Waandamanaji maelfu walikusanyika Jumamosi katika miji mbalimbali Marekani kupinga utawala wa Rais Trump, katika maandamano makubwa zaidi tangu aingie madarakani.
Maandamano hayo ya "Hands Off" yalifanyika katika majimbo yote 50 na hata nje ya Marekani, ikiwemo London na Berlin.
Waandamanaji walipinga sera za Trump, kuanzia za kiuchumi hadi kijamii, hasa baada ya kutangaza ushuru kwa bidhaa kutoka mataifa mengi. Boston, watu walichochewa na kukamatwa kwa wanafunzi wa kigeni, akiwemo Rumeysa Ozturk kutoka Uturuki.
London, maandamano yalikuwa na ujumbe wa kupinga sera za kigeni za Trump kama nia yake ya kuitawala na kuichukua Greenland na Canada.
Aidha huko Washington DC, wabunge wa chama cha Democratic walikosoa ushawishi wa matajiri kama Elon Musk ndani ya serikali.
==============================================
Crowds of protesters gathered in cities across the US on Saturday to denounce President Trump, in the largest nationwide show of opposition since the president took office in January.
The "Hands Off" protest planners aimed to hold rallies in 1,200 locations, including in all 50 US states. Thousands of people turned out in Boston, Chicago, Los Angeles, New York and Washington DC, among other cities.
Protesters cited grievances with Trump's agenda ranging from social to economic issues.
Coming days after Trump's announcement that the US would impose import tariffs on most countries around the world, gatherings were also held outside the US, including in London, Paris and Berlin.
Source: BBC
View attachment 3294615