Maandamano Ufaransa kupinga kampuni ya Total kujenga bomba la mafuta la Uganda na Tanzania

Wameshindwa kuandamana kupinga uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na viwanda kwao wanakuja kutuingilia huku?
 
Habari imetoka Russia Today 😂😂
 
Chief hangaya.. sini alienda ufaransa kufanya nini.. bora hata angebaki tu.. wakati wa Jpm alikua ashoboki kwenda ulaya na bomba la mafuta lilikua linaandaliwa kujengwa..
 
 
Hao bado Putin hajawanyoosha vizuri, wameshaona kwamba mafuta yataleta utajiri pande hizi si muda mrefu,
WAMESHAJUA WATATUANGUKIA MIGUUNI MUDA SIO MREFU, WAACHE WARUKERUKE TU, PESA WATAILETA AFRIKA WATAKE WASITAKE, WALICHUKUA HUKU NA WATARUDISHA HUKU, TUTAUZA SANA HIZO OIL NA GAS.


Viva Putin, viva Russia.
 
Gesi haina uchafuzi wa mazingira kama mafuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii trick imekuwa inatumiwa sana na Russia. Kila nchi za Ulaya wanapotaka ku invest kwenye energy kunatokea maandamano. Wao huko Russia wanawekeza bila bughudha. Sasa Ulaya iko dependent kwenye energy ya Russia. Na sio ajabu RT kuandika hayo.
 
A ha propaganda. Huo waandishi wa habari kama walivyi wanahabari wengine. Unadhani Uganda ina mafuta mengi kiasi gaini kuizidi Urusi au Nigeria pamoja na nchi nyingine za kiarabu. RT imeripoti tu hao wanafki wanaotaka kutufanya tuendelee kuwa gizani. No more. Na sometimes wanataka terms and conditions za mikataba ziendelee kudidimizwa wakiambiawa unaona watu wanapinga huko, mradi unaweza kukwama.

Uncle Magu, uko wap uje ututee wanyonge...

Wale wa umeanza vzur ila hapo mwshon umeharibu pita hiv, PUA
 
Duuh makubwa haya,kwamba wanauchungu sana na Tanzania au Nini? Hii EACOP itaathiri vipi Mazingira? Na je athari hiyo itaigusa France?
Typically Bongo mindset! Kufikiria nje ya box ni haraka kama muislam kula kibudu! Take your time, tafakari kabla ya kuandika! Anayeharibu mazingira hata akiwa ule North pole, aliye South pole ataathirika! Halafu unaonyesha ubinafsi tulio nao watanzania wengi. Kitu mpaka kiwe kinakuathiri wewe ndiyo uwe na concern! Anyways, haya maandamano ya wanaharakati za mazingira Ulaya yapo kila kona na kila siku. Kwa mfano kuna wanaotaka magari yanayotumia mafuta yapigwe marufuku kabisa baada ya miaka 10 ijayo. Huwa wanafunga barabara na kufanya kila aina ya ghasia. Hata hivyo bomba litajengwa na haya maandamano hayatazuia.
 
tusilolijua wengi, Mrusi anafanya biashara kubwa sana ya gas na mafuta ulaya na ndio wateja wake namba moja...

Kwa sasa mataifa mengi ya Ulaya yanajaribu kutafuta njia mbadala na kuacha kuwa tegemezi kwa Urusi ili wamuue njaa ndio maana hata makaa ya mawe yamepanda bei sasa maana plants za umeme zinazotumia makaa ulaya zimeanza kuwashwa na kila kwenye mafuta duniani kwa sasa projects zinakimbizwa haraka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…