***********************
Nikasepa zangu mkoani kikazi. Siku napokea simu toka kwa Mama kijacho,alinielezea "Kibuyu hongera umepata mtoto wa kiume." Nilifurah sna si kwa kauli yake ya kunimilikisha mtoto, bali kwa kuwa sehemu ya uhai wa huyo mtoto.
Baada ya saa 24 akaruhusiwa kutoka Amana hospitali.
Mwajuma akawa ananiambia rafiki zake wanataka kujua jina la mtoto, kwahiyo nichague jina nimpe mtoto. Nilimwambia awape nafasi wazazi wampe jina mjukuu wao. Akasema nitoe Mimi baba. Ukatokea mvutano wa kijinga, sikuwa tayar kumpa mtoto jina. Mimi n mkristo wao n waislamu.
Nilikuwa na sababu, daima sipend unafiki. Kwani nilijua lazima mtoto atapewa jina lingine tu. Kuepusha hilo sikutoa jina.
Kesho yake jioni mwajuma alinipigia akiniambia mama ake anataka kuongea nami. Nikaona mambo yameanza; nikamwambia kwasasa nipo kwenye kelele anipe dakika kumi ntawapigia. Nikamuuliza mama ulimwambia ukweli kuwa Mimi siye?? Alisema hajamwambia. Sikutaka kukuza mada nikanyamaza tu.
Mama alichoniambia ni kunishukuru kwa kumjali mwenzangu, "ila familia inakuomba ukirudi uje nyumbani tuzungumze. Yaliyopita yamepita mwanangu, kwani tumeshakuwa ndugu. Hongera sana baba kwa kupata mtoto wa kiume mwenye afya!"
Nikaitikia "Asante sana mama, nawe hongera kwa kupata mume."
Akacheka kisha akasema haya ongea na mwenzio. Akampa simu mwajuma.
Tukaongea kidogo tu.
*****************
Mwajuma alinisumbua wiki kuhus jina la mtoto nami nikagoma kutoa jina. Akampa jina Hamadi. Binafsi mpaka hapo sikuwa na wazo kuendelea nae huyo binti; mkataba wetu akishajifungua mwisho.
Ikafika karibia na 40,akaniambia anataka kumfanyia kisomo mtoto kwani anamtoa nje. Nikamuuliza anataka nifanyaje? Akaniambia anahitaji pesa. Nikamwambia afanye budget ndogo anipe. Kesho yake jioni akanipa budget. Nikamtumia pesa. Nikamuomba Shem akanunue nguo na bag la mtoto nikamtumia pesa. Maana Shem wangu tulielewana sana.
40 ikafana kwa kila lililopangwa. Nikapigiwa simu na kupewa shoga zake wote waliokuwepo niongee nao. Shem nae akanipigia akinipongeza kumsaidia mwajuma.
Baada ya kurudi nikaletewa mtoto nimuone. Alikuwa mtoto mzuri mwenye afya njema. Nilifurahi sana hasa mtoto aliponifurahia.
Nikamwambia kesho nakuja kwenu. Akafurahi sana. Ila nikamwambia nitasema ukweli tu. Nikamuona amekuwa kimya.
Kesho yake nikajiandaa kwenda kwa wakwe nikiwa na rafiki zangu wawili na bro na mkewe.
Itaendelea.........