Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Acha ujinga ww. Kama alikuwa na mapenzi na wewe angekutafuta mkawa wote. Tupo busy na maandalizi ya kampeni. Huyo dadani muhuni nadhani hauwajui wanawake wapore .
Wanawake wapoRE ndo wapoje?
Nafikiri kweli hawajui wanawake wapore.
 
Hongera sana.utabarikiwa zaidi.ya uliyombariki huyo dada.binadam wema wapo wengi sana
 
Njoo basi tutazaa wetu mmoja tupate 🖐🏼 eeh baba ila mashart sitaki maana hawa 4 wote wakiume usije sema unataka wa kike 😂😂😂😂
Hakuna shida kama ni wa kiume...watoto ni baraka toka Kwa Mungu, lini naanza majukumu rasmi!
 
Wewe ni baharia mwelevu ........nimekupa maksi 💯.............ikitokea wewe ndio muwe 100 nadhani hatutawaona single mother wala watoto wa mitaani.......hongera sana na Mungu akibariki sana....DADY MATERIAL
 
Huwezi kujimilikisha damu ya mtu mwingine kirahisi hivyo. Provided alishamtaarifu mzazi mwenzie kuhusu mimba basi wewe hauna chako hapo. Mtoto akizaliwa jamaa lazima aje amuone mtoto wake na pia kama ni damu yake ataclaim mtoto wake kama baba hapo baadae.

Umefikiria kirahisi sana kwa kuomba tu jina la mtoto apewe la kwako ila hiyo sio tiketi ya wewe kuwa baba kwa hali yoyote. Mie nadhani labda ungemuoa huyo dada ili uwe at least baba wa kambo laikini si kwa style uliyotumia.

Njia za kuasili mtoto kwa nchi yetu ni ngumu sana sio mizaha mizaha kama hii unayoifanya.
 
Huwezi kujimilikisha damu ya mtu mwingine kirahisi hivyo. Provided alishamtaarifu mzazi mwenzie kuhusu mimba basi wewe hauna chako hapo. Mtoto akizaliwa jamaa lazima aje amuone mtoto wake na pia kama ni damu yake ataclaim mtoto wake kama baba hapo baadae.

Umefikiria kirahisi sana kwa kuomba tu jina la mtoto apewe la kwako ila hiyo sio tiketi ya wewe kuwa baba kwa hali yoyote. Mie nadhani labda ungemuoa huyo dada ili uwe at least baba wa kambo laikini si kwa style uliyotumia.

Njia za kuasili mtoto kwa nchi yetu ni ngumu sana sio mizaha mizaha kama hii unayoifanya.
Haja yangu sio kuitwa baba kwa style hiyo, bali haja yangu ni kuwa baba kwa aliyekataliwa na baba, kumpa matunzo na fursha atoayo baba.
Ikiwa baba halisi atajitokeza mapema nabkumpa furaha mimi sina neno kabisa na hata akimuoa huyo binti pia sina kikwazo labisa.
Nataka huyu binti asipitie uzazi kwa kinyongo, maumivu na machozi pia
Ninajua hali warnazopitia mabinti wakitelrkezwa katika hali hiyo, wanaumia, wanarlia sana lkn nani awasrikiloze.
Jramii huwargeuka na kuwaona malaya.
Wrazazi hruwachukiat kwa rkuona wameletewa aibu.
Wanaume huwaona hawana thamani tena.
Je harwarsitahili huruma na upendo wrtu kama jamii???/?
amu
Khantwe
luckyline
Melanny
 
Anafahamu kila kitu kuhusu mimi, hajaniomba bali mimi nimetaka.
Pili baba halisi ana uwexo mkubwa tu lakini hakuona haja ya kulazimisha mambo wala kutaka kwenda eti kwa mke wake.
Pili hata kwao wako vizuri kiasi sio hahehohe.
Kama ulivyolileta ili jambo hapo kupata maoni nashauri uwaeleze na wazazi wako watoe maoni yao. Wewe si peke yako kuna ukoo wako na kuna maamuzi lazima beneficiary na warithi wako wayajue. Ingawa najua hiyo process yako umeifanya kienyeji na haina legal back up. Mtoto ni damu ya mtu so huwezi kumnyang'anya mwenye nayo kwa kuomba tu uandikwe kwenye kadi kama baba. Mbona kuna watoto wana kadi mbili za kliniki na kila moja ina jina la baba tofauti wanawake wanatumia huu ujanja kutupiga lakini mwisho wa siku baba halisi atajulikana tu na atakuwa responsible kisheria

Nimekumbuka mbali uliposema binti kwao wako vizuri kiasi. Ndugu yangu mambo yanabadilika na muda mfano mimi nimekulia Temeke Mwisho na sasa hivi nimejenga na naishi ushuani na wale tuliosoma nao enzi hizo wakitokea ushuani sasa hivi wamepigika wambwele huko pembezoni mwa mji. Muda ni kitu cha ajabu sana
 
Yuko desperate jamaa akibadili mawazo atarudi kwake hili bora nilifanye nikiwa na familia yangu
 
NI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI

Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.

Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.

Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina. Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.

Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka).

Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute. Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale. Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.

Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa. Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri. Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea na walikuwa wamepanga kuoana.

Nini kilitokea kati yao?

Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake. Alifanikiwa kwenda na kurudi. Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.

Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito. Nikampa hongera zake. Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi. Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?

JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja

Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena. Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.

Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye ana familia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.

Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto akiwa tumboni wazazi wanajua hili.

2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia ya ajabu.

MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa wa hiyari na apewe ubini wa jina langu kama baba alikubali hili kwa mshangao mkubwa sana (Haya[emoji116]sijamshirikisha)

2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito

3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya mama na ya mtoto atakaye zaliwa

4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru wake.

5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.

Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.

Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi sio nyumbani kwangu lakini. Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.

Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.

Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;

Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.

Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi. Muwe na wakati mwema wote.
(KATIKA HILI SITEGEMEI ANY RETURN)

Like yangu ni ya 88 pangekuwa na option mbili za kulike kma wewe ni female au male tujue hayo maamuzi ni jinsia ipi inayapenda, mimi ni male
 
Back
Top Bottom