Maana ya "Kwenu" inatofautiana, si kila mtu kwao yao inalingana, wewe kwenu ni wapi?

Maana ya "Kwenu" inatofautiana, si kila mtu kwao yao inalingana, wewe kwenu ni wapi?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Naona hili neno huwa linatumika ndivyo sivyo kwa kumaanisha ni mtu kurudi kwa ndugu zake vijijini, uhalisia upo tofauti.

Kwenu ni kule ambako una ukaribu nako, ni sehemu mnayoshirikiana nje ya misiba na sherehe.

Kuna wengine kwao yao inaishia kwa wazazi wao, kaka zao, dada zao na wadogo zao hawana ukaribu

Kuna wengine kwao yao ni familia nzima kiujumla walizotokea, hapa ni wazazi wao, kaka zao, dada zao na wadogo zao.

Kuna wengine kwao yao ni familia walizonazo hasa watoto na wenza wao, mtu anaweza akawa hajarudi kwa wazazi ama wenzake kwa miaka.

Kuna wengine kwao yao ni familia walizonazo na familia walizotokea.

Wengine kwao yao imefikia level za ndugu, hawa ni wachache zaidi, mfano kila mwaka hurudi vijijini kwao ili ndugu wote waweze kukutana,
 
Kwenu/kwako, ni mahali popote pale ambapo umeishi kiasi kwamba umeweza kujenga mahusiano na watu tofauti tofauti wa eneo hilo na ukaweza kuchukuliwa kama sehemu ya jamii hiyo....

Vitu ulivyojifunza na mapito uliyopitia vinaweza kukusaidia kwenye maisha yako mbeleni hata kama ukihama hapo.

Mfano shule ulizosoma, makanisa uliyosali, ni kwenu/kwako.
 
Marafiki wengi tuliosoma nao mawasiliano yanakata tulipomaliza vyuo / shule japo tukikutana huwa tunachangamkiana ila baada ya hapo tunapotezana tena, kwa sasa tupo na marafiki ambao tunashinda nao, marafiki wanakuja na kupotea ila kwenu hapabadiliki
 
Back
Top Bottom