Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Mleta mada yupo sahihi maana kwa sasa anawaza kwa kutumia kichwa cha juu , which is good😁😁, tusubiri akianza kuwaza kwa kutumia kichwa kidogo.atarudi hapa home sweet home Jf kwa ushauri mwingine😁😁😁😁
 
Mleta mada yupo sahihi maana kwa sasa anawaza kwa kutumia kichwa cha juu , which is good[emoji16][emoji16], tusubiri akianza kuwaza kwa kutumia kichwa kidogo.atarudi hapa home sweet home Jf kwa ushauri mwingine[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sijawahi kufikiri kuwa hata wewe mchokozi na mtundu kiaina
 
Haya mambo nchi za wenzetu ni ya kawaida sana tatizo huku shit hole tunaona ya ajabu kwasababu ya roho mbaya.
Usemayo ni kweli, kuna mzee mmoja Danish alioa single parent tena mkurya toka Tz alikuwa masomoni huyo Madanish akamwambia tulee mtoto wako tusizae na hadi leo wanazeeka pamoja
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Eti???
Nisimpende hivyo???
Kwa kifupi ninayemhurumia ni yule aliyekataliwa.
Sioni nafasi ya upendo wetu kuendelea zaidi ya heshima na urafiki wa kawaida.
Sikusudii kumfanya kuwa karibu yangu zaidi ya kumpa sapoti ndogo ndogo wakati huu mgumu kwake.
Ninajua thamani ya mtu kukukali ngaa kidogo wakati wa mapito yako magumu.
Ni hivyo tu Lucky
 
***********************
Nikasepa zangu mkoani kikazi. Siku napokea simu toka kwa Mama kijacho,alinielezea "Kibuyu hongera umepata mtoto wa kiume." Nilifurah sna si kwa kauli yake ya kunimilikisha mtoto, bali kwa kuwa sehemu ya uhai wa huyo mtoto.
Baada ya saa 24 akaruhusiwa kutoka Amana hospitali.

Mwajuma akawa ananiambia rafiki zake wanataka kujua jina la mtoto, kwahiyo nichague jina nimpe mtoto. Nilimwambia awape nafasi wazazi wampe jina mjukuu wao. Akasema nitoe Mimi baba. Ukatokea mvutano wa kijinga, sikuwa tayar kumpa mtoto jina. Mimi n mkristo wao n waislamu.
Nilikuwa na sababu, daima sipend unafiki. Kwani nilijua lazima mtoto atapewa jina lingine tu. Kuepusha hilo sikutoa jina.

Kesho yake jioni mwajuma alinipigia akiniambia mama ake anataka kuongea nami. Nikaona mambo yameanza; nikamwambia kwasasa nipo kwenye kelele anipe dakika kumi ntawapigia. Nikamuuliza mama ulimwambia ukweli kuwa Mimi siye?? Alisema hajamwambia. Sikutaka kukuza mada nikanyamaza tu.

Mama alichoniambia ni kunishukuru kwa kumjali mwenzangu, "ila familia inakuomba ukirudi uje nyumbani tuzungumze. Yaliyopita yamepita mwanangu, kwani tumeshakuwa ndugu. Hongera sana baba kwa kupata mtoto wa kiume mwenye afya!"
Nikaitikia "Asante sana mama, nawe hongera kwa kupata mume."
Akacheka kisha akasema haya ongea na mwenzio. Akampa simu mwajuma.
Tukaongea kidogo tu.

*****************
Mwajuma alinisumbua wiki kuhus jina la mtoto nami nikagoma kutoa jina. Akampa jina Hamadi. Binafsi mpaka hapo sikuwa na wazo kuendelea nae huyo binti; mkataba wetu akishajifungua mwisho.

Ikafika karibia na 40,akaniambia anataka kumfanyia kisomo mtoto kwani anamtoa nje. Nikamuuliza anataka nifanyaje? Akaniambia anahitaji pesa. Nikamwambia afanye budget ndogo anipe. Kesho yake jioni akanipa budget. Nikamtumia pesa. Nikamuomba Shem akanunue nguo na bag la mtoto nikamtumia pesa. Maana Shem wangu tulielewana sana.

40 ikafana kwa kila lililopangwa. Nikapigiwa simu na kupewa shoga zake wote waliokuwepo niongee nao. Shem nae akanipigia akinipongeza kumsaidia mwajuma.

Baada ya kurudi nikaletewa mtoto nimuone. Alikuwa mtoto mzuri mwenye afya njema. Nilifurahi sana hasa mtoto aliponifurahia.
Nikamwambia kesho nakuja kwenu. Akafurahi sana. Ila nikamwambia nitasema ukweli tu. Nikamuona amekuwa kimya.

Kesho yake nikajiandaa kwenda kwa wakwe nikiwa na rafiki zangu wawili na bro na mkewe.

Itaendelea.........
 
Kwanini usiangalie uwezekano wa kumuoa? Unataka apate njemba mwingine amnyanyase kisha nawe uanze tena kukosa raha mama wa mwanao ananyanyasika?
Mkuu kuoana hakuhitaji huruma wala fadhila, ni upendo wa dhati katka hali zote.
 
We jamaa una akili sana, na una upendo sana, Mungu akubariki sana kwa utashi huo, mimi naamini ukifanya hivyo Mungu atakupa zaidi, cha kukusisitiza usimshirikishe kila kitu, hivyo ambavyo vipo moyoni viweke moyoni sio lazima kila kitu umwambie, msome tabia huyo mdada, all in all hongera sana.
 
Naogopa sana kuahidi kwani mimi ni binadamu.
Kitu ambacho kipo tayari ni kiwanja nacho sitamwambia hadi kila kitu kimekaa sawa na nitafanya kisheria.
Asante
 
Wazazi wako unawasaidia kweli? Una matatizo sio bure.
Tusilinganishe hizi hoja na kuwalinganisha wazazi wako na wachumba tunaokutana nao,

Wazazi wako ni watu muhimu sana hapa duniani sio wakulinganishwa tu unavyojisikia, wana heshima yao aiku zote za maisha yetu mpaka kifo
 
Mkuu sijawahi kuwaza ku fake jambo nyeti kama hili.
Hii ni habari ya kweli na maamuzi haya yana siku 3.
Najua ni magumu hadi najishangaa lakini sitarudi nyuma kwani nilifanya kwa msukumo wa ndani ya moyo

Pamoja na unafanya kitu cha kiungwana sana, na moyo wako umerizia basi we fanya na jitoww kwa moyo mmoja, ila sasa pia usifanye kwa matakwa ya mapenzi ya mwanadada, baadae ukaja jutia sana, nenda taratibu na kwa umakini sana, wanawake wana siri kubwa sana huwezi juwa yeye anakuwazia nini?
 
Nitazingatia jirani, asante
 
Umefanya jambo jema lakini fahamu mtoto akikua na kupata ufahamu atamtafuta baba yake halisi!
 
Tukipata mwingine aliyekataliwa tukujulishe au wametosha mkuu
 
Itakuwa vizuri amtafute babake lakini alishapata malezi bora
Jirani watu hawana utu tena ndiyo maana wanashanga mbona unawezaje hili, ila mimi natambua unaweza kwa kuwa unalifanya kutoka moyoni, na nina uhakika unafanya kwa mapenzi ya dhati kabisa ya mtoto na maa yake, mambo ya a good Samaritan hayo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…