnamwita Lissu masiha wa bwana!
Masihi wa bwana anatangaza Uhuru haki,kufunguliwa watumwa/wafungwa,upendo naa faraja

Sasa muuaji,kutekana,kuoneana ,kudhulumiana kuna mfanya MTU awe masihaaa
 
Wana CCM wanatambua kabisa Tundu Lissu anakubalika na kuungwa mkono na wananchi wengi sana huku Tanganyika. Ni sawa kabisa na Maalim Seif kwa kule Zanzibar. Mpaka sasa wanatambua kura ya maoni inaonyesha endapo uchaguzi ungalifanyika leo hii angepata ushindi wa 65% huku akifuatiwa kwa mbali na Rais anayemaliza muda wake akiwa na 28% na wagombea wengine waliobakia wakigawana 7%
Sawa ngoja tuone sanduku la kura litasemaje!

Ila nyinyi ni wanafki kiwango cha bombadier aisee! Mlimjaza upepo membe wee kwa thread za kila aina, kumsifia na kumpa kichwa kwamba mnamkubali, yeye ndie mrithi wa magu! Leo hii anaingia kwny konyanganyiro mmempa kisogo!? Sishangai saivi mnavomsifia lissu na kumnadi ati masihi wa bwana, ngoja tuone oct 28!
 
Kweli ni MAAJABU ya LISSU na ni kama mfalme, kwa lugha yako Lord denning na wengineo upande wake Lissu, kwamba:-
• kwa watu kuhudhuria mikutano ya YAKE kuona na kusikiliza Vioja, jinsi alivyo bingwa wa kuwadharilisha viongozi wa Serikali, hasa Rais Magufuli na watumishi wa Mungu, badala ya Hoja; na
• kuongelea nadharia za kisomi badala ya kuwaeleza wapiga kura jinsi gani ya kuondokana na masikini au Serikali yake itapata fedha ili afanye hayo anayoahidi kama vile bima kwa wote, kupunguza kodi, kugharamia mchakato wa Katiba mpya, wakati huo huo akiboresha huduma za jamii (afya, elimu, maji nk), na kuendesha Serikali, nk.

Je, ni kweli, kwa majigambo yake, nchi hii haiwezi kujitegemea pasipo mjomba wa nje? Kwa maana hiyo, akipewa ridhaa ya kuongoza nchi hii, mategemeo yake ni wajomba zake wa nje kuendesha Serikali na kugharamia miradi ya maendeleo? Au kwa jinsi anavyobeza miradi hiyo, akiita maendeleo ya vitu na "white elephant" ataweka pembeni?

Kwamba, anaishi kinadharia kutokujua uhusiano wa miradi ya maendeleo na maisha ya kila siku ya mwananchi! Kwa maana ya kuwepo huduma bora za jamii na za kutosheleza, miundombinu bora na imara ya usafiri, nishati ya umeme unaotosheleza na wa bei nafuu, nk?

Sasa naamini ndiyo maana Lissu hana lolote la kukumbukwa kama kiongozi wa kisiasa na mwanaharati wa miaka mingi, tangu utawala wa Baba wa Taifa aliyekuwa akimtukana ati leo hii anamsifia. Kwa mfano:
√ Jimbo lake alilokuwa mbunge kwa zaidi ya miaka kumi ni moja ya majimbo maskini kabisa; na
√ akiwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, hakuweza kushawishi viongozi wenzake wa chama kujenga japo ofisi ya Makao Makuu, wakati wanapata ruzuku na wabunge wao wakichangia kila mwezi.

Bila kumung'unya maneno, na msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Lissu, hakika atakuwa Kiongozi wa nchi wa ajabu kabisa kutokea katika dunia hii, akipewa ridhaa. Bahati mbaya kwake aendelee kuishi katika ndoto hiyo tu.
Bora umesema wewe!
 
Kuna Mambo ya ajabu nimeyashuhudia na ninaendelea juu ya huyu Lissu na Chadema yake.

Habari zake za kampeni zilikua zinahujumiwa na baadhi ya Vyombo vya habari zisitoke au kupungua umuhimu,lakini zinatoka.na watu wanahudhuria mikutano yake.

Sijaona bango hata moja la Lissu lakini watu wanafurika kwenye mikutano yake.

Chadema na Lissu hawana hell ya kutisha ya kampeni Kama CCM,lakini watu wanawachangia na kwenda kwa wingi mikutano yake.

Ndio mgombe anaepewa muda mrefu kuhutubia,lakini watu huwa hawachoki kumsikiliza,Ana akimaliza watu hutamani aendeleee kuhutubia.

Wahudhuriaji wa mikutano yake hutulia kumsikiliza Kama vile wapo darasani.

Ndio mgombea pekee Usalama wake uko mashakani.

Ndio mgombea pekee kampeni zake zinafatiliwa kwa umakini kabisa hapa EA a kwingine.

Ndio mgombea pekee anaechunguzwa au kufuataliwa kwa Siri na hadharani na majasusi.

Ndio mgombea pekee mikutano yake watu wana shamrashamra Sana wakati hawana pesa mifukoni,wala Hakuna wasanii isipokua timu yake inatembea na flashi ya nyimbo tu.

Idadi ya wahudhuriaji wa mikutano yake Ni halisi,Hakuna wasanii,hawajaletwa kwa maloli au mabasi.
Tofauti na Wahudhuriaji wa Lowassa.lowassa alikuja na wana CCM,Wana CUF,Wana NCCR,Wana NLD na CDM wenyewe.
Kwa kifupi Lowassa alibebwa na UKAWA.
Lisu Ni Jeshi la mtu mmoja.

Ndio mgombea pekee watu walikua na hofu huenda asipitishwe na NEC.

Ndio mgombea pekee anakabiliana na mpinzani mwenye nguvu kubwa lakini hawezekani.
CCM inatumia nguvu kubwa Sana kumkabili Lisu.
Pesa,Dola,Mahakama,Polisi,TISS,Jeshi,waganga.mamlaka ya anga,wadukuzi.

Anawaeleza watu machungu yake na Yao,anawaeleza makosa ya mtawala wa Sasa na anaeleza yeye atafanya nini.

Ndio mgombea ambae VIONGOZi wa serikali na CCm wanafuatilia hotuba zake kwa Siri Sana na zinawasisimua.

Lisu ndio mgombea aliewekewa vihunzi vingi Sana na amekua akivivuka,kesi,kifo,kuenguliwa,kutotangazwa tiviini,redioni na magazetini.
Na dalili zinaonesha atashinda lakini kutangazwa ushindi wake itakua mbinde,
Watabana kwa siku kadhaa lakini wanamtangaza tu.kwa sababu inaonesha jamaa Ni mtu wa kuvuka kwa taabu Sana.
Akitangazwa utatokea mlipuko mkubwa Sana wa furaha hapa Tanzania na Afrika mashariki.
Miongoni mwa watakaofurhi Sana Ni pamoja VIONGOZi wa serikali na makada wa CCM kwa uwingi wao.hamtaamini.
Historia ya Lissu imemlinda tangu hapo kale. Hajawahi kushinda kirahisi. Ubunge wake wa kwanza mwaka 2010 aliqekewa pingamizi peke yake akashinda, ushindi wake akanyanganywa na mahakama akashinda kesi. Kila anapopita anapita kwa taabu. Hata urais wa TLS alishinda kwa mbinde form ya NEC kuipata mbinde kutangazwa ugombea ilichukua masaa 12 kwa kitendo cha kutangaza dakika 10 tu
 
Wana CCM wanatambua kabisa Tundu Lissu anakubalika na kuungwa mkono na wananchi wengi sana huku Tanganyika. Ni sawa kabisa na Maalim Seif kwa kule Zanzibar. Mpaka sasa wanatambua kura ya maoni inaonyesha endapo uchaguzi ungalifanyika leo hii angepata ushindi wa 65% huku akifuatiwa kwa mbali na Rais anayemaliza muda wake akiwa na 28% na wagombea wengine waliobakia wakigawana 7%
Swadatka
 
Historia ya Lissu imemlinda tangu hapo kale. Hajawahi kushinda kirahisi. Ubunge wake wa kwanza mwaka 2010 aliqekewa pingamizi peke yake akashinda, ushindi wake akanyanganywa na mahakama akashinda kesi. Kila anapopita anapita kwa taabu. Hata urais wa TLS alishinda kwa mbinde form ya NEC kuipata mbinde kutangazwa ugombea ilichukua masaa 12 kwa kitendo cha kutangaza dakika 10 tu
Duh, acha fix mkuu! Fomu ya nec ameenda kuchukua kweupe tumeona hiyo mbinde ya wapi? Kwa nini kusema uongo mahali pasipostahili?
 
Hebu rudia kusoma ulichokiandika alafu usome swali langu uone kama vinaendana mkuu

Nimekujibu huelewi nn
Nilimuuliza bwana akaniita tukakaa akaniambia lissu ndio masihi wake kwa nchi hii na ukanda wote wa maziwa makuu
 
Uzuri wa Lissu ni kwamba,anafanya kampeni uku anakuelimisha ujue haki zako za msingi,dhuluma na uonevu.labda uwe na kichwa kizito ndo utashindwa kumuelewa.Yuko tofauti na yule mgombea mwingine wakusema amejenga hichi na kile mbele ya watu wasiojua hata haki zao za msingi.,na kamwe hawezi kuwaambia swala la wao kuelimika.Kwahiyo Lissu sio mchoyo wakuelimisha watu.
 
Huku mtaani watu hawana habari kabisa na lissu
Kuna wamoja jana wamevaa nguo za Chadema wakaishiwa kudhihakiwa niliwahurumia sana
Umepewa kichwa ubebee meno na wala si kutumia ubongo kupambana na changamoto za kimaisha.
 
Back
Top Bottom