Maana ya Jina la Rais wa Tanzania, Samia Suluhu

Maana ya Jina la Rais wa Tanzania, Samia Suluhu

Jina la Rais wetu Bi Samia Suluhu limeundwa kutokana na maneno ya Kiarabu.

1) Samia: Maana yake ni msikivu. Neno hili hupatikana hata katika salat za kila siku kwa Waislaam, pale Muislam anaposali, akinyanyuka kwenye rukuu husema "Samia Llahu liman Hamida". maana yake, Ni "Allah humsikia mwenye kumhimidi".

2) Suluhu: Ingawa neno hili linatokana na neno la Kiarabu "Sulh" lakini Kiswahili tunalitumia sana, suluhu kwa maana ya kukubaliana yaishe kwa amani na si kwa ugomvi.

Mfanya Suluhu mara nyingi huwa ni anaeheshimika na pande zote mbili, msikivu, mwenye hekima na asiependelea.

Tutegemee mema sana kutoka Kwa bi Samia Suluhu.

Ma Shaa Allah.

Ndugu yetu kaongezea maana ya jina la tatu: Maana ya Jina la Rais wa Tanzania, Samia Suluhu.
Madamoiselle, Samia kakuibua.
Karibu tena.
 
Hujui ndio maaana unasema hivyo bas kaaa na hizo maaaana zako
Kweli kabisa sijui, tufahamishe. Mimi nekuwekea uzi wa wazee wa Madrassa hapo wanavyojenga taifa kwa ubunifu wao, wewe je?
 
Kweli kabisa sijui, tufahamishe. Mimi nekuwekea uzi wa wazee wa Madrassa hapo wanavyojenga taifa kwa ubunifu wao, wewe je?
Ok za siku ming FAIZA KARIBU SANA HATUJAKUONA KITAMBO TUNASHUKURU KWA MAAANA
 
Sasa wewe na Faidha nani mdini hapi?

Kaelelzea maana tu ya Jina tayari Povu limejaa kifuani
Wewe Ustadhati Faiza na Mzee Mohamed Said hapa JF forum nawapongeza sana kwa Propaganda za kidini na kutaka kuligawa Taifa

Naona mmetoka mafichoni sasa mnaanza kuhubiri udini kama kawaida yenu

Ahaaa nilijua tu sasa utakuja kwa kasi baada ya miaka mitano kujificha chini ya utawala wa JPM, Sasa umekuja kueneza Propaganda na itikadi kali za kidini kama kawaida yako

Huu ni mwanzo tu Mama Faiza naona mvua yenyewe tunasubiri

Ni wakati mtaanza tena kushinikiza mahakama ya kadhi kama wakati wa JK

Ni wakati Mama asipokuwa makini Nyaraka kali na za onyo zitaanza kutembezwa toka CCT, Tec na Vatican

Ndio maana JK aliamua kuziba masikio na kusafiri tu kila siku maana nyumbani ilikuwa Wengine Nyaraka Wengine Tunataka Mahakama ya kadhi

Tutashuhudia mengi
 
Mara kadhaa jina limesadifu maisha ya mtu na Kama huamin watafute wakina Shida, tatizo na wengine wenye majina hayo utajifunza kitu au jisomee Haya majina tusiwape newborn (watoto)
I strongly support your comment. Katika kabila la Wahaya kuna msemo unasema "Eibala lita Nyinalyo"! Kwa tafsiri ya kiswahili isiyo rasmi ni "Jina linaua mwenye nalo"! Yaaani kuna uwezekano jina lako likadetermine or predict your future!

Hivyo sio sahihi sana kumuita mtoto wako jina kama vile Shida, Taabu, Maskini, Matatizo na mengi kama hayo!
 
Huu mzimu umeibukia wapi? Kwa Jiwe mzimu huu ulipotea kabisa!
 
Kwahiyo suluhisho la umaskini na ufukara wa Watanzania ni kuwapa watoto majina ya kiutajiri?

Mimi siafiki kuwa jina la mtu ndio huleta matokeo ya maisha yake.

Kama Samia atawatendea mema basi ni uamuzi wake tu.

Je, wakevi waliongezeka kipindi cha John Pombe?
 
Welcome back FaizaFoxy Mama Samia Suluhu kama lilivyo jina lake ni Zawadi kwa Watanzania baada ya kipindi kigumu cha mtangulizi wake (Mungu ampumzishe anapostahili).
Lets hope for the Better.
 
Jina la Rais wetu Bi Samia Suluhu limeundwa kutokana na maneno ya Kiarabu.

1) Samia: Maana yake ni msikivu. Neno hili hupatikana hata katika salat za kila siku kwa Waislaam, pale Muislam anaposali, akinyanyuka kwenye rukuu husema "Samia Llahu liman Hamida". maana yake, Ni "Allah humsikia mwenye kumhimidi".

2) Suluhu: Ingawa neno hili linatokana na neno la Kiarabu "Sulh" lakini Kiswahili tunalitumia sana, suluhu kwa maana ya kukubaliana yaishe kwa amani na si kwa ugomvi.

Mfanya Suluhu mara nyingi huwa ni anaeheshimika na pande zote mbili, msikivu, mwenye hekima na asiependelea.

Tutegemee mema sana kutoka Kwa bi Samia Suluhu.

Ma Shaa Allah.

Ndugu yetu kaongezea maana ya jina la tatu: Maana ya Jina la Rais wa Tanzania, Samia Suluhu.
mama uliadimika sana. karib mjengoni
 
Back
Top Bottom