Maana ya Mwanamke Bikra, Kuwa na Mahusiano/Kuoa Mwanamke Bikra

Siujui naomba muongozo

Ukipata mwanaume mwingine, mwambie unaomba uvunje agano la ubikra ulilofanya na mwanaume(ex wako marehemu) hata kama sio marehemu, kisha baada ya kutangua agano lile mnaweza anza mahusiano ya ndoa.
 
sasa shida kupata huyo bikira ni ngumu labla huyo mke atoke kwa mungu na usijitafutie
 
Huu ni ukweli mtupu na unatakiwa kuungwa mkono na kila mwenye akili,vijana tunakosea sana linapokuja suala la kuoa.Unamkuta mtu humjui hata kwao akikwambia jina lake tu inatosha na unataka ule tu,aidha uondoke au ndio hivyo tena unaoa.Mkianza kupishana unaanza kumlaumu Mungu,kama tu kwenye mambo ya kwaida tunatumia muda kuulizia kwanini tuwe na papara kwenye kuoa na kuolewa?Tumwombe sana Mungu atusamehe na kuturehemu kwa tulioa,na wale ambao bado jifunzeni kwenye hili.Kusema ukweli mimi nimeoa,lakini kuukubali ukweli kuwa kuna mtu alimtoa bikra mke wangu inakera na kudhalilisha sana,yaani hata ukitaka kuona hilo mwulize tu mwanaume aliyemtoa bikra yupo wapi uone hasira zake.
 
kuna siku hapa nilisema....''mwanamke/msichana asie na BIKRA hapasi kutolewa mahari" , ni aibu iliyojificha katika tamaa zetu wanadamu.....but.....hao wenye bikra wako wapi.........????....
 
Huoni umuhimu wa bikra zama hizi wakati huo huo unaona ndoa nyingi zikipumulia mashine kisa na mkasa wengi wamechukua wake na waume wasio wao?

Hapa ndio utajua vijana wa siku hizi uwezo wao wa kufikiri upo chini, wanazidiwa hata na wanyama wa porini
@Jokajeusi hakuna kuimbe cha kuielew hii kitu bikra haiimarishi ndoa broo ni mtu mwenyew

utamtoa bikra akion huelewki anagawa kwingine
utamtoa bikla lkn usipo muelew unapiga chini

kuna matendo kabla ya tend na pia baada ya tendo kuna matendo


nimekuuliza je kwa walio tolewa bikla kwa misukosuko kam vile kubakwa huyu nae tunamuwek wapi!?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Sasa Kama aliyenibikiri alikufwa nifanyeje?
 
Ukipata mwanaume mwingine, mwambie unaomba uvunje agano la ubikra ulilofanya na mwanaume(ex wako marehemu) hata kama sio marehemu, kisha baada ya kutangua agano lile mnaweza anza mahusiano ya ndoa.

Sawa asante
 
Joka mimi huwa nakuelewa sana, sema tu kuna viumbe humu wamegeuza mioyo yao kuwa migumu kama jiwe.

Bikra ni kila kitu katika ulimwengu wa Roho.
 
Joka kama joka hujazingatia ile note
 
Wapi uliona kutongoza ikawa ni uzinzi?

Hakuna sheria inayomzuia mwanaume kutongoza, lakini ipo sheria inayomzuia asizini.

Mwanamke ndio hujitunza kwa ajili ya mwanaume na sio mwanaume ajitunze kwa ajili ya mwanamke
Safi kabisa. Tuje hapa.

Mithali 6:32 "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake." (Obviously anayeongelewa hapo ni mwanaume)

Andiko hilo hapo lakini cha ajabu wanaume wengi wanazini je kwanini wanazini? Na je unakubaliana na maandiko kuwa mwanaume anayezini na mwanamke hana akili kabisa?

Kwa maana hiyo basi ni kwamba mwanaume naye anatakiwa asizini! Which brings us back to my point kuwa kama ndiyo hivyo basi hata mwanaume anatakiwa ajitunze hadi ndoa!
 
Kwa kifupi tu ni kwamba virginity means purity. Kitu chochote ambacho hakijawahi kuguswa au kutumika na chochote basi hicho ni bikira hivyo kwa muktadha huu hapa mtu bikira ni mtu yeyote yule ambaye hajawahi kushiriki tendo la ndoa.

Mnachokosea ni kudhani kuwa mwanamke tu ndiyo bikira eti kwa sababu yeye amewekewa alama ya kile kimlango ambacho hufunguka anapokutana na mwanaume kwa mara ya kwanza na wengi kutokwa na damu! Bikira ni zaidi ya hicho kimlango na zile damu!

Hicho kimlango kinaweza kutolewa kwa sababu lukuki ambazo zinajulikana mfano mwanamke kuendesha baiskeli kupita kiasi nk! Je unataka kuniambia hicho kimlango kikitoka ndiyo tayari mwanamke anakuwa ameshapoteza bikira yake hata kama hajawahi kukutana na mwanaume?

Kwa mantiki hiyo unataka kuniambia mwanamke wa aina hiyo akikutana na mwanaume kwa mara ya kwanza asipoona kile kimlango au damu zisipomtoka basi yule mwanamke siyo bikira? Halafu kuhusu takwimu hauwezi kukurupuka tu kuja kusema umejitolea mfano wa wewe na ukoo wako wakati hii dunia ina watu zaidi ya billion 7!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…