Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Umeanza kushangilia ushindi mapema mno,mchezo wa mahusiano una trick nyingi mpk kuushinda.
Kila la kheri mkuu ni wachache sana wenye moyo waa ivyo Tanzania bara na visiwan
 
Umeanza kushangilia ushindi mapema mno,mchezo wa mahusiano una trick nyingi mpk kuushinda.
Kila la kheri mkuu ni wachache sana wenye moyo waa ivyo Tanzania bara na visiwan
Mkuu sishangilii ushindi, huu ni mwanzo wa mbio ndefu...nipe pumzi kwa ushauri mkuu
 
Mhh wew utakuwa fisad had viwanja unaenda kununulia unborn child , na wa kwako umewanunulia tayari

Swal la kumpa faraja ili asipatwe na sonona ni jambo jema tu ..ila hawa ndugu zetu hawatabiriki nakuambia cku utakuja kusikia ana mtu mwingine kisirsiri ndio akili itakah sawa mnk ata hcho kiwanja utamnyanganya ...brooo zaidia lkn acha shoboo ungekut hayo mawazo unamuwazia. Dad ako au mdgo ako mbna nzuri ..pengine umewatelekeza ndugu zako. Afu uko unaenda kununulia watu viwanja. ....
 
NI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI

Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.

Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.

Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina.
Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.

Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka)

Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute.
Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale
Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.

Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa.
Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri.
Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea...na walikuwa wamepanga kuoana.

Nini kilitokea kati yao???

Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake.
Alifanikiwa kwenda na kurudi.
Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.

Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito.
Nikampa hongera zake..
Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi.
Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?

JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja
Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena.
Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.

Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye anafamilia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.

Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa
wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto
akiwa tumboni...wazazi wanajua hili
2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo
katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia
ya ajabu

MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa
wa hiyari na apewe ubini wa jina langu
kama baba alikubali hili kwa mshangao
mkubwa sana
(Haya[emoji116]sijamshirikisha)
2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito
3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya
mama na ya mtoto atakaye zaliwa
4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa
na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru
wake
5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.

Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.

Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi...sio nyumbani kwangu lakini.
Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.

Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.

Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;
Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.

Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi.
Muwe na wakati mwema wote.
KAMA hujaoa hebu omba Mungu akupe kibali umuoe huyu dada. Atakupenda na kukuheshimu maisha yako yote. Ni mke mwema huyu. Ninamsifu kwa kuamua kulea mimba yake. Na watoto wa hivi huwa wanaofanikiwa sana kimaisha. Baraka za Mungu ziambatane nawe daima.
 
Hili limechelewa mkuu siwezi kubadili gia angani, asante
 
Mhh wew utakuwa fisad had viwanja unaenda kununulia unborn child , na wa kwako umewanunulia tayari

Swal la kumpa faraja ili asipatwe na sonona ni jambo jema tu ..ila hawa ndugu zetu hawatabiriki nakuambia cku utakuja kusikia ana mtu mwingine kisirsiri ndio akili itakah sawa mnk ata hcho kiwanja utamnyanganya ...brooo zaidia lkn acha shoboo ungekut hayo mawazo unamuwazia. Dad ako au mdgo ako mbna nzuri ..pengine umewatelekeza ndugu zako. Afu uko unaenda kununulia watu viwanja. ....
Yuda Isikariot aliwahi kumwambia Aliyemmiminia Yesu mafuta kuwa kwanini anachezea mafuta ya thamani badala ya kuuza awape masikini?

Yesu alijibu kuwa masikini mnao siku zote.

Mkuu wazazi nawasaidia siku zote lakini mtoto aliyekataliwa sinao siku zote.
Ninafahanya kama sadaka na sio kwa lolote lile.

Tatu mimi sio tajiri wala fisadi bali ni mpambani wa hali zote na Mungu hubariki kazi za mikono yangu
 
Hili limechelewa mkuu siwezi kubadili gia angani, asante
I understand that you had clear crystal about your relationships. So sad of her to have missed a potential husband. But you have a great heart. Be blessed
 
I understand that you had clear crystal about your relationships. So sad of her to have missed a potential husband. But you have a great heart. Be blessed
[emoji120]
 
Yuda Isikariot aliwahi kumwambia Aliyemmiminia Yesu mafuta kuwa kwanini anachezea mafuta ya thamani badala ya kuuza awape masikini?

Yesu alijibu kuwa masikini mnao siku zote.

Mkuu wazazi nawasaidia siku zote lakini mtoto aliyekataliwa sinao siku zote.
Ninafahanya kama sadaka na sio kwa lolote lile.

Tatu mimi sio tajiri wala fisadi bali ni mpambani wa hali zote na Mungu hubariki kazi za mikono yangu
Na kupitia hili la huyo mtoto mkataliwa utabarikiwa uingiapo na utokapo. Kifupi soma Kumb 28:1-13 kama wewe ni a believing Christian. Namba mumpatie jina zuri la kuashiria mafanikio/bahati/FURAHA.
 
Bahati mbaya ni kuwa mtoto akishazaliwa na kukua Mama anarudi kwa mzazi mwenzie na kubeba mimba nyingine.
Hawa viumbe sio wa kuwaonea huruma kiasi hicho.
Kama mlishakuwa na uhusiano alishindwa Nini kukutafuta alivyopata stress huko ng'ambo!?
Si angerudisha majeshi kwako?
 
Back
Top Bottom