Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Huyo jamaa ipo siku ataibuka na kudai mtoto wake. Kama uliamua kumsaidia ungemsaidia tu lakini ubini atumie wa baba wa mtoto.
 
NI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI

Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.

Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.

Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina. Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.

Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka).

Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute. Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale. Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.

Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa. Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri. Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea na walikuwa wamepanga kuoana.

Nini kilitokea kati yao?

Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake. Alifanikiwa kwenda na kurudi. Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.

Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito. Nikampa hongera zake. Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi. Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?

JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja

Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena. Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.

Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye ana familia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.

Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto akiwa tumboni wazazi wanajua hili.

2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia ya ajabu.

MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa wa hiyari na apewe ubini wa jina langu kama baba alikubali hili kwa mshangao mkubwa sana (Haya[emoji116]sijamshirikisha)

2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito

3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya mama na ya mtoto atakaye zaliwa

4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru wake.

5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.

Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.

Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi sio nyumbani kwangu lakini. Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.

Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.

Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;

Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.

Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi. Muwe na wakati mwema wote.
(KATIKA HILI SITEGEMEI ANY RETURN)
Hongera kwa kupima kina cha bahari kwa kutumia mguu mkuu!

Hapo utalea mimba kisha utatunukiwa penzi na mimba nyingine itajaa,kisha utakua baba kamili[emoji23]
 
Hongera kwa kupima kina cha bahari kwa kutumia mguu mkuu!

Hapo utalea mimba kisha utatunukiwa penzi na mimba nyingine itajaa,kisha utakua baba kamili[emoji23]
Asante kwa uzoefu huo
 
Sitamuumiza mkuu, tangu nimweleze nina mahusiano yangu, ameyaheshimu kwa kiwango cha juu siku zote.
Hivyo anafahamu fika mipaka ya mahusiano yetu mimi naye.
Pia sitamfanya kuwa karibu nami kivile
Hapa unajidanganya. Moto wa mtu no kiza kinene. Naona unatengeneza bomu taratibu
 
Mkuu yeyote ambaye atathubutu kuhatarisha mahusiano yangu hulia sana
Kuwa tu makini. Maisha si kama unavyoweza kuyafikiria au kuyapanga wewe. Pia mfikirie huyo uliyenaye kwenye mahusiano sasa, don't be selfish. Kama umeamua kumsaidia mtoto basi usitake aitwe ubini wako. Unaweza kumwambia mama mtoto kwamba utasaidia pale itakapobidi. Ni mapema sana wewe kujicomit [emoji817] saivi hata mtoto hajazaliwa bado.
 
Il in reality ni ngumu sana kufanya hayo bila mama kutaka mahusiano na wewe
Wanawake wengi tunashindwa kutenganisha hilo.
Mwanaume akimpenda mtoto na akiwa wa karibu na mtoto automatically unajikuta upendo umejengeka, upendo ukiwepo wivu lazima uwepo.
Ni ngumu sana kutenganisha mapenzi hayo.
Wewe utakuwa na msimamo huo mwenzako ataanza kucatch feelings.

Mitego itaanza.

Kama ulichoandika ndo utakachofanya simama kwenye nafasi yako ukirudia kula tunda tu utaharibu kila kitu na future ya huyo mtoto.
Na ndo tatizo lilipo hapo. Ingekuwa anamuoa dada wa watu sawa, vinginevyo atamtesa kihisia mdada wa watu na mambo yakaja kuishia vibaya.
 
In tears , nipo emotional sana sijui kwanini
Anyways baba barikiwa , Mungu akutie Nguvu na uzao wako uwe wenye kuzidishiwa
Kwa imani yako sema amin
 
kwanza nimegundua vitu vitatu

1. ww una wivu wa kimapenzi

2. unawaza kwa kutumia moyo sio akili

3. huwa uwezo wa kuunganishaa matukio why ( jamaa wa kwanza kamakataa, wapil kapiga mimba kakimbiaa watatu fal* ndo wewe sasa)


kaka shirikushaa familia yako kama watakushauri
 
Nasapotiii hio comment kama ni dini nyingine sawa ila kwa sisi waislam kubadili ubini wa MTU ni strongly prohibited!!


Nashaurii msaidie ila mtoto abaki na ubini wake
We kama unamsapoti msapoti lakini maswala ya mtoto kutumia ubini wako sio vizuri
 
hujatueleza wewe una maisha gani mpaka sasa umeoa hujaoa una plan gani maisha yako nk.

unapopanga kumlea,kumsomesha na kumjengea wewe upande wako maisha yakoje? umeoa au hujaoa ? umejenga au hujajenga, au upande wako vp ?

au unajipa kichwa tu kumsaidia mtoto wa mwanaume mwenzio tu ?
 
hujatueleza wewe una maisha gani mpaka sasa umeoa hujaoa una plan gani maisha yako nk.

unapopanga kumlea,kumsomesha na kumjengea wewe upande wako maisha yakoje? umeoa au hujaoa ? umejenga au hujajenga, au upande wako vp ?

au unajipa kichwa tu kumsaidia mtoto wa mwanaume mwenzio tu ?
Umeuliza maswali muhimu sana lakini meishoni umemalizia vibaya.
Sio rahisi kwa mwenye njaa kukupa chakula.
Hilo linatosha
 
kwanza nimegundua vitu vitatu

1. ww una wivu wa kimapenzi

2. unawaza kwa kutumia moyo sio akili

3. huwa uwezo wa kuunganishaa matukio why ( jamaa wa kwanza kamakataa, wapil kapiga mimba kakimbiaa watatu fal* ndo wewe sasa)


kaka shirikushaa familia yako kama watakushauri
1. Moja ni kosa [emoji709] kubwa sana
 
Umeuliza maswali muhimu sana lakini meishoni umemalizia vibaya.
Sio rahisi kwa mwenye njaa kukupa chakula.
Hilo linatosha

kwa hio unamsaidia kulea ujauzito k'rafiki au kwa sababu unamnyandua mtoto wa kike ?

kwa lugha rahisi umejipatia mteremko ?
 
kwa hio unamsaidia kulea ujauzito k'rafiki au kwa sababu unamnyandua mtoto wa kike ?

kwa lugha rahisi umejipatia mteremko ?
Ninasikitika sana mmejaa mawazo ya ngono.
Kwa taarifa yako wapo wengi wanatamani niwabandue lakini hata muda sina, why nitamani mteremko tena kwa mjamzito?
 
Ninasikitika sana mmejaa mawazo ya ngono.
Kwa taarifa yako wapo wengi wanatamani niwabandue lakini hata muda sina, why nitamani mteremko tena kwa mjamzito?

kama nilivotangulia kusema sijui maisha yako kwa sasa na kama ungeeleza hapa ningekupa ushauri kulingana na upeo wangu ila kwa sasa ngoja nikubaliane na maamuzi yako
 
Back
Top Bottom