Yeah watatue matatizo ya msingi ya wananchi yanayolalamikiwa.
Kama kwa sasa ni ngumu wawapa faraja na matumaini wananchi.
Kwenye kitabu changu cha SIASA NA UTAWALA; CHESS GAMES
Kinaeleza mbinu za kutawala watu kwa muda mrefu huku wakitolea kwaajili ya serikali Yao.
Mbinu hiyo ni faraja na matumaini ambayo hata kwenye Dini mbinu hiyo inatumika.
Sio ajabu Uislam na ukristo umedumu kwa maelfu ya miaka.
Kwa faraja na matumaini hapo kwa kiwango cha matatizo yaliyopo sikubaliani na wewe japo ni mbinu ya kupoza tu joto kwa muda mfupi.
Kwanini nasema hivi, enzi zetu tukiwa tunakua teknolojia haikua kubwa , unaweza kuona uchumi umeyumba ila akija kiongozi akasema mambo ni safi tu ule ulikua upepo mbaya tuliweza kumsikiliza maana hatukua na means za kuchimba zaidi kupata taarifa .
Kizazi hiki cha teknolojia ambacho kinaongozwa na Gen Z kwa asilimia karibu 55% , wakifuatiwa na Millenials 35% kinajua ukweli na uongo, mbivu na mbichi , nyeupe na nyeusi hivyo wanasaka taarifa nukta kwa nukta utaanzaje kuwadanganya?
Enzi zetu ilikua ni ngumu mtoto wa miaka 20 kuvuka hata mpaka wa nchi kwenda ziara za kibiashara au utalii wa kawaida leo hii hawa vijana wadogo utakutana nao wanapiga hizi safari na wanachakarika unaweza kushangaa wakikwambia umri wao, vijana wadogo wana exposure wanajua uchumi unaoleta matokea na wanajua uchumi duni utawadanganya nini?
Kuna msemo unasema "information is power" huu msemo unaweza kuuona wa kawaida ila una maana kubwa , enzi zetu shahada za kwanza zilikua za kuhesabu leo hii vijana wangapi tena wadogo wana shahada za kwanza hata na za pili?
Hivyo watawala walitakiwa kubadilisha mikakati yao kabla mabadiliko hayajawalazimisha kubadilika.
October 29 wameua maelfu ya vijana , walitarajia nchi ingetulia kimya hakuna ukosoaji je ukosoaji uliisha, jibu ni kwamba waliibuka wakosoaji wengine na bado wataendelea kuwepo tu mpaka mambo yawekwe sawa .
Angalia hii inayojiita serikali inavyopoteza vita mtandaoni pitia na usome maoni kwenye page za hawa watu waliosema wamechaguliwa kwa kura milioni 32 sawa na 98% utapata uhalisia tofauti ndio utagundua tupo zama gani.