Maalim siku zote focus yake ni Zanzibar tu na anavitumia vyama vya siasa vya bara kama vyombo vya kufikia lengo lake. Alikichukua chama cha wakina Aleck Che Mponda na kukigeuza kuwa chama ambacho priority yake kubwa ni masuala ya Pemba na Unguja. Ameingia sasa ACT-WAZALENDO na anarudia mchezo ule ule. Nasema hivi kwa sababu:
1. Anaposema wanachama wa ACT-WAZALENDO waliulizwa kuhusu hatua ya kuingia kwenye GNU sidhani kama anamaanisha wanachama walioko Kibondo au Newala. Kwake yeye mradi wanachama walioko Pemba na Unguja wameulizwa mchezo umekwisha.
2. ACT Wazalendo ni chama cha kitaifa na hivyo kabla ya uamuzi wowote kuchukuliwa walipaswa kuangalia athari au faida yake kwa Chama kwa ujumla na sio kwa upande mmoja wa Muungano. Mpaka sasa hivi tunachosikia ni faida tu kwa wanachama walioko Zanzibar lakini hatusikii lolote kuhusu faida ambazo mwanachama wa Kibondo atapata kutokana na hatua hii.
3. Lugha ya kuwa Zanzibar sio Tanzania Bara ni ya kuwakataza hata wanachama wenzake wasio wazanzibari kushiriki katika mjadala unaohusu uamuzi wao wa kujiunga katika SUK.
4. Kwa ACT-WAZALENDO ( Bara) uamuzi huu unaweza kuwaathiri sana maana wamejiweka wazi kwa tuhuma za kuwa wao sio sehemu ya upinzani makini bali ni sehemu ya utawala uliopo. Hali hii inaweza kukubalika Zanzibar lakini itawaathiri kwa wanachama wao waliokipigania chama chao kwenye mikoa kama Lindi na Mtwara.
5. Kwa matamshi yake tayari anajihesabu yeye ni sehemu ya utawala wa Zanzibar. Ameanza mpaka kutumia lugha za vitisho dhidi ya wale ambao hawakubaliani na uamuzi wake. Kwa kufanya hivi anaonyesha yeye by nature ni authoritarian na hataki watu watofautiane nae. Hii inasikitisha kwa sababu inaonyesha kuwa si muumini wa Demokrasia na kuna uwezekano mkubwa kama angekuwa na uwezo angefanya vitendo hivyo hivyo ambavyo alifanyiwa.
Hata hivyo pamoja na kusema hivi, ninawaombea heri ACT-WAZALENDO na viongozi wao katika safari yao ya kutuonyesha kuwa kuna njia mbadala. Mafanikio yao yatakuwa yetu sote. Na wakionyesha kuwa mawazo yangu ni potofu sitasita kurudi tena humu na kuwaomba msamaha.
Amandla...