Maana halisi ya "Luxury Bus" ni nini?

Maana halisi ya "Luxury Bus" ni nini?

Katika mabasi nilyopanda naweza kusema KILIMANJARO Express ndio wana hizo huduma za luxury
Ac mwanzo-mwisho.
Comfortable seat.
Toilet safi kabisa.
Mda wa kula hotelini ni nusu saa (30 min), kampuni nyingine ni dkka kumi tu!
Mwendo (uendeshaji) murua kabisa.
Konda-mwanamke mzuri mwenye kutoa huduma ya viwango wakati wote (miithili ya air hostes), kampuni nyingine makonda ni wahuni tu kazi yao pekee ni kuokota abiria wa njiani shenzi kabisa.
Runinga kama kawaida ila sio muvi ya kina mkojani, ni media zilizo pangiliwa vizuri
Biskuti+ soda+maji+pipi.
Booking office very comforting huduma zote ukiwa unasubiri gari ifike usepe

Kwakweli nikitumia pesa yangu kwa hawa jamaa huwa sijutii kabisa ila kampuni nyingine tutapambana mpaka nihakikishe natoa pesa ya mmiliki wa gari pekee hakuna cha ya mpiga debe wala nini
Still hiyo sio luxury.

Ni semi luxury.
 
Ni tatizo kubwa sana, konda anashindwa kujua tabia za mteja wa luxury na wa ordinary?
Mara 100 uweke hata miziki mbalimbali. Unatengeneza playlist ndefu yenye kila aina ya nyimbo.

Zile muvies ni kero kubwa sana.
 
View attachment 1780996
1. Je ni hizo huduma hapo ☝️ au ni upya wa basi?
2. Basi la zamani lenye vigezo hivyo huu au basi lolote jipya?

Ikitokea huduma tajwa hapo ikakosekana kwenye gari na kiwango cha nauli umelipia luxury abiria anasaidiwaje au achukue hatua gani?.

SUMATRA wanatumia kigezo gani kugawa haya madaraja?

Wajuvi tusaidiane hapo☝️
Hii ni Luxury bus gani hapa
 
Back
Top Bottom