Bukhari juzuu ya 8.82.1 na.794-795 uk.520 ni kukata watu mikono na miguu, kuchoma macho yao, na kuwanyima maji hadi kufa baada ya kukatwa miguu na mikono. Angalia Bukhari juzuu ya 8.82.3 na.796 sura ya 4 uk.797; Bukhari juzuu ya 6 sura ya 150 kabla ya na.198 uk.158-159 pia Fiqh us-Sunnah juzuu ya 1 uk.133.
Bila shaka utakubali kwamba hizi ni dhambi nzito sana. Kwa vile Muhammad alifanya hivi, alihitaji sana msamaha. Swali la kidadisi ni hili: "Ni nani hasa anayelipa gharama ya dhambi zako?" Yesu alisema alilipa fidia ya dhambi zetu. Uislam haufundishi kuwa kuna mtu yeyote aliyelipa gharama. Je, dhambi zako zinalipwaje, au Allah anazifumbia macho baadhi ya dhambi na kuadhibu nyingine??
Watu wengine wanaweza kufikiri kuwa uovu hauna madhara yoyote ili mradi mtu anajiita Muislam. Katika karne hii Waislam wanawaua wakiristo na kufanya mauaji ya kinyama kwenye vijiji vyao katika nchi za Sudan, Nigeria na Indonesia. Wakati watu walioitwa wakristo waliwaua Waislam, watu walisema kuwa wanafanya kinyume cha tabia ya Kristo.
Wakati Waislam wanawaua Wakristo, wanaomwabudu Mungu wa kweli, sijawahi kusikia mtu yeyote akisema wanafanya kinyume cha tabia ya Muhammad.
Nisamehe kwa kusema bila kuficha kiasi hiki, lakini mauaji ya watu wanaomwabudu Mungu yanayofanywa na Waislam lazima yaachwe. Waislam wanapohalalisha mauaji haya kwa sababu hata nabii wao alifanya hivyo, watu hushangazwa na nabii wao, na Allah wao ambaye anatengua neno lake, na chimbuko la Uislam.