Maandamano yaanza kwenye majimbo yote 50 Marekani kupinga utawala wa Donald Trump

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,509
Reaction score
16,734
Waandamanaji maelfu walikusanyika Jumamosi katika miji mbalimbali Marekani kupinga utawala wa Rais Trump, katika maandamano makubwa zaidi tangu aingie madarakani.

Maandamano hayo ya "Hands Off" yalifanyika katika majimbo yote 50 na hata nje ya Marekani, ikiwemo London na Berlin.

Waandamanaji walipinga sera za Trump, kuanzia za kiuchumi hadi kijamii, hasa baada ya kutangaza ushuru kwa bidhaa kutoka mataifa mengi. Boston, watu walichochewa na kukamatwa kwa wanafunzi wa kigeni, akiwemo Rumeysa Ozturk kutoka Uturuki.

London, maandamano yalikuwa na ujumbe wa kupinga sera za kigeni za Trump kama nia yake ya kuitawala na kuichukua Greenland na Canada.

Aidha huko Washington DC, wabunge wa chama cha Democratic walikosoa ushawishi wa matajiri kama Elon Musk ndani ya serikali.

==============================================

Crowds of protesters gathered in cities across the US on Saturday to denounce President Trump, in the largest nationwide show of opposition since the president took office in January.

The "Hands Off" protest planners aimed to hold rallies in 1,200 locations, including in all 50 US states. Thousands of people turned out in Boston, Chicago, Los Angeles, New York and Washington DC, among other cities.

Protesters cited grievances with Trump's agenda ranging from social to economic issues.

Coming days after Trump's announcement that the US would impose import tariffs on most countries around the world, gatherings were also held outside the US, including in London, Paris and Berlin.

Source: BBC​

1743918472988.png

Maandamano hayo yamefanyika kupinga utawala wa kipindi cha pili cha rais Trump pamoja na swahiba yake Ellon Musk.
Waandamanaji hao walishika mabango wakisema hatukutaki na wengine wakisema awekwe ndani .
Tangu mwezi uliopita mali kadhaa za Ellon Musk ambaye alikuwa mfadhili mkubwa wa Trump zimekuwa zikihujumiwa
Tajiri huyo amepata hasara ya mauzo kwa zaidi ya bilioni 100 ambayo yamewashangaza watu wa wall street kwamba anguko la nmna hiyo hawajalirekodi kwa muda mrefu.

‘Hands Off’ protesters rally across US to oppose Trump’s policies​

Hayajaanza leo mbona wanaandamana mara wachome magari ya tesla, watishie wanaoyaendesha. Siku hizi hadi baadhi ya watu wanabandika logo za brand zingine kwenye magari. Wamechoma ahdi magari na kuvamia dealers wa tesla. Yapo tu kila siku
 
sasa ni kwa Trump mwenyewe
 
sasa ni kwa Trump mwenyewe
Watatulizwa tu. Ila trump anawapa tabu na hao mabilionea wanaipata pata kweli maana wanapoteza fedha sana. nasikia soon elon atastep down kutoka kuiongoza doge
 
Kikubwa wawe raia kamili, vinginevyo itakuka kwa viguu na njia.
 
Shida ya hao matajiri wawili ni wanachuki na races nyengine, chuki yao wanaionyesha waziwazi na kivitendo huku wakisahau nchi wanayoiongoza ni mchanganyiko wa races mbalimbali!..
Huyu musk mwenyewe kapewa tu uraia huko wala si mzaliwa!, na anachuki na ngozi nyeusi sijui walimfanya nini kule Africa kusini.

Kwa wanayoyafanya wasipowekewa speed governer sijui tu!, hii ndo shida mfanya biashara kupewa nchi wale maswala ya utawala wangewaachia wengine tu wenyewe wakadili na biashara zao!, wasifikiri watu ni mazwazwa kiasi hicho.. imefikia hatua musk anamshauri trump amuachie yule polisi aliemuua George!..
ile nchi ni kama imeanza kuteua watu wenye maruhani tu!, na heri bado kuna watu wanajitambua lkn kama na huko kwenye majeshi yao wapo wasiojitambua nakujiona wao ndio first and last walahi tunaenda kuingia kwenye vita ya nuclear muda si mrefu!
 
Propaganda, angekuwa na chuki hiyo mkuu huyo trump asingemfanya mhindi akawa kiongozi wa CIA. By the way mimi nakubaliana na trump kwenye mambo ya inclusivity. Huwezi kuwaajiri watu kisa ni shoga, kisa mwafrika, kisa mwanamke. badala yake waajiri watu kwa uwezo wao na ndiyo maana makampuni kama meta yamekimbilia kuanza utekelezaji baada ya sera hiyo kufutwa.
 
Mi sijazungumzia ajira ama watu kuwa favoured, kauli zao na mambo yao yafatilie utaelewa
 
Maandamano hayo yamefanyika kupinga utawala wa kipindi cha pili cha rais Trump pamoja na swahiba yake Ellon Musk.

Waandamanaji hao walishika mabango wakisema hatukutaki na wengine wakisema Trump na Musk wawekwe ndani .

Tangu mwezi uliopita mali kadhaa za Ellon Musk ambaye alikuwa mfadhili mkubwa wa Trump zimekuwa zikihujumiwa

Tajiri huyo amepata hasara ya mauzo kwa zaidi ya bilioni 100 ambayo yamewashangaza watu wa wall street kwamba anguko la nmna hiyo hawajaliona kwa muda mrefu.

​

View attachment 3294615
Trump's brain is resembling shrimp's brain
 
Mi sijazungumzia ajira ama watu kuwa favoured, kauli zao na mambo yao yafatilie utaelewa
Trump chizi ila wamarekani ni machizi zaidi. Nao wanamezeshwa fake news kila uchwao. Jana nimekutana na post moja ikisema kuwa kuna binti alikuwa PA wa musk miaka ya nyuma. Binti aliomba kuongezwa mshahara musk akampa likizo ya wiki mbili aliporudi akamwambia hamhitaji tena so akamwachisha kazi. Comments sasa za wasiompenda wanasema ana roho mbaya, binti alikuwa akimfanyia kazi zake zote akamfukuza hivyo na kalikuwa kabinti kadogo.
Kumbe story ni kwamba, alitaka kumpa cheo kikubwa zaidi kwa sababu kazi aliyokuwa anaifanya ilikuwa kubwa kwa wakati huo baada ya kampuni kukua, so wakaigawa kwa watu kadhaa. binti akakataa alitaka kujiunga na kampuni nyingine, Musk akampa malipo ya week 52, na stocks kama shukrani kiasi kwamba binti hata angeamua kutofanya kazi, angeishi vizuri tu.
Lakini watu wa fake news hiyo sehemu waliacha makusudi maana haendani na wanachotaka.
Ila binafsi hata mimi toka kitambo namwona musk ni tapeli fulani hivi ambaye ni opportunist. Musk ukifuatilia kama kitu hakimfaidishi anakikandia. Ndiyo maana hata mpango wa trump wa kujenga data center ambao ulimhusisha CEO wa Open AI musk aliukandia kisa ana bifu naye.
 
Propaganda, angekuwa na chuki hiyo mkuu huyo trump asingemfanya mhindi akawa kiongozi wa CIA. By the way mimi nakubaliana na trump kwenye mambo ya inclusivity. Huwezi kuwaajiri watu kisa ni shoga, kisa mwafrika, kisa mwanamke. badala yake waajiri watu kwa uwezo wao na ndiyo maana makampuni kama meta yamekimbilia kuanza utekelezaji baada ya sera hiyo kufutwa.
Mimi naona kama vile Trump hana tofauti na hitler. Ukitazama tensions siku zote huanza kwa taifa moja kuanza mambo ya nationalism na kiongozi huwa anafanya akidai na kwa maslahi ya taifa lake na watu wake. Ulaya nashangaa kwanini hawataki kusema, imagine ingekuwa ni china anasema anataka kisiwa fulani kwa ajili ya maslahi ya kiusalama ya nchi yake?
Ila kwa greenland hawataki kusema kuwa Marekani analofanya ni baya wakamkandia kama wanavyoikandia urusi. Wako busy eti kuongeza budget ya kupambana na mrusi wakati US anatishia kuchukua ardhi ya mwana NATO mwenzao.
 
Trump chizi ila wamarekani ni machizi zaidi. Nao wanamezeshwa fake news kila uchwao. Jana nimekutana na post moja ikisema kuwa kuna binti alikuwa PA wa musk miaka ya nyuma. Binti aliomba kuongezwa mshahara musk akampa likizo ya wiki mbili aliporudi akamwambia hamhitaji tena so akamwachisha kazi. Comments sasa za wasiompenda wanasema ana roho mbaya, binti alikuwa akimfanyia kazi zake zote akamfukuza hivyo na kalikuwa kabinti kadogo.
Kumbe story ni kwamba, alitaka kumpa cheo kikubwa zaidi kwa sababu kazi aliyokuwa anaifanya ilikuwa kubwa kwa wakati huo baada ya kampuni kukua, so wakaigawa kwa watu kadhaa. binti akakataa alitaka kujiunga na kampuni nyingine, Musk akampa malipo ya week 52, na stocks kama shukrani kiasi kwamba binti hata angeamua kutofanya kazi, angeishi vizuri tu.
Lakini watu wa fake news hiyo sehemu waliacha makusudi maana haendani na wanachotaka.
Ila binafsi hata mimi toka kitambo namwona musk ni tapeli fulani hivi ambaye ni opportunist. Musk ukifuatilia kama kitu hakimfaidishi anakikandia. Ndiyo maana hata mpango wa trump wa kujenga data center ambao ulimhusisha CEO wa Open AI musk aliukandia kisa ana bifu naye.
kwenye biashara vita lazima sijui wanajikuta ni wanani wale jamaa wawili
 
Back
Top Bottom