Maandamano makubwa yaendelea Libya, vijana waingia mtaani

Gaddafi angeishi milele??dikteta huwa na mwisho mbaya na huacha maumivu makubwa..ndio kama hii ya Libya.

#MaendeleoHayanaChama
 
Acha upoyoyo mkuu the man was a hero to his people, sasa hayupo kuna faida uyt libya
 
Wazungu ndio waliondamana wakitaka dikteta Gaddafi aondoke kisha wakaanza kuuwawa kama mende??
 
Thibitisha walitumika na mabeberu, onyesha ni lini mabeberu waliwaambia waandamane kumkataa dikteta wao.
 
Thibitisha walitumika na mabeberu, onyesha ni lini mabeberu waliwaambia waandamane kumkataa dikteta wao.
"Katika makosa ambayo serikali yangu iliyafanya ni kuondoa utawala wa Gadafi, najisikia radhi kwa hilo.....," beberu Obama Barack 2018
 
Thibitisha walitumika na mabeberu, onyesha ni lini mabeberu waliwaambia waandamane kumkataa dikteta wao.
Ila we jamaa unapenda ubishi,tena ubishi wenyewe kama ule ule wa MESSI NA RONALDO, au ule wa LOWASA FISADI AU SIO FISADI.
 
Napata shida kuelewa uwezo wako wa kung'amua mambo especially international politics
 
kweli binadamu hatunaga aibu !

kwani Gadaf bado yuko hai ?😁
 
Hunaga hoja bali vioja.

#MaendeleoHayanaChama
Gaddafi katolewa madarakani na NATO na USA,alitaka kuanzisha benki itayokopesha afrika bila riba,huu ndiyo mrija wa wazungu kunyonya na kutawala afrika,alitaka kuanza na francofone kutopeleka gold reserve France,ndiyo maana France alikua mbele zaidi na hata majasusi waliomkamata na kumuua ni wa France,alitaka afrika iwe na satellite yake ya mawasiliano,mb zisingekua ghali hivi...ulishaona wapi waandamanaji Wana silaha za Vita!?
 
Hehehe heheh daaah... nchi ngumu hii.
 
yote yanayoendelea ktk taifa la libya aliyasababisha mmarekani na washirike wake. laana ishuke juu yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…