Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo!
Najua wahusika mpo humu na mnanisoma mara kwa Mara.
Vitisho sio njia pekee ya kutuliza mambo. Njia nyingine ni kutoa mlango wa uani wa Faraja na matumaini.
Faraja kwa maana yakuwa watu kwa mujibu wa Katiba na sheria wanayohaki ya kuandamana na kutoa maoni Yao, kutoa madai Yao, kwa kufuata sheria na wapewe ulinzi na serikali itoe sikio.
Kutokana na nyaya kupigana shot Mara kwa Mara baina ya Serikali na vyama vya upinzani pamoja na Wanaharakati.
Ambapo wanaharakati wanahoja zao.
Bill kujali hoja hizo ni halali au sio halali. Utaratibu wa kuyapa ulinzi maandamano ili Iwe rahisi kuyadhibiti Bila kusababisha madhara.
Lakin pia ingekuwa njia nzuri ya serikali kujisafisha na kile kilichotokea oct29 kuliko kuyazuia.
Yaweza kuwa maandamano ya 7/7 vyombo vya Dola vikajitetea kwamba haijulikani kiongozi wake ni Nani, na wanaharakati wengi wanaogopa kutoa barua za kupata Kibali cha maandamano.
Serikali na vyombo vya usalama havishindwi kuyaratibu maandamano hayo kwa kutafuta viongozi walioupande wao(waserikali). Serikali inavijana wengi. Wapo Vijana ambao wamejitambulisha na wanajulikana kama wanaharakati wenye msimamo mkali Lakini wapo upande wa serikali. Wawatumie hao kama viongozi wa maandamano.
Njia ya mlango wa nyuma hutumika ku clear cache, serikali kujisafisha Lakini pia kushusha mzigo wa wananchi wale wenye kuona wanahaki ya kuandamana kulingana na Katiba.
Kuyazuia Moja kwa Moja ni kuleta tension na kuifanya siku hiyo na zingine zitakazokuwa zinatangazwa kuwa siku za hofu, wasiwasi na baadhi ya shughuli kusimama.
Pia, kwenye Maonyesho ya Sabasaba waandamanaji wanaweza kutumia maeneo hayo kuleta taharuki na vurugu. Jambo ambalo litawapa kazi ya ziada Jeshi LA polisi na wanausalama kukabiliana kwa weledi na Hali hiyo.
Ndio yaleyale ya waliopo na wasiopo kujikuta kwenye matatizo.
Kuingia na NIDA au vitambulisho kwenye SabaSaba haitoshi na haizuii watu kuleta vurugu.
Kusajili watu wanaoingia Lodge na Guest kwa kutumia NIDA haizuii kwa namna yoyote maandamano. Zaidi itahatarisha weledi wa jeshi LA polisi na usalama.
Haitakiwi serikali kushindana na wananchi wake. Wala wananchi kushindana na serikali Yao.
Bila kujali interests za watu. Iwe kweli au sio kweli kwamba wapo wanaharakati wanatumia maandamano kama sehemu ya kazi Yao kuchochea watu kuandamana.
Lakini lazima tukubali ukweli kuwa, wanaochochewa na wao wanaliona tatizo, kwamba tatizo na matatizo yapo. Yanayowapa sababu ya wao kufikia hatua ya kuandamana.
Ugomvi wa ndani unakuwaga sio Mzuri sana. Ni Hatari na hautabiriki.
Taifa ni Kama Familia kwenye nyumba zetu. Ugomvi wa kifamilia ni Hatari sana. Kwani watoto wasioridhishwa na baadhi ya sheria na taratibu wasipozikilizwa huweza kuimega na kuigawa familia.
Ubabe unasaidia kutuliza machafuko. Busara na Haki huleta Amani ya kudumu.
Sasa sio mbinu sahihi kutumia ubabe sehemu ambapo hapajachafuka. Kwani ubabe wakati usio wa machafuko ni kuchochea machafuko.
Nimemaliza
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam