Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,237
Zawadi Lupelo
Wanajamvi salamu kwanza!
Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz kwa makini sana. Kitu kilichonitatiza na kuja kunishughulisha hapa jamvini ni neno hallelujah na namna lilivyotumika ni maoni yangu kwamba limetumika kimakosa katika wimbo huo ambao ni wa mapenzi hasa ukizingatia maana ya msingi ya neno ambapo huwa linatumika kwenye ibada katika kumsifu Mungu ni neno linalomaanisha "Mungu apewe sifa".
Ni neno ambalo linaenda sambamba na maneno Bwana asifiwe, tumsifu Yesu Kristo na kadhalika huko makanisani kufikia hatua ya kulitumia hili neno kwenye wimbo wa mapenzi katika muktadha wa Diamond Platnumz ni kufeli kwake katika uteuzi wa maneno.
Haiwezekani umezungukwa na mademu wapo nusu uchi unaimba Hallelujah huku ni kuitweza imani na utukufu wa Mungu.
Ni matumaini yangu wakati mwingine atakuwa makini kwenye kuchagua maneno ya kutumia ili kuhakikisha haleti mkanganyiko wowote.
I rest my case.
Zawadi Lupelo.