Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
CHADEMA imepata pigo kubwa sana baada ya wananchi kuyapuuza na kuyakataa maandamano yao haramu na yaliyopigwa marufuku na jeshi la police pamoja na kulaaniwa na mamilioni ya watanzania,kutokana na kauli zake zenye kuhamasisha vurugu na machafuko hapa Nchini.
Wananchi wanasema hawaoni sababu wala hoja yenye mashiko ya kuunga mkono na kushiriki kwenye maandamano hayo haramu,.zaidi ya kuona ajenda iliyojificha ya kutaka kuvuruga amani ya nchi yetu na kuchochea machafuko hapa Nchini.
Wana Dar es salaam waliyakataa maandamano haya tangia muda mrefu sana ,ndio sababu CHADEMA wakawa wanatumia nguvu na gharama kubwa kuwaomba watu wa mikoani wasafiri kuja kuandamana Dar. Embu jiulize ndugu yangu inakuwaje CHADEMA wasafirishe watu kuja kuandamana Dar es Salaam yenye watu zaidi ya Millioni 6? Kwanini wanatumia gharama kubwa na pesa nyingi kusombelea watu kuja dar wakati chama hicho hicho kinashindwa hata kujenga ofisi za chama mikoani?
CHADEMA ina Ombwe kubwa sana la uongozi.ndio maana inakwenda tu kama gari bovu linaloendeshwa na kipofu gizani. Chama hakina mwelekeo wala Dira wala mvuto wala ushawishi kwa watu ,hakina uungwaji mkono wala nguvu ya Umma,hakina watu wa kukitetea wala kukipigania.zaidi utakuta wachache wapo huko Twitter wakitukana Mimatusi yao huku wakiogopa kuingia barabarani kuandamana kama walivyokuwa wakiwadanganya wengine waandamane.
Uzuri ni kuwa watanzania wanafahamu utapeli na ubabaishaji wa CHADEMA ndio sababu hawapo tayari kamwe kuwaunga mkono.wanajuwa ni wasaka Tonge, wachumia tumbo na watu wenye kupigania maslahi yao binafsi. Ndio maana kuna wakati walipendekeza uwepo wa wabunge wawili wawili katika kila jimbo.lengo likiwa kuongeza upana wa njia ya wao kupata ubunge ili wakavune pesa na kujilimbikizia, halafu baadaye wakishiba waje kuwatukana watanzania kuwa ni maskini na wanaofanya kazi za kimaskini na zilizolaaniwa.kama ambavyo nyote ni mashahidi wa kauli za Godbless Lema akiwatukana watanzania.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
- LIVE - Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024