Maana halisi ya kutafuta mpenzi, ni kutafuta mtu aje akusaidie kutumia fedha zako ulizozitafuta kwa jasho

Maana halisi ya kutafuta mpenzi, ni kutafuta mtu aje akusaidie kutumia fedha zako ulizozitafuta kwa jasho

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Maana halisi ya kutafuta mpenzi, ni kutafuta mtu aje akusaidie kutumia fedha zako ulizozitafuta kwa jasho. Kama wewe unaponda kokoto tani 20, unatafuta mtu aje akusaidie kutumia fedha zako kutokana na mapato uliyoyapata kwenye kazi ngumu ya kuponda kokoto. Kwa hiyo kama mpenzi wako anayumbisha uchumi wako hutakiwi kulalamika, kwa sababu ulimtafuta mwenyewe aje atumie fedha zako.

Kwa wale wenye wapenzi wawili, kumi, ishirini, sita n.k jua umewaalika mwenyewe waje watumie mapato uliyoyapata; kwa hiyo usilalamike. Ukiwa peke yako kilo ya sukari inamaliza wiki 2 ,baada ya kumualika mwenzako kilo ya sukari inakaa siku 3. Ulipokuwa peke yako ulikuwa smati, baada ya kumualika mwenzako umeanza kuchakaa; ni sawa na kubeba gunia tano za mahindi kwa kichwa.

Ndio maana wanaume wengi siku hizi wanaenda bar na kuagiza nyama choma, kuku, mbuzi, kitimoto n.k huku nyumbani amewaachia matembele, wapambane na hali zao.
 
Back
Top Bottom