Uchaguzi 2020 Maalim Seif: ACT Wazalendo hatuna mpasuko lakini Membe anataka kuwaaminisha Watanzania hivyo. Adai Mzee wa Ubwabwa ni bora kuliko Mgombea wao

Uchaguzi 2020 Maalim Seif: ACT Wazalendo hatuna mpasuko lakini Membe anataka kuwaaminisha Watanzania hivyo. Adai Mzee wa Ubwabwa ni bora kuliko Mgombea wao

..ugomvi wao wasubiri baada ya uchaguzi.

..muda huu utumike kuwatafutia kura Maalim Seif, Tundu Lissu, wabunge, na madiwani wetu.
Hakuna muda huo..waache wagombane mpaka wapate ufumbuzi Nani ni Nani..waje baada ya tarehe 28 tuonane
 
Fedha za Kampeni za Membe zimedhibitiwa Airport akitokea Dubai na wasaidizi wake wamekamatwa!

Sasa hizo kampeni atafanyaje peke yake bila ya sapoti ya secretariet ya ACT?

Lipumba mara zote za uchaguzi alikuwa anasimama kwa miguu yake na wajanja wenzie wa mjini, pesa zote za kampeni mnapeleka Znz kunajisi Mapinduzi mnataks Jasusi afanyaeje?
Hehe..mnatufurahisha..mafahari wawili hawakai zizi moja..mlikuwa na mbweeeembwe Kama mmepata kumbe mmepati
Maalim mkorofi sana huyu babu,kaingia ACT juzi tu keshaanza migogoro,kwanini walimpa baraka zote Membe za kupeperusha bendera ya Urais ilhali wanajua kabisa hafai!?
Ndio maana prof Lipumba alimfukuza CUF, amebaki ana hanghang akaonewa huruma na Zito
 
Ha ha ha,sio kuwachanganya,,,yaani mmenisurika sana kubugi step,,ndo mkome kudandia dandia wagombea
 
Mwenyekiti wa Act taifa anaongea na wanahabari jijini Dar es salam

--

Nimesikitika sana kwa aliyoyazungumza ndugu yangu Bernard Membe, ACT-Wazalendo kupitia mkutano mkuu wa Taifa ulisema tunataka mabadiliko, mkutano mkuu ukatoa mamlaka kwa uongozi ili kuhakikisha tunashirikiana na vyama vya wenzetu ambavyo ni makini....
Membe katumwa na CCM, makosa ya Mbowe 2015
 
"Jasusi mbobezi" busy akikamilisha kazi aliyotumwa na chama chake. Ni kweli kuwa Zitto hajajifunza toka CHADEMA na Lowassa 2015 au ndio ule ule "umamluki" uliomfukuzisha CHADEMA na yeye yupo kazini?
 
Jasusi is there to stay

Uchaguzi ukimalizika anaukurupusha mgogoro kama wa NCCR ya Mrema na Mabere Marando 1995~2000

Siku nyingine CCM ikigombana na wanachama wake wapinzani wapunguze shobo
Tunahama tunamwachia chama na kuunda kipya kama tulivyomwachia Lipumba.
 
Mgombea urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa amesikitishwa na suala la mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Bernard Membe kusema ataendelea kuwania urais kinyume na msimamo wa chama.



MEMBE-NA-MAALIM-WEB.jpg

Maalim Seif na Bernard Membe
Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo Oktoba 20, 2020 Jijini Dar es Salaam, wakati akiongea na vyombo vya habari, ambapo amesema kuwa msimamo wa kumuunga mkono mgombea urais wa CHADEMA Tundu Lissu, ulitolewa na chama cha ACT-Wazalendo na wala sio wa kiongozi mmoja mmoja.

Maalim Seif ameeleza kuwa wao kama ACT-Wazalendo waliamua hivyo baada ya kuona mgombea urais wao haonekani kwenye kampeni kama wagombea wengine wa vyama vingine na wakaamua wamuunge mkono Tundu Lissu kutoka CHADEMA.

“Tuliona mgombea urais wetu haonekani kwenye kampeni za uchaguzi mkuu, bora hata Mzee wa ubwabwa kuliko mgombea wetu, ndio maana tukakubaliana kumuunga mkono Lissu,” - alisema Maalim Seif.

Maalim Seif ameongeza kuwa, “ACT- Wazalendo tulimwambia mapema Bernard Membe, wakati anakuja kwenye chama chetu, kwamba katika hiki kitu cha uchaguzi huwa tunashirikiana na chama makini na alikubali”.






 
Fedha za Kampeni za Membe zimedhibitiwa Airport akitokea Dubai na wasaidizi wake wamekamatwa!

Sasa hizo kampeni atafanyaje peke yake bila ya sapoti ya secretariet ya ACT?

Lipumba mara zote za uchaguzi alikuwa anasimama kwa miguu yake na wajanja wenzie wa mjini, pesa zote za kampeni mnapeleka Znz kunajisi Mapinduzi mnataks Jasusi afanyaeje?
Hela gani za kampeni unazungumzia mbona Maalim Seif na Zitto wanapanda jukwaa moja, kwanini yeye ,asionyeshe ushirikiano wa kupanda jukwaani hata mara moja, Membe ni garasa tu
 
Mwenyekiti wa Act taifa anaongea na wanahabari jijini Dar es Salaam

--

Nimesikitika sana kwa aliyoyazungumza ndugu yangu Bernard Membe, ACT-Wazalendo kupitia mkutano mkuu wa Taifa ulisema tunataka mabadiliko, mkutano mkuu ukatoa mamlaka kwa uongozi ili kuhakikisha tunashirikiana na vyama vya wenzetu ambavyo ni makini...
Mshindi wa Urais wa Zanzibar huko nyuma huamuliwa na kura zisizozidi elfu 20 hivi na ubunge/ udiwani kura elfu 3 au chini kidogo. Sasa Maalim anapowachochea wafuasi wake wafanye vurugu tarehe 27, je haoni kuwa wakikamatwa hata watu elfu 10 tu itampunguzia kura tarehe 28 hivyo kumkosesha ushindi kama ilikuwa ashinde au hata ubunge/ uwakilishi?

Afuate sheria kwani tarehe 27 na 28 anaruhusiwa kuwa na mawakala na pia daftari la wapiga kura wamepewa.

Uchaguzi wowote ule kuna kushinda na kushindwa awe tayari kwa matokeo yeyote.

Pia Maalim anamdhalilisha Membe hadharani jambo ambalo sio uungwana. Huyu Membe walimuona mali ndio maana walienda nyumbani kwake Mtama kumuomba ajiunge nao na kumuahidi fursa ya kugombea urais.

Sasa anamkana kwa sababu anaona fursa ya kuibomoa Tanzania ni kubwa chini ya Lissu kwa sababu ya mihemuko ya Lissu na urahisi wake wa kuchotwa na kuzungukwa lakini Maalim anajua kuwa Membe hawezi kukubali kuibomoa Tanzania ili tu kukidhi maslahi binafsi ya Maalim na masters wake wa nje.
 
Membe hakupaswa kukaribishwa hata msalani, hili ni donda ndugu la upinzani akitoka ccm, asiingie chumbani...kibarazani panamtosha, tena cha uani.
 
Ni dhahir shahir kwamba mwenendo wa wanachama wa CCM kuhamia upinzani na baadae kurudi tena CCM utaendelezwa na Membe pia. Hii inadhihirishwa na kutokuwepo kwa kampeni ya maaana katika kugombea nafasi ya urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo na badala yake tumewahi kumsikia kiongozi wa chama hicho akimpigia debe Tundu Lissu.

Zipo habari pia za kuwepo kwa mfarakano mkubwa ndani ya chama hicho kulingana na suala hilo. Kitendo cha SSH kwenye kampeni za TL ni udhahidi tosha kuwa Membe is done and it wasn't meant to be. Hasta la vista Membe.
 
Habari wana jf, maalim seif ameongea na waandishi wa habari na kuzungumzia suala la membe huku akimtolea maneno makali sana.

Nimeshindwa kushangaa, leo hii maalim seif unasema membe katumwa? Mbona siku ya kumpitisha pale chamani kuwa mgombea uraisi ulimsifia sana?
Membe unalo la kujifunza, pole sanaView attachment 1605967View attachment 1605968View attachment 1605969View attachment 1605971

Safi kabisa Maalim, kama joka la kibisa linaleta za kuleta kinyume na makubaliano ya vikao ambavyo na yeye alikuwepo, hamna haja ya kumumunya maneno - mpasue hadharani asije waingiza choo cha kike wkt mkikaribia kufikia malengo ya kuing'oa ccm Bara & Visiwani!
 
Safi kabisa Maalim, kama joka la kibisa linaleta za kuleta kinyume na makubaliano ya vikao ambavyo na yeye alikuwepo, hamna haja ya kumumunya maneno - mpasue hadharani asije waingiza choo cha kike wkt mkikaribia kufikia malengo ya kuing'oa ccm Bara & Visiwani!
Kitu nilichojifunza ni kuwa,ukikuta mtu ni muislamu kweli kweli huwa hawaogopi kusimamia ukweli. Seifu asingekuwa muumini kweli Kweli wa imani yake angekuwa ashanunuliwa na CCM kwa gharama kubwa. Hivi sasa watu wanaoshikilia upinzani Tanzania ni Seifu na Mbowe pekee
 
Back
Top Bottom