Mamlaka zizingua sana katika ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili.
Lugha ikiwa sehemu ya utamaduni, inatokana na jamii, ni mali ya jamiii na inanyumbulika kwa kufuata matakwa na mabadiliko ya jamii.
Siyo sahihi kwa wataalamu wa lugha ya kiswahili kufanya maamuzi kuhusu unyumbukaji wa lugha ya Kiswahili. Wanachopaswa kufanywa ni kurasimisha matakwa ya jamii na siyo wao kuwapa jamii maana. Iwapo wataendelea na hii desturi ya kutaka kumiliki lugha ya Kiswahili, watasababisha tafsiri yao ya lugha iliyomo mkwenye kamusi kutofoautiana lugha halisi ya kiswahili. Mfano wananchi wanaita Kompyuta lakini wao wamejitungia tafsiri yao hali amabyo imesababisha wananchi wasiizingatie kamusi.
Aidha wanapaswa kuelewa kuwa lugha ni flexible inabadilika kutokana na wakati na kutokana na eneo. Mfano kuna kiswahili cha Zanzibar, Pwani, Bara, Mombasa, Nairobi, East DRC, Burundi n.k. Wote hawa wapo sahihi kwani wanaweza kuelewana katika model hizo za kiswahili na wao ndio wameamua iwe hivyo. hata Kamusi ya Kiswahili isemeje haiwezi kubadili model zao za Kiswahili.
Kifaransa cha Paris ni Tofauti na cha Ubelgiji, Canada, Geneva, Kinshasha, Bujumbura n.k. English ya London ni tofauti na Birmingham, Liverpool, Marekani, scotland, Ireland, Kenya, South Africa, Zimbabwe, USA, Malawi n.k. Pamoja na tofauti hizo wote wanaonea kiingereza sahihi na kamusi zao hazilazimishi wote waongee kingereza cha London au French ya Paris.
Wanapaswa kubadilika ili kuitendea haki jamii