Maandamano makubwa ya kudai maji Dar es Salaam

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Katika zunguuka yangu vijiweni Dar es salaam, Wananchi wanahasira kali sana juu ya ukosefu wa maji Jijini.

Wananchi wanasema Maji wakati mwingine yanakosekana kwa wiki nzima.

Kinachowakera zaidi ni kuwa wamekuwa wakitumia gharama kubwa sana kununua maji na hivyo kufanya maisha yao kuwa magumu maradufu.

Wananchi wanasema, Wameivumilia serikali kwenye mambo mengi sana ikiwemo kuvuruga uchaguzi serikali za mitaa mwaka 2019, Kuvuruga uchaguzi mkuu, Kuwatoza tozo kubwa, Ukatili wa kisiasa, Kuendesha zoezi la wamachinga kihuni. Sasa wanasema hili suala la Maji limewafika shingoni hali ni mbaya.

Inadaiwa Wananchi wanazungumza uwezekano wa kufanya maandamano makubwa ya kudai maji nchini.

Wananchi wanakumbushia kuwa kwenye rasimu ya Warioba MAJI ILIKUWA NI HAKI YA MSINGI ya mwananchi, wanasema kuwa kukataa katiba mpya maana yake ni kukataa wananchi wasipate hayo maji.

Katika mazungumzo yao, wananchi wanasema wanahitaji majibu ya suala la maji haraka sana la sivyo watatoka barabarani na ndoo za maji na magudulia ikiwa ni ishara ya kuonyesha kudai maji!

Wazazi wanalalamika watoto wanaenda shule bila kuoga, Watu wanalalamika wanashindwa kujisitiri chooni vyema sababu ya maji. Watu wanahoji hii nchi ni nchi ya namna gani?

Wakati huo wanahoji, Inakuwaje serikali inatumia matrilioni ya hela kununua ndege halafu inashindwa kujenga miundo mbinu bora ya maji kwa ajili ya jiji la watu milioni 8?

Haya mdogomdogo tutafika. Serikali ijiabdae kwa majibu, Mabomu ya machozi, virungu na bunduki havitoweza kuzuia watu wenye kiu!
 
Andamaneni,tutatoa kipigo cha mbwa koko-Rpc Mroto

Mama anaponya nchi,anaupiga mwingiiiiiiii.
 
Unazungumzia Watanzania sisi au "wa kufikirika"?

Unadhani kuna mtu ataenda kuandamana akiona FFU wenye mitutu na maji ya kuwasha na wajeda wakiwa barabarani "wanafanya usafi"? Labda Tz ingine !!
Kwenye ishu ya Maji, FFU watageuka kama sisimizi siku hiyo.

Tofautisha madai ya kisiasa na yale basic need. Wananchi wengi hawajui au kujali mbo ya kisiasa, lakini yale ya Basic need kama Maji, utawashangaa watakavyogeuka na kuwa watu hatari
 
Tofautisha madai ya kisiasa kama vile demokrasia na madai ya uhai, maji ni uhai. Ukiwa na kiu kimekukaba hayo maji utayafuata hata kambini kwa FFU na hutojali virungu wala bunduki zao
Kila MTU ni kichaa ukitaka ujue ukichaa wake anapokuwa na hasira
 
Kiukweli inasikitisha sana kukosekana kwa huduma ya maji.

Kwanza coverage ya wanaofikiwa na huduma ya maji safi ni ndogo Sana ukilinganisha na mahitaji ya watu na idadi ya watu lakini hata hiyo asilimia ndogo sana iliyofikiwa bado imeshindikana kuweza kupata huduma ya maji ya uhakika throughout the year. Imagine [emoji15]
 
Mbona mlisema mama anaupiga mwingi kukomesha Sukuma gang? Imekuaje tena?
 
Kuoga ni anasa nyie watu wa daslam, hebu tulieni🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…