Mheshimiwa, ni lazima nikiri kuwa nimeangalia Kanuni za Bunge na ni kweli kuwa hakuna takwa la kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Kwa mujibu wa kanuni zilizopo ni kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani itaundwa pale tu ambapo vyama vya upinzani vitapata angalau asilimia kumi na mbili na nusu za wabunge wote. Sijaona pia sehemu ambapo inasema kuwa ni lazima Mwenyekiti wa Kamati Fulani atoke Upinzani. Kama niko sahihi basi Spika hana hata haja ya kubalisha kanuni maana ana mamlaka ya kuendesha bunge bila kuwepo kwa Kambi Rasmi ya Upinzani. Lakini hii haiondoi kuwepo kwa "leverage" kwa CDM maana itakuwa vigumu sana kushawishi wananchi na dunia kuwa nchi yetu ni ya demokrasia ya vyama vingi wakati wabunge wote ni wa Chama Kimoja, takriban madiwani wote ni wa chama hichohicho na wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa ni wa chama kilekile. Aidha, inasemekana kuwa sharti la PAC kusimamiwa na upinzani linatoka kwa "Development Partners" wetu na hii ndio inawapa "leverage" nyingine CDM. Spika anaweza kuendesha Bunge bila kuwa na upinzania rasmi ndani yake lakini athari yake ni kupewa talaka na hao tunaowaita mabeberu na wahuni. Bila shaka ndio maana zinafanyika juhudi za ziada kuhakikisha bungeni kuna wabunge wa upinzani zaidi ya hiyo asilimia inayotakiwa, ambayo kama kutakuwa na jumla ya wabunge 395 basi angalau 45 ( ila kuna sehemu nimesoma idadi inayohitajika ni 30) watahitajika. Sasa hivi wako 25 ( 19 viti maalum CDM, 1 wakuchaguliwa CDM, 1 CUF na wanne ACT Wazalendo. Bado safari ni ndefu.
Amandla...