Maana ya baadhi ya maneno ya kiingereza

Maana ya baadhi ya maneno ya kiingereza

Wana-complicate maneno kiasi ambacho raia hawatakaa wayatumie kwa sababu ni magumu halafu hayaendani na vitu. Kwa nini hawashirikishi umma? Kwenye hii list neno walilolipatia ni kadikazi (business card). Ukiniambia mimi nitoe maoni yangu:
1. Charger - kichajio
2. Appertizers - kitiahamu
3. Simcard - kadisimu
4. Memory card - Kadikumbu
5. Business card - kadikazi (nalikubali)
6. Microwave - Jikomiale
7. Cocktail - tafrijatanzu
8. Lift - lifti
9. Toothpick - kichokoameno
10. Scanner - Kidurufu
Wasingepata tabu kubwa kutunga maneno na yangekubalika haraka.
 
Eti TISHU kwa KISWAHILI fasaha inaitwa "shasi"
View attachment 2971871
shasi ya kufutia mashonde
Kwaiyo utaagiza kibanzi yai😃
mwandazi naomba nipatie vibanzi na sharubati karakara usisahau kuniwekea na kimbaka
(waitress naomba unipatie chips juisi ya passion usisahau kuniwekea na toothpick)

NB tukiwaendekeza bakita tutajikuta ni wageni nchini kwetu 😁😁
 
wadada wa jf wana usangati mwingi sana
images-1372.jpeg
😃
 
Ukawii kuhisiwa wee ni mhamiaji haramu
shasi ya kufutia mashonde
mwandazi naomba nipatie vibanzi na sharubati karakara usisahau kuniwekea na kimbaka
(waitress naomba unipatie chips juisi ya passion usisahau kuniwekea na toothpick)

NB tukiwaendekeza bakita tutajikuta ni wageni nchini kwetu 😁😁
 
Hii misamiati yenu huwa mnaibuni kutoka wapi aisee

1. Charger – kimemeshi
2. Appetizers –vihamuzi
3. Simcard – kadiwia/mkamimo
4. Memory card –kadi sakima
5. Business card – kadikazi
6. Microwave –tanuri miale
7. Cocktail party – tafrija mchapalo
8. Lift – kambarau
9. Toothpick – kimbaka
10. Scanner –mdaki

Ongezea misamiati mingine yenye utata.....
The Stress Challengerr = Maghayo

Cc. adriz
 
Kuna uwezekano pale Bakita kumejaa wapumbavu si kila neno liwe na kiswahili chake haswa vitu vipya ambavyo havijawahi kuwepo duniani before.. wagunduzi lazima wapate heshima zao na sio dharau. Mwana fizikia ametumia ujuzi wake wote akalipa jina gunduzi lake vijizee vya Bakita vinakuja na uarabu wao vinageuza geuza na kuleta majina yao ambayo hata mitaani hakuna eti Kambarau ndio Elevator.. Na sisi tunataka jina la Allah kwa Kiswahili
 
Hii misamiati yenu huwa mnaibuni kutoka wapi aisee

1. Charger – kimemeshi
2. Appetizers –vihamuzi
3. Simcard – kadiwia/mkamimo
4. Memory card –kadi sakima
5. Business card – kadikazi
6. Microwave –tanuri miale
7. Cocktail party – tafrija mchapalo
8. Lift – kambarau
9. Toothpick – kimbaka
10. Scanner –mdaki

Ongezea misamiati mingine yenye utata.....
Mamlaka zizingua sana katika ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili.
Lugha ikiwa sehemu ya utamaduni, inatokana na jamii, ni mali ya jamiii na inanyumbulika kwa kufuata matakwa na mabadiliko ya jamii.

Siyo sahihi kwa wataalamu wa lugha ya kiswahili kufanya maamuzi kuhusu unyumbukaji wa lugha ya Kiswahili. Wanachopaswa kufanywa ni kurasimisha matakwa ya jamii na siyo wao kuwapa jamii maana. Iwapo wataendelea na hii desturi ya kutaka kumiliki lugha ya Kiswahili, watasababisha tafsiri yao ya lugha iliyomo mkwenye kamusi kutofoautiana lugha halisi ya kiswahili. Mfano wananchi wanaita Kompyuta lakini wao wamejitungia tafsiri yao hali amabyo imesababisha wananchi wasiizingatie kamusi.

Aidha wanapaswa kuelewa kuwa lugha ni flexible inabadilika kutokana na wakati na kutokana na eneo. Mfano kuna kiswahili cha Zanzibar, Pwani, Bara, Mombasa, Nairobi, East DRC, Burundi n.k. Wote hawa wapo sahihi kwani wanaweza kuelewana katika model hizo za kiswahili na wao ndio wameamua iwe hivyo. hata Kamusi ya Kiswahili isemeje haiwezi kubadili model zao za Kiswahili.

Kifaransa cha Paris ni Tofauti na cha Ubelgiji, Canada, Geneva, Kinshasha, Bujumbura n.k. English ya London ni tofauti na Birmingham, Liverpool, Marekani, scotland, Ireland, Kenya, South Africa, Zimbabwe, USA, Malawi n.k. Pamoja na tofauti hizo wote wanaonea kiingereza sahihi na kamusi zao hazilazimishi wote waongee kingereza cha London au French ya Paris.

Wanapaswa kubadilika ili kuitendea haki jamii
 
Back
Top Bottom