Maana halisi ya "Luxury Bus" ni nini?

Maana halisi ya "Luxury Bus" ni nini?

Hili halizingatiwi. Juzi kati baada ya kukosa magari yote sijui yalikuwa yamekodishwa kwenda wapi nimepigwa vibaya kuambiwa ni luxury nauli 33,000 Arusha Dar.
Kuingia ndani nusu nizimie basi chafu ni kama halijawahi kufanyiwa usafi, halina service yoyote..unaambiwa linaondoka saa 12 lkn linaondoka masaa matano baadae.
Nauli kila mtu kalipa tofauti..
Tupo tuliopigwa 33, wengine 25, 22 hadi.17.
Kundoka Arusha saa 2 asb kufika dar saa 5 usiku.

Osaka Express pambav zenu.
Osaka wakwe zangu hawa washauwawa siku nyingi kiuchumi
Mtoto wa mzee kaomba poo juzi hapo..
Alichonifanya miaka 18 iliyopita mungu shahidi
Nimemsamehe anyway.
 
Wild Boy kwa hiyo mzee Kilimanjaro vs Tahmeed ngap ngap kulingana na wadau na picha huku?

Binafsi nimeikubali sana Tahmeed asee hawa jamaa wako vizuri
Kwa muonekano wa picha za gari tahmeed anaongoza, ila kwakuwa sijalipanda kwenye swala zima la huduma bado nasimama na Kilimanjaro express kuanzia booking, huduma ndani ya gari, hotelini mpaka mwisho wa safari huduma zimepangiliwa vyema kabisa
 
Alafu kampuni inaangalia faida pia, sio ilete kitu luxurious alafu wateja wawe robo ya gari sababu ya bei ghali. Na hakuna vile utashusha bei, utarudisha vipi hela ulioinunulia hilo bus? 😂
Hapo umekata mzizi wa fitna
Mazingira ya biashara hapa TZ ndio yanapelekea uwepo wa aina za magari hapa nchini na sio kwamba matajiri hawana uwezo wa kununua hayo magari luxury ya nchi za nje. Biashara yataka akili ukikurupuka na masifasifa utaangukia pua, wengi wameshaumia kwenye hii biashara
 
Kweli mkuu, watu wana hela ndefu lakini sio za kumwaga ovyo pasipo na faida. Ingekuwa nchi zilizoendelea, hapo sawa kuwekeza mitambo kama hiyo ya barabarani, lakini nchi nyingi za Africa, kuanzia wateja hadi barabara zenyewe balaa tupu, alafu dingi akanunue mtambo super luxurious, yaani ndani kama uko kwenye ndege vile, urongo. Hata ka hela ipo lakini akili pia hutumika kiasi kwa kuekeza sehemu flani!
 
Kabisa mkuu, 'huwezi kuwa tajiri kama hauna akili'
 
Tanzania kuna basi zina choo ndani zina free wifi ,2 in 1 seats + VIP seats ,ina tablet kila seat , ndani mnapewa vinywaj na baadhi ya vitu vya kutafuna na zimepewa daraja la luxury
Kupewa daraja ni jambo jingine na uhalisia wa luxury bus inatakiwa kuwaje ni jambo jingine, Tanzania hata daladala zinaweza kupewa hilo daraja ni pesa yako tu ukiwapa mamlaka husika unapata, na ndicho kimefanyika kwa mabasi mengi yamebandikwa madaraja kwa viwango yasivyostahili
 
Kwa muonekano wa picha za gari tahmeed anaongoza, ila kwakuwa sijalipanda kwenye swala zima la huduma bado nasimama na Kilimanjaro express kuanzia booking, huduma ndani ya gari, hotelini mpaka mwisho wa safari huduma zimepangiliwa vyema kabisa
Kwa hotelini mm nakataa... chips kavu 7k kweli!!🤔😬🙄

Tahmeed 3 Kilimanjaro express 1
 
Kula bus ubungo siku moja sijui luxure Dar lux au Rungwe
, Msamvu limetuacha na dereva tulimpa taarifa nampeleka dogo chooni. Kaondoka
Tukaanza kukimbizana na boda tukakuta yupo mbele kule kabla hajaanza kuitafuta mikumi.
Namuuliza hana hata majibu, ye anawai tu
 
Kwa hotelini mm nakataa... chips kavu 7k kweli!!🤔😬🙄

Tahmeed 3 Kilimanjaro express 1
Hio 7k ukicheki vizuri ni pamoja na miundo mbinu ilyopo pale, na hoteli zote zenye mandhari kama ile huwezi kuta chakula cha bei ya chini.
Na ninavyofahamu ni either chips kuku au chips nyama choma hakunaga kavu, japo sina uhakika sana maana mimi natumiaga bufee (mlo kamili)
 
Siku moja zamani Nimekatishwa tkt Abood ya Tunduma pale Mbeya E bana wale wasengerema, basi limefika kmmk kama vile nikasukumwa tu ndani.
Nimekaa kwenye kiroba cha mchele toka Mbeya mpaka Dar.
Sina hamu,alafu Wale wasenge kufika moro wakapaki bus pale gereji yao wanadai inapigwa service 🤸‍♂️😥masaa ma2 ndio tukaondoka kwenda Dar.
Sipandi tena mabus ya bongo
 
Hakuna luxury bus inayobeba abiria zaidi ya 30. Hizo ni busses za nauli ya juu tu kwa vile zina choo na WiFi. Luxury ni pale unapokuwa na maximum comfort wakati wa safari. Mabasi yetu hata hiyo Wi-Fi wameandika tu haipo. Kwenye TV huwezi kuchagua unachotaka kuangalia.... Utaoneshwa mkojani au muvi zilizotafsiriwa njia nzima. Utapewa biscuit na soda moja au maji tena hata soda yenyewe hauchagui unapewa yeyote tu.
Njiani mtaongia hotel moja na kina CHAKITO au Ms. SERENGETI. Wahudumu wa ndani wataongea na nyie kwa kebehi kama wamewapa lift tu.
Tofauti yenu na aliyepanda KING MUSUKUMA ni kuwa nyie hamtachimba dawa njiani.
 
Hahahahaaaa jiwe la gizani kwa wanaojidai wamepanda luxury Tanzania, sijui walishapanda luxury bus ughaibuni!!!
 
Hahahahaaaa jiwe la gizani kwa wanaojidai wamepanda luxury Tanzania, sijui walishapanda luxury bus ughaibuni!!
Utapeli tu mkuu. We toka lini luxury bus ikawa na siti 60 tena Yutong.?
Gari inatembea km 1000 kwa speed kubwa unashikilia roho muda wote. Kuna luxury gani hapo.
 
Una moyo kweli afu abiria wapole sana
Siku moja zamani Nimekatishwa tkt Abood ya Tunduma pale Mbeya E bana wale wasengerema, basi limefika kmmk kama vile nikasukumwa tu ndani.
Nimekaa kwenye kiroba cha mchele toka Mbeya mpaka Dar.
Sina hamu,alafu Wale wasenge kufika moro wakapaki bus pale gereji yao wanadai inapigwa service 🤸‍♂️😥masaa ma2 ndio tukaondoka kwenda Dar.
Sipandi tena mabus ya bongo
 
Osaka wakwe zangu hawa washauwawa siku nyingi kiuchumi
Mtoto wa mzee kaomba poo juzi hapo..
Alichonifanya miaka 18 iliyopita mungu shahidi
Nimemsamehe anyway.
Biashara ya mabasi kufilisika ni sekunde tu......mwanae anaitwa hashim sijui nimesahau jina
 
Back
Top Bottom