Maandamano IFM

Maandamano IFM

Wanafunzi wenzao walio kuwa wamepanga huko kigamboni wamevamiwa na majambazi na kujeruhiwa huku wasichana wakibakwa, inasikitisha sana, sasa waliamua kwenda wizara ya mambo ya ndani wakidai ulinzi na malalamiko ya kukosa ulinzi wa polisi eneo la tukio!

Hii ni
Kwa mujibu wa mwanafunzi anayesoma chuoni hapo
 
Hapa wanafunzi wa IFM wakiandamana kupinga wenzao wawili kuvamiwa na majambazi halafu wakalawitiwa. Wamekwenda ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi kupeleka malalamiko yao kuwa waliwahi kuripoti kukosa usalama katika mabweni ao ila jeshi hilo halijachukua hatua zozote.

Wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha IFM wakiwa ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi nchini jijini Dar es salaam leo mchana.

Kiongozi wa wananfuzi iFM akimweleza kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam Suleiman Kova juu ya kadhia iliyowapata wenzao kwa kuvamiwa na majambazi wakiwa wamelala.

Baada ya kuzungumza nao kamanda Kova aliamua kuandamana nao mpaka zilipo Hostel na kituo cha polisi walichodai waliripoti matatizo yao lakini hawakusikilizwa. Kova aliwaahidi watapanda kivuko bila malipo, tatizo wanafunzi walijaa kuliko uwezo wa kivuko. Hapa akijadiliana na askari wenzie namna ya kuwapunguza wanafunzi hao....


Wanafunzi hao walivamia makao makuu ya jeshi hilo majira ya saa nne na nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.

 

Wanafunzi wa Chuo cha IFM wakiwa nje ya Ofisi ya Wizara ya mambo ya nje ambapo ndipo wamefikia kwa Maandamano yao




****

Katika hali isiyo ya kawaida Wanafunzi wa Chuo cha IFM wameandamana mpaka Ofisi ya Wizara ya mambo ya Ndani muda huu, Chanzo cha maandamano Bado hakija fahamika, Mpaka sasa Kamanda Kova ameshafika eneo la Tukio kuongea na wanafunzi hao.


Habari Kamili Tutawaletea Baadae endelea kufuatilia hapa hapa.. Tone Multimedia Live Group Tupo eneo la Tukio.



Picha na Blogs za Mikoa

Kule Kigamboni wanafunzi wengi wa IFM wamepanga kwenye nyumba za uswahili au hosteli bubu ambazo usalama ni wamashaka kwani kuna vibaka toka temmeke, tandika au hata hapo kigamboni katika makundi ya vibaka 10 hadi 20 na kuwapola wanafunzi vitu vya kwahiyo hali kigamboni hali siyo shwari kabisa huo ndio mkasa wa huo mkusanyanyiko kumpa kutaarifa Kova kwamba law enforcers wako wapi hali siyo shwari ktk Tanganyika hii Mbunge Ndugulile uko wapi jimbo lako sio shwari kwani sio hii tu hata ukiharibikiwa na gari kigamboni basi uwe tayari kwa lolote la kiharifu.
 
Polisi wafanye kazi yao..sio lazima mpaka majanga yatokee.
hii sasa kali mpk vijana wa kiume wanabakwa,watu wazima!
 
..., poleni sana wanafunzi kwa kufanyiwa kitendo cha kinyama! Je mpaka sasa wamebakwa wanafunzi wangapi?
 
Tumepgwa mabomu ya machozi kabla ya kuongea na Afande Kova kuna wenzetu wameumia, kweli askar wetu wanahtaji mechi ya majaribio.
Kunawenzetu wavulana wanne wamevamiwa hostle mbali na kuibiwa vtu wameingiliwa kinyume na jinsia na isitoshe Police post ya kigambon wanataarifa za matendo yanayotokea huku lakin hakuna jitihad zozote zinazochukuliwa.
Ukianika nguo nje za mwanafunzi znaibiwa lakini mwanakijiji aziibiwa hayo ndo maisha ya uku Kigambon
 
tanzania bila UKIMWI haiwezekani.
 
inasikitisha sana,ndio maana sishangai majambaz na wezi wakishikwa uchomwa moto
 
Majambazi kutoka upande gani mwa Tanzania ambayo yana taka kutuharibia msimamo wetu sisi wa kugomea ndoa ya jinsia moja,
 
Kazi ipo!sasa hapo mimi sijaelewa,ulinzi gani unatakiwa kwenye hostel hizo?au wanafunzi wanatakaje?kuwepo askari pale kwenye hostel zao au iweje?hakuna walinzi binafsi kwa ajili ya hostels zao?hao majambazi wanafahamika?kwa maana wanajulikana na polisi hawajawakamata?au ni wale wa kustukiza na kuvamia?
 
Back
Top Bottom