Maalim Seif ateuliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuwa mgombea Urais Zanzibar

Maalim Seif ateuliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuwa mgombea Urais Zanzibar

Hatimaye Mwenyekiti wa ZEC amethibitisha kuteuliwa kwa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar.

=====

ZEC YAMPITISHA MAALIM SEIF KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imempitisha Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif kuwa mgombea wa Urais baada ya kuwekewa mapingamizi 2 siku ya jana

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Hamid Mahmoud amesema kuwa rufaa iliyokatwa dhidi ya Maalim haina mashiko

#Uchaguzi2020

Zaidi, soma: Zanzibar 2020 - Njama? Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Maalim Seif awekewa Pingamizi
Iwe tayari kumpa haki yake ya ushindi pale itakapobainika hivyo.
 
Huyu Seif inasemekana sijui ni mtu wa system, aya majina ya kuitana watu wa system hakuna uzalendo wowote.

2015 alishinda uchaguzi ila akaifyata, 2020 pia ni hivyo hivyo tu. Tanzania tunahitaji watu wasioufyata kama akina Lissu, Lema n.k

Hatuwezi kupoteza muda wetu na nguvu zetu kumuunga mkono mtu ambae upande wa pili wanajiitana wa system, hawezi kufanya maamuzi magumu mtu kama huyu.

Yangu ni hayo, nimemaliza.
Usijitoe ufahamu wewe, Lissu alifutwa ubunge akaufyata in maana hujui?
 
Sitasahau kampeni za mwaka 2005 wafuasi wa CUF na CCM walikutana maeneo ya Kwerekwe. Kama kuna siku ambayo nilikuwa naelekea kupoteza macho ni siku hiyo. Mawe yaliyokuwa yanarushwa kutoka pande ni kama mvua
 
System...

Wajanja washajua...mchezo tunaochezewa siku zote!
 
Ndo kapata uungwaji zaidi bila kutegemea kwa walicho mfanyia
 
ilishiriki uchaguzi wa mwaka jana kama kiongozi chama changu mwaka jana, mzee wanarough mbaya sana hao ccm na wasimamizi, forgery ndo kazi yao na wanabariki balaaa
Safari hii kila mhusika akae akijua mzigo wake ataubeba yeye mwenyewe. Safari hii kina ni kirefu sana, chukueni tahadhari msitumbukie haijalishi wewe ni nani, utawajibika kwa ngazi yako. Nchi hii imechezewa sana.
 
Back
Top Bottom