ipyax
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 4,247
- 6,578
Basi za mchina hazina comfort kabisa , suspension zao ziko jittery mwanzo mwisho mpaka huwa nashindwa kusoma vitabu nikiwa safarini.Hakuna luxury bus inayobeba abiria zaidi ya 30. Hizo ni busses za nauli ya juu tu kwa vile zina choo na WiFi. Luxury ni pale unapokuwa na maximum comfort wakati wa safari. Mabasi yetu hata hiyo Wi-Fi wameandika tu haipo. Kwenye TV huwezi kuchagua unachotaka kuangalia.... Utaoneshwa mkojani au muvi zilizotafsiriwa njia nzima. Utapewa biscuit na soda moja au maji tena hata soda yenyewe hauchagui unapewa yeyote tu.
Njiani mtaongia hotel moja na kina CHAKITO au Ms. SERENGETI. Wahudumu wa ndani wataongea na nyie kwa kebehi kama wamewapa lift tu.
Tofauti yenu na aliyepanda KING MUSUKUMA ni kuwa nyie hamtachimba dawa njiani.