Leo nizungumzie jambo moja ambalo binafsi naona ni tatizo kwa sasa.
Chadema ni chama kikubwa sana na kina wafuasi wengi, ila nathubutu kusema wafuasi/mashabiki wa chadema na upinzani humu mitandaoni ni tatizo kubwa sana.
Wote tunakumbuka humu kila ilipoitwa leo zilijazwa thread za kumsifia Membe kwa kila alichofanya na kusema, lakini sasa hivi wamemgeuka na kumuita pandikizi.
Hii tabia wameifanya kwa watu wengi sana ila kwa Membe naona sasa sio fair kabisa.
Kumbuka kuwa Membe ni binadamu na mwanasiasa hivyo kama hapitii maoni ya mitandaoni basi kuna watu wake wa karibu wanapitia na hivyo taarifa anazipata.
Pengine baada ya kuona upepo wake humu mitandaoni unavuma vizuri aliamua kufanya alichofanya na kujitosa kugombea Urais bila kujua watu wengi wa mitandaoni ni wa kupelekwa na upepo.
Nakumbuka kule twitter Membe alibatizwa jina la."role model" na vijana wa huko, ila sasa hivi matusi anayotukanwa huwezi amini.
Ilifikia kipindi Membe akiweka hata post/tweet ya kawaida tu kule twitter basi zitakuja comments nyingi sana za kumsifia na kumtukuza kwa kila namna kwa maneno yote matamu.
Membe amefanya ambayo nyie wenyewe mlikuwa mnatamani, kwa nini sasa hivi mumtukane? Sio fair.
Hii tabia nashauri washabiki wenzangu tuiache, ipo siku, nasema ipo siku huyu mgombea fulani naye yatamkuta. Ukitakana kujua hilo angalia aliyegombea mwaka 2010, 2015 yanayomkuta huko mitandaoni kwa kutukanwa kwa watu wale wale waliokuwa wanamtukuza kwa kila aina ya maneno matamu.
Hapa chini nimeweka link thread moja humu ambayo ilikuwa na comments zaidi ya 3000 kuhusu membe mwaka 2018, angalia vijana wa chadema wakimsifia membe kwa kila aina ya neno tamu
Uchaguzi 2020 - Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania
Hapa nimeweka picha za tweet zake huko twitter, ona wale watu walivyokuwa wanamtukuza
View attachment 1606246