Bado kauli hii ina ukakasi, nadhani na wewe unajua ila hautaki tu kukiri
Unaelewaje ^usizitegemee akili zako mwenyewe^ na ^usizitumie akili zako^?
Biblia haisemi usizitumie akili zako, bali zisiwe mwongozo, na kumfanya mwanadamu aishi nje ya Mungu.
Ukakasi uko wapi?
Hili si kweli, hata maneno yako yanakiri kwamba binadamu hatakiwi kufuata utashi wake mwenyewe
Ukatoliki ndio umekuwa ukifundisha tangu karne na karne hadi sasa kwamba fikra ya mwanadamu haipaswi kuwa huru nje ya mafundisho ya Ukatoliki.
Kwa maneno mengine, muumini hapaswi kuwa na utashi huru. Kamwe hilo si fundisho la Biblia.
Kila mahali Biblia imeonesha kwamba mwanadamu amepewa uhuru wa kuchagua, ama kumtii Mungu au kufuata utashi wa nafsi yake, kama alivyofanya Shetani.
Uamuzi wa kumtii Mungu na kuishi, au kumwasi na kuangamia, uko kwa mtu mwenyewe.
^Waambie, Kama Mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali
aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya.^ Ezekieli 33:11
ambayo kwa tafsiri nyingine utashi huo unaweza kuhusishwa na kutafuta maarifa na maendeleo.
Kama nilivyojibu kwenye swali lililopita, si kweli hata kidogo kwamba mwanadamu akiwa chini ya mamlaka ya Mungu hawezi kupata maendeleo na wala kufanikiwa.
Kinyume chake, msingi wa maendeleo na mafanikio ya mwanadamu hutegemea kujiweka kikamilifu katika usimamizi wa Muumba wake.
Maisha ya Ibrahimu, Daudi, Sulemani, na wengine wengi wacha-Mungu katika historia huthibitisha hilo pasi na shaka.
Ni kweli Shetani anaweza kumpa mtu utajiri na mafanikio (ya muda), lakini haina maana kwamba kuwa chini ya utawala wa Mungu ni kuchagua umaskini.
^Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao siku zote, wa kunicha, na kushika amri Zangu zote siku zote, wapate
kufanikiwa wao na watoto wao
milele!^ Kumbukumbu la Torati 5:29